Tusisubiri Mtetezi suala la Pensheni atoke nje ya wafanyakazi!

Wana JF,
Ningpenda kujua kama chama changu amabacho ndicho kinachotetea wanyonge nchi hii kimeshatoa tamko rasmi juu ya jambo. Tunaomba watuback up sisi wafanyakazi katika kupinga dhuluma hii tunayofanyiwa na serikali hii dhuluma ya magamba.

Life span ya mtanzania ni miaka 45, wewe unaweka sheria ya kumpa mafao yake baada ya miaka 55. Ukimwi unaenea kama nini, na magonjwa yanatuua kila siku. Kwani serikali imeingia ubia na Mungu kwamba kila mtu ni lazima aishi miaka 55.

Je kama wabunge wamepitisha hiyo mbona hawakusema na wao wasubiri mafao yao wakimaliza bunge?
Naamini muda si mrefu viongozi wetu watatoa tamko kali.

Naomba kuwakilisha.
 
Mkuu hivi wabunge walilala wakati sheria hii inapitishwa?
Wote walipoingia bungeni walihongwa pesa ya kununulia magari sh 90m. Kuna habari za uhakika kwamba pesa hii ilikopwa kwenye hii mifuko ya hifadhi ya jamii. Hapa humsikii Filikunjombe wala Lisu akisema kitu. Kwenye hili ni solidarity forever.
 
Jamani pamoja na hasira tulizonazo, jana nilisikia KITU cha ajabu. Mbunge mmoja alisema kwamba katika sheria ya mafao waliojadili na kuipitisha bungeni, hicho kipengele cha kuzuia mafao ya kujitoa na kusubiri miaka 55 na 60 ndipo uchukue mafao hakikuwemo kwenye huo muswaada wa sheria. Yeye anadhani eti hivyo vipengele vimechomekwa baadae.

Akadai kwamba atathibitisha madai yake kwa kuleta HANSARD YA BUNGE.

Wafanyakazi wenzangu tuelimishane, Je madai ya huyo mbunge ni ya kweli au ndiyo alikuwa anajikosha.

Tunaomba wabunge ambao ni wana JF (although ninajua > 90% wa wabunge wa JMT husoma JF) eg Zitto Kabwe, Mnyika, Kigwangallah, Lameck Mkumbo Madelu, etc mtuelezeni juu ya UKWELI wa jambo hili.
 
Kwa kuwa wawakilishi wetu fibuka, tucta, tamico , trawu, chodawu, talgwu na wengine wamesaliti wafanyakazi wote wa nchii kwa kitendo chao cha kukukabali sheria dhalimu ya kupoka mafao ya wafanyakazi na kuyahonga kwa serikali, basi naomba wafanyakazi wote tujitoe kwenye vyama vyetu. Vyama hivi vinaishi kwa michango yetu na kwa hili la sasa la kuzuia mafao ni kwamba wamehonga mafao yetu ccm na ikulu.

Kuwawajibisha kwa usaliti huu, kuanzia mwezi wa nane makao makkuu ya vyama vya wafanyakazi nilivyovitaja wasipate tena michango toka matawini mpaka rushwa waliyo kula ili watusaliti iwatokee puani au la wawaendee bwana zao warekebishe sheria hiyo.
Jinsi ya kuwanyima michango: Wafanyakazi wote mahala pa kazi yaani tawini, pitisheni azimio kwa saini kwenye form kisha mzipeleke finance department kwamba hamtaki makato yenu yaende makao makuu ya chama chenu tena.
Wakirekebisha usaliti huu, ndipo muwafungulie mfereji wa michango yenu. Haiwezekani watu wawe wanalipwa kufanya usaliti. Yuda alilipwa kwa usaliti akaambilia kifo kwa kujinyonga. Nicholaus mgaya na wengine tuwanyonge kwa kuwanyima michango. Watakwenda kwa bwana zao sisiem na kuwapigia magoti.

Nawasihi sana wenzangu, tuanze kwa kuwawajibisha makao makuu ya vyama vyetu waliohongwa chai ikulu kisha wabunge wote wapuuzi, tena ni wote bila kuchagua chama. Wabunge wote ni wasaliti. Kuna faida gani ya kuwa na mbunge kama mchawi maji marefu? Anajua kitu zaidi ya uchawi?

Tuanze na vyama vyetu vya wafanyakazi, 2015 tuwanyooshe ccm , chadema na vyama cyote vya siasa. Kama ni rais bora awe mbwa kuliko mwana chama wa ccm , chadema, cuf au nccr. Wote wezi wa haki za mtanzania.

