Tusitishane: Hakuna maisha baada ya kifo!

Ukisoma Biblia agano la kale linataja kufa kama kuingia kwenye shimo la giza, hakuna kuminya maneno.

Mungu alipoamua kuwa Musa utakufa tena alimwambia unaenda kulala na baba zako hakumwambia kuwa nitakufufua na kulingana na Bibilia Mungu alimzika huko msituni, Mungu angeweza kuondoka naye ila hakuondoka naye.

Wote waliomtumikia Mungu sana kama Yoshua, Samwel na wengine wengi walikufa walizikwa bado miili yao iko au wameshakuwa udongo.

Tuseme Mbinguni kinachoenda huko ni roho, Eliya alikwenda Mbinguni mzima mzima sawa ila roho ya Eliya iliirudi ikazaliwa kwa Yohana Mbatizaji, moja ya ushahidi kuwa Mbinguni hakuna sehemu yao.

Henoko yawezekana ni yeye tu aliye hai huko Mbinguni maana yeye aliondoka na Mungu, soma Biblia.

Agano jipya mambo mengi ni ya kutu please kututia moyo,

Bwana Yesu alisema naenda kuwaandalia makao kisha nitarudi nije kuwachukua, lini ?

Bado anaanda, maana kwamba Mbinguni hakuna kitu yuko Mungu Mkuu, Walio hai wanne (kina nani?), wazee 24 (wazee gani?) na malaika wengi,

Ngumuuu Mshana Jr
 
Kama hakuna maisha baada ya kifo ina maana waovu na wadhalimu wote waliotesa binadamu wenzao hawatapatiwa hukumu yao. Ni vigumu sana kuamini jambo kama hilo.
Maisha baada ya kifo ni hadithi zakufikirika tu

Mara sijui kuna adhabu ya kaburi kuudanganya umma kua malaika anakuja kaburini na mijoka kukupa adhabu eti na watu kweli wanaamini......ni ujinga tu
 
Kama hakuna maisha baada ya kifo ina maana waovu na wadhalimu wote waliotesa binadamu wenzao hawatapatiwa hukumu yao. Ni vigumu sana kuamini jambo kama hilo.
Kwaiyo wewe furaha yako waovu wakateseke.ni mpumbavu pekee ndie anaeweza kuchoma mtoto wake mtoto umzae wewe tena uue utakuwa na akili wew
 
Huu msemo "maisha baada ya kifo" inabidi uwe unafafanuliwa vizuri na kukumbushwa kila wakati. Uzuri kwenye nyumba za ibada huwa wanaufafanua sana, labda huwa hatuelewi au hatuhudhurii.

Kuna wanaodhani "maisha baada ya kifo" ni kuendelea kuishi (kwa hali yoyote ile) baada ya kufariki hapa duniani (wanasema unaingia next phase). Wakimaanisha ulimwengu hauna mwanzo wala mwisho yaani upo upo tu! Na hii ndio shabaha ya ibilisi kututeka kifikra.

Pia kuna "maisha baada ya kifo" kiimani zaidi. Hapa unaamini kuna Mungu Aliyemtoa Mwanae kwa ajili yako upate uzima wa milele. Yaani hata ukifariki(lazima ufariki) basi tumaini la kuishi tena linakuwepo kupitia Huyo Mwana (ikiwa ulishika mafundisho Yake). Kwa maana Amesema Yeye Ndiye Mwenye funguo za kuzimu,mauti inamtii Yeye! Na Yeye Ndiye 'reference' maana Alikufa lakini Akafufuka na hadi sasa Anaishi.

Sasa basi kuna mauti ya milele na uzima wa milele. Sote tutakufa, tutafufuliwa kwa ajili ya hukumu. Hapo kila nafsi itapata ujira wake, mauti au uzima. ( huwezi kuelewa haya mambo km huamini ktk Mungu na uwezo Alionao)

Ibilisi anajitahidi kupotosha kua kuna maisha baada ya kifo kwa mazingaombwe mbalimbali, km vile kumwagia kaburi maji, sala za wafu, yale maswala ya kujifanya unaongea na roho zilizokufa zamani, zile hadithi za 'reincarnation' nk.

Kiufupi mtu akifa hajui lolote, hana hisia tena, kumbukumbu zake zimefutika! Ni suala rahisi tu kuelewa labda ujiweke mwenyewe kwenye mikanganyiko.
 
Kama hakuna maisha baada ya kifo ina maana waovu na wadhalimu wote waliotesa binadamu wenzao hawatapatiwa hukumu yao. Ni vigumu sana kuamini jambo kama hilo.
Hii inakuja pale ambapo ume assume kua baada ya kifo kuna jehanam na pepo.

Na bahati mbaya huwezi thibitisha hiyo assumption kwa fact
 
Kwanza unatakiwa ukiri ya kuwa wewe ni muongo na huna ushahidi juu ya hili ulilo andika, kisha mengine yafate.

Acheni ujinga.
Ha ha ha!
Kwanza unatakiwa ukiri ya kuwa wewe ni muongo na huna ushahidi juu ya hili ulilo andika, kisha mengine yafate.

Acheni ujinga.
Ha ha ha! Mkuu kila mtu abaki na ujinga wake.. kukujibu nilishakujibu Kama hujaelewa hilo sio swala langu.
 
Sisi kwenye maandiko yetu tumeambiwa tuangalie mfano wa mbegu, inakufa inaoza then mmea unazaliwa na maisha yanaanza upya...

Binafsi naamini kama Sikuwahi kuwa kitu na nikawa, bac hata nisipokua kitu nitakua tena kwa nguvu za yule aliyenifanya kua mara ya kwanza.
 
Mimi nimechukua point yako unayosema una ujinga wako kwahiyo ujakosea wewe ni mjinga kwahiyo subili ukifa bila kumpokea Yesu kuwa mwokozi wako ndio utaelewa
 
Umeielewa sivyo. Uhai unaanza ukiwa tumboni. Kabla ya hapo hakuna uhai
 
Maisha baada ya kifo ni hadithi zakufikirika tu

Mara sijui kuna adhabu ya kaburi kuudanganya umma kua malaika anakuja kaburini na mijoka kukupa adhabu eti na watu kweli wanaamini......ni ujinga tu
Rejea #15
 
Mzee umemaliza mada yote.
 
Vp kuhusu elia na musa kumtokea yesu wakati tunajua musa alizikwa mlimani na elia alirudi kwenye mwili wa yohana .yohana yeye hatmq yake ni ipi
 
Vp kuhusu elia na musa kumtokea yesu wakati tunajua musa alizikwa mlimani na elia alirudi kwenye mwili wa yohana .yohana yeye hatmq yake ni ipi
“Watakatifu walio mbinguni ninaomaanisha hapa ni Henoko na Eliya, ambao walipaa mwili na roho kwenda mbinguni, na Musa; ambaye alikufa, hata hivyo hakuzikwa na mtu yeyote, baadaye Yesu alikuja akamfufua na kwenda naye mbinguni (Yuda 1:9). Watakatifu wengine walio mbinguni sasa ni wale waliofufuka wakati wa tetemeko kipindi Yesu anakufa.)
 
Maisha baada ya kifo ni hadithi zakufikirika tu

Mara sijui kuna adhabu ya kaburi kuudanganya umma kua malaika anakuja kaburini na mijoka kukupa adhabu eti na watu kweli wanaamini......ni ujinga tu
Tuthibitishie ya kuwa hakuna haya yote na utuambie ya kuwa umejuaje kama hizi ni hadithi za kufikirika.

Angalizo, usilete dibaji na kupoteza muda.
 
Tuthibitishie ya kuwa hakuna haya yote na utuambie ya kuwa umejuaje kama hizi ni hadithi za kufikirika.