Mimi siku zote nasema hawa wanasiasa ni wajinga sana na hawajui wapi wanakwenda. Kwanza hawa jamaa wanaotamba na siasa uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana ndo maana hata mashuleni tulikuwa tunawakimbiza sana. Utaona wengi ht matokeo yao ya shule si mazuri na waliishia kusoma vitu vya ajabuajabu tu leo hii ndo wanataka kutuongoza na kutuamlia nini cha kufanya. Wameshindwa kukusanya mapato migodini, bandarini na kodi nyingine, matokeo yake wanafikiria pombe, sigara, PAYE zitaongoza nchi, wameona ahadi hazitekelezeki na chama kinapoteza dira wakaibuka na pesa zetu ili warudi madarakani na kuendeleza wizi wao. Ukisoma ule mswada utaona kuna kiswahili na kiingereza, sasa kwenye kiingereza wanaandika mtu atachukua michango yake upon retirement na juu mwanzoni mwa paragraph wamedifine retirement to be 55 or 60yrs. Hakuna sehemu wamesema mtu haruhusiwi kuchukua pesa yake, ila walificha hilo neno na baada ya wabunge wetu kutoliona na kuelewa wao wamelichukua na kulitolea ufafanuzi sasa, ht hao wabunge ukiwauliza watakwambia hicho kitu hawakijui ila walipitisha bila kujua. Na sehemu ya kiswahili wameandika utachukua pesa yako baada ya kustaafu ila hawajaandika maana ya kustaafu. Sasa km mimi naacha kazi na kukurusishia kadi yaki nikiwa na miaka 35 inamaana mimi sio mwanachama wako na sina uhusiano na wewe, niache niondoke zangu ya nini unataka kukaa na pesa zangu wakati mimi nazihitaji na sijakuomba unitunzie? Kwani wao ni bank mpk wang'ang'anie pesa zetu? Mbaya zaidi huyu rais na timu yake muda wao ndo umekwisha hivyo sasa inakuwaje wao waamue kuliingiza taifa ktk mgogoro mkubwa hivi na wao wanaondoka? Wanadanganya eti ni kwa manufaa ya wanachama, Mkapa alikuwa hana akiri aliyeanzisha mifuko yote hii ila Kikwete ndo clever wakati kila mtu anajua uwezo wa Ben Mkapa? Hapa mmechemka na hiyo sheria haitofanya kazi kwani Bisimba na TUCTA wanaenda mahakamani so mpk kesi iishe ndo sheria itaanza km kisingizio chenu cha siku hizi cha "KESI IPO MAHAKAMANI".
 
"Ukicheka na Nyani utavuna mabua". Usemi huu unazidi kudhihirika katika nchi yetu hasa katika suala la wafanyakazi kuendelea kukandamizwa bila ya kuwa na mtetezi. Wafanyakazi hawa ndio wamekuwa walipa kodi kwa serikali kwa asilimia 100 kuliko chanzo kingine chochote cha kodi. Hili serikali imefanikiwa kuwanyamazisha wafanyakazi.

Sasa kanakwamba hilo la kodi halitoshi, Serikali imeamua kuwatikisa tena wafanyakazi kwa kuwalazimisha kusubiri pesa zao za akiba mpaka ufike umri wa kustaafu. Hivi kwanini serikali inapanga maisha ya mtu mmojammoja. Kesho itakuja na sheria nyingine ya matumizi ya mshahara.

Kwa hili tafadhali wafanyakazi wasitarajie kupata mtetezi asiyekuwamfanyakazi na anaeumizwa moja kwa moja na sheria hii. Sheria hii imepitishwa Bungeni kwa urahisi kabisa pasipo kuzua mijadala na ndio maana watanzania wengi wameshtuka na kushangaa kusikia sheria hiyo ilipitishwa muda mrefu Bungeni, April mwaka huu.

Kama ni suala la kuweka akiba, mfanyakazi wa leo anajua kuna mabenki mengi nchini atakwenda kuhifadhi pesa za watoto wake. Kumekuwa na utetezi potofu juu ya sheria hii kuwa itasaidia mfanyakazi kukopa Nyumba. Je, mahitaji ya wafanyakazi ni nyumba tu? kuna ambao tayari wameshajenga kwa njia wanazozijua wenyewe na mahitaji yao si nyumba tena.

Na kama suala ni kumlinda mfanyakazi asijekudhalilika uzeeni, basi suala hili liwe ni hiari ya mfanyakazi mwenyewe lakini kwa wanaotaka kuchukua pesa zao, waachwe wachukue. Kwa hili serikali ndio inajifanya kuwajali wafanyakazi, mbona wazee wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mpaka leo wapo wamelala pale makao makuu ya stesheni Dar wanaokoteleza vyakula, serikali haiwaoni? Mafao yao yako wapi?

Wafanyakazi ujumbe ni kuwa "ukicheka na Nyani utavuna Mabua".
Umesema kweli mkuu,kwanza kodi katika mshahara ni kubwa kuliko mchango wako katika hiyo mifuko ya pensheni,pili kweli tunahitaji kiongozi wa nchi mfanyakazi hata awe wa zamani atakuwa na uchungu wa wenzake na siyo mwanasiasa hawana uchungu na wafanyakazi hawa,tatu ule usemi wa kura zao sizitaki unajirudia sasa nakumbuka usemi huu uliumiza wengi mwaka 2010 kwa kuwa hana la kupoteza tena kwa wafanyakazi anafanya kweli.ni kweli kabisa "ukicheka na nyani utavuna mabua"inabidi jambo fulani liandaliwe kuonyesha hasira zetu juu ya haya maovu kwa wafanyakazi,mbona hawaweki sheria kuwabana hao waliobainika na matrilioni huko nje ya nchi badala yake wanambana mfanyakazi maskini wa nchi hii mvuja jasho.
 
Hivi mimi mpaka leo najiuliza hivi ni kweli hii sheria imepitishwa Bungeni? Kama imepitishwa kweli bungeni naanza kuwa na shaka na wabunge wote bila kumuondoa hata mmoja hata wale niliowaamini wa upinzani.

Ilikuwaje ikapita kimyakimya tusisikie hata kelele kwa akina Mnyika, Mkosamali, Filikunjombe, Lissu wote kweli mkanyamaza kimya watanzania tunapitishiwa sheria ya kutuumiza kiasi hiki?

niko kama wewe, hata sisadiki hili jambo, mie naamini litakuwa limechomekwa, kwa nini limeibuka sasa, inawezekana kabisa halikuwemo, ila kama lilikuwemo na likapitishwa basi inawezekana labda uchawi ulitumika au inawezekana walihongwa wote? au wao hii sheria haiwahusu wabunge ila ni watumishi wengine tu
 
mimi hapa kazi yangu ni "dei waka", nimefanya kazi kwa mkataba wa mwaka then ukaisha sasa inakuwaje nisubiri miaka yote hio kwa ajili ya kupata shs.300,000 ya leo baada ya zaidi ya miaka 30 ijayo, jamani hio si itakuwa ni kama shs.300 ya leo? je hio laki 3 itanisaidiaje kupata huo mkopo wa nyumba? au tutakuwa tunachangia wengine wenye ajira za uhakika? TUCTA amkeni tusiishie kuimba solidarity forever, hio solidarity ionekane wazi sasa kila sehemu - sehemu za kazi, barabarani, mitaani, kwenye vyomba vya habari na kila sehemu, shime jamani, mgaya upo wapi?
 
Kuna siri au mkakati gani katika sheria hii? kwanini wabunge wajipendelee kwa kulipwa mafao yao mara baada ya kustaaafu? kwanini wasisubiri hadi miaka 55 au 60 kama wengine?

Jana tu magazeti yaliandika kwamba serikali imekopa pesa nyingi sana katika mifuko hii ya jamii na imeshindwa kurejesha mikopo pamoja na riba hizo. mikopo hiyo ni pamoja na ujenzi wa UDOM, Nyumba za polisi, Ofisi za serikali n.k Nachelea kusema sheria hii hailengi kumlinda mwanacha wa mfuko hii bali kuilinda serikali dhaifui iliyoshindwa kufanya marejesho ya mikopo ndani ya mifuko hii. kuto kulipa wafanyakazi mafao yao pindi wanapoacha kazi ni serikali kutaka kuwa na fedha za kukopa bila PRESHA kwani ina presha ya kushindwa kulipa madeni iliyonayo hadi sasa!

Kwanini tusiwe kama Nchi za jirani? kwa mfano kule Kenya mwanachama wa mfuko wa kijamii ana haki ya kutumia mafao yake kama dhamana ya mkopo katoka mabenki. hili linafanyika wakati wowote ili maradi tu mwanachama huyo anasifa ya kukopesheka!

Uchumi wetu ndo upo alijojo sasa hivi ita kwaje hapo miaka ya mbleni kama tutanyimwa fursa ya kutumia michango yetu pindi tunapoaachishwa au kuacha kazi mapema? Je michango hiyo itakuwa na riba kwa wakati wote wa kuisubiria?

Hii sheria haifai hata kidogo, kwanini pia imnalenga kutoa unafuu kwa wafanya kazi wa migodini na wabunge tu?

Mifuko si lazima iwekeze hapa nchini inaweza kuwekeza hata nje ya nchi hasa katika nchi zenye amani na utulive kama Ulaya na Asia.

Utawekezaje katika serikali dhaifu inayo shindwa hata kumadi Chenge vile vijisenti hata mara baada ya change ya rda kurudishwa!

NATUJA KUTOKUWA MWANASHERIA HAPA PANGEKUWA PATAMU SANA KWANGU HATA KAMA WANGE NI ULIMBOKA POTELEA MBALI. UPUUZI HUU HADI LIKI? PUMBAFU ZAO WANASHERIA WANAOCHEKELEA UPUUZI HUU WA MICHEZO MICHAFU SERIKALINI!
 