Angalizo, usilete dibaji na kupoteza muda.
Kilichokufa hakina sense ya kupata maumivu hivyo habari za kusema kuna mateso ayapatayo marehemu kwa dhana ya adhabu ya kaburi itolewayo na malaika ni utapeli mtupu

Pia kilichokufa kinaoza na kikioza biashara inakua imeishia hapo, sasa huo muendelezo wa maisha ya mbeleni unaupatia wapi kwenye kitu kilicho oza ambacho hata mabaki yake kuyapata ni ngumu hata kwa carbon 14 na DNA?

Pia kuna watu wengi hufa vifo ambavyo huwapukutisha mazima kiasi hata maiti huikuti, mfano mtu kafia kwenye moto kaungua hakuna sehemu ya mwili uliobaki salama yani familia inaweka msiba tu ila hakuna mazishi maana chakuzika hakipo. Huyo malaika anaekuja na mijoka kaburini anapataje access ya kuwaadabisha watu kama hawa ambao hawana kaburi ila wamekufa

Hizi ni myths tu ambazo waarabu walikaa chini na kutafakari ni namna gani ya kuwa indoctrinate mapimbi na ndio maana huwezi kuzitetea kwa facts bila kuleta quotes za kuran hapa
 
Hata mimi naamini hivyo, ukifa, umekufa, you are gone, done, finito, nothing, the end...

Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...





Cc: mahondaw
 
Rejea #15
Uwe unajaribu kusoma kwa ku reason angalau, hiyo post sio kwamba sijaiona nimeiona ila ni bonge ya ridiculous

Amesema hizi habari zipo katika mfumo wa imani, maana yake huyu anatufunga tushindwe kujadili mambo kwa facts na kututaka tukubali tu any claims as long as ni imani

Amesema swala la maisha baada ya kifo halitambuliki kwa milango ya fahamu ila kwa bahati mbaya hajatuambia ni utambuzi wa njia ipi utumikao kutambua maisha baada ya kifo na amejua hilo kwa kutumia mfumo upi wa ufahamu kwamba mfumo wetu huu hauwezi kuyajua haya?

Bila shaka atakua amesoma vitabu vya dini vyenye hayo malezo, sasa kusoma kuna husisha macho na ufahamu kupitia mfumo mzima wa ubongo ambavyo yeye amevikataa kua haviwezi kukufikisha kwenye kujua maisha baada ya kifo, sasa ye amejuaje?

Pili, kama hii ishu ni imani inayotegemea mfumo wa dini na tunaona kuna dini zaidi ya maelfu ambazo kimsingi zinapishana kwenye hiyo imani ya dhana ya maisha baada ya kifo kiujumla. Kwanini imani hizo zipishane wakati source yake ni moja (isiyo tumia milango ya fahamu)

Haiwezekani imani ya kiislamu kuhusu maisha baada ya kifo iambatane na adhabu ya kaburi halafu kwa ukristo ikawa ni opppsite kua utafufuliwa na yesu halafu imani zote hizi ziwe sawa

Kama imani ingekua njia sahihi ya kujua ukweli wa kitu basi leo hii kungekua na dini moja na mungu mmoja au kila kitu kingekua sahihi as long as kitawekwa katika mfumo wa imani, imani sio njia sahihi ni utapeli tu na ndio maana imani flani ni kipingamizi wa imani nyingine kutoka dini fulani

Huyo mdau kasema kua kwasababu jamaa haamini kuna mungu basi hawezi kusadiki habari zake. Well hapa hatuko katika zama za kuamini, zama za kuamini zilishapita now tuko katika zama za kujua kwa facts so nami pia nakubaliana na huyo mdau ambaye haamimi mungu.

Kwanini niamini mungu yupo kama kweli yupo? Huyu mungu ni stori kama ilivyo habari za maisha baada ya kifo na ndio maana amefuchwa kwenye pazia la imani ili kuwaepusha watu wasiufikie ukweli
 
Jibu swali nililo kuuliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…