1. Serikali inataka ijihakikishie matumizi ya hizo hela zetu
2.Mifuko ya pensheni imefilisika kwa kuwakopesha serikali na kujifanya wana fadhili miradi .
3.Huko kuwajali wafanyakazi wanataka kuanza leo? sikuzote walikuwa na hela kwanini wasiwasaidie wafanyakazi wakaishia kujenda majengo makubwa wanapangisha hela wanakula wao.
Miaka 55 wanajua wengine watakuwa wamekufa na kuna watanzania familia zao hazinauelewa wa hiyo mifuko so watazichukua wao mwisho wa yote.
Huu ni wizi na mabavu yakimachomacho, mwisho hata hao watoto watatakiwa kufika miaka 55 ndo wapewe.
IKIWEZEKANA WAFANYAKAZI WOOOOTE NCHI NZIMA TUANDAMANE NA TUGOME KUFANYA KAZI MPAKA WATUACHIE PESA ZETU.
 
niko kama wewe, hata sisadiki hili jambo, mie naamini litakuwa limechomekwa, kwa nini limeibuka sasa, inawezekana kabisa halikuwemo, ila kama lilikuwemo na likapitishwa basi inawezekana labda uchawi ulitumika au inawezekana walihongwa wote? au wao hii sheria haiwahusu wabunge ila ni watumishi wengine tu

Katika hili nimeanza kupoteza imani na wabunge wote wa Tanzania bila kujali chama,mpaka hapo nitakaposikia
kauli zenu wabunge kuwa mlipinga juu ya hili au kipengele hiki kimechomekwa hakikuwemo wakati mnapitisha
sheria hii.Please Mnyika,Zitto ,H Kigwangala answer me,where were you???????
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Wakuu nimeshangaa sana kusikia eti hii kitu imepitishwa toka April! Bunge hili hili ambalo tunasema watu wamekuwa macho and very vocal? Siamini kabisa.Nini kilitokea? Halafu nimesoma utetezi wa CEO wa SSRA juu ya upitishwaji wa hii sheria kwamba zitatungwa kanuni ambazo zita-address yale yote yanayolalamikiwa na waathirika.Bado utetezi wake haujaniingia akili aslan! ''Workers, Stand Up, Unite, and shout 'foul'!
 
Kwa masikitiko makubwa jana nilenda PPF nikakutana na Branch Manager wa tawi husika mwenyewe anaonyesha kukatishwa tamaa sana na uamuzi huu wa serikali kusitisha utaratibu wa mtu kupata mafao yake pindi atakapo achishwa kazi.
Alikosa cha kusema hadi ananiuliza mimi sasa tufanyaje kupinga hili?

Ki ukweli watanzania tunaburuzwa sana zaidi ya ng'ombe wanavyopelekwa machinjoni.
 
  • Thanks
Reactions: Aza
haya sasa, tumelalamika weeee, utafikiri ni wajinga fulani hivi ambao hawajui la kufanya.

Sasa ni wakati wa kuweka mipango na mikakati, halafu utekelezaji.

Viongozi wa maandamano na migomo tuteuwe ifuatavyo.

A- Kituo cha haki za binadamu

B-CHama cha wafanyakazi TUCTA

C- Viongozi kutoka vyama vyote

D- Viongozi wa DIni

Kumbukeni kuwa hii haina itikadi ya Siasa na Haina dini.

Watu wote ni waathirika wa hili jambo bila kujali dini yako wala itikadi.

Msiogope, watakuja baadhi ya vibaraka kutukatisha tamaa na kutuvuruga.

Karibuni katika mjadala kupanga mikakati.

Kama ni kulalamika, usichangie hapa

shime watanzania wenzangu, haya twende mbele na maandamano, Bunge limeshindwa
 
na ambavyo hatuna ushirikiano sasa?kama tumechanjiwa ivi.. labda kuna muujiza unaokuja kuaifuta hii sheria ya pensheni mana imeanza vuuuu tukajua labda ipo katika hatua na itatekelezwa baada kumbe inaaza on-spot!! aisee
 
Katika hili nimeanza kupoteza imani na wabunge wote wa Tanzania bila kujali chama,mpaka hapo nitakaposikia
kauli zenu wabunge kuwa mlipinga juu ya hili au kipengele hiki kimechomekwa hakikuwemo wakati mnapitisha
sheria hii.Please Mnyika,Zitto ,H Kigwangala answer me,where were you???????

Inawezekana hata hao waheshimiwa uliyowataja watakuwa nao wanashangaa! Hebu tusubiri mjadala wao utakavyokuwa wakati wakijadiri hili suala
 
Back
Top Bottom