barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Hii ni moja ya barua iliyoandikwa na Padre kwa Papa ili aweze kumruhusu kuachana na useja.
Naona watu wanachanganya sana hapa,wanashindwa kujua kuwa kwa mujibu wa Sheria za Kanisa,"Canon law 290" mcleri yoyote,awe askofu,padre au shemasi anaweza kuachana na upadre,akawa mlei na baadae kuondolewa useja na kuruhusiwa kuoa.
Upadre is just a descpline and not a dogma in catholic's way of life.Kuna namna padre anaachishwa kama adhabu hii inaitwa kwa kilatini kama "ad poenam" na kuna ile anaachishwa kama "favour" sbb ya afya (hili ni neno pana) kama kurukwa akili nk,hii inaitwa kwa kilatini "ad gratia"
Kuna kitu inaitwa "defrocking" au "unfrocking".Hii ni hali ya padre kuachishwa upadre kwa sababu ya nidhamu,criminal Convictions,kukana doctrine au dogma of the catholic church,kuzaa watoto nje ya ndoa na ikagundulika na kuletwa malalamiko kuwa ana watoto anaoishindwa kuwatunza na kupata upendo wa baba.
Hali hii hufanya kanisa "kumpokonya" padre husika madaraka ya kipadre,lakini "upadre" wake huendelea kuwa ulivyo,kwana wanasema Kuachishwa huku hufanywa na Papa kupitia askofu wa jimbo la padre husika.
Na kuna kitu kinaitwa "Laicization".Hii Padre yoyote anaweza kuacha kwa kufuata utaratibu sahihi.
Huandika barua kwa askofu kwenda kwa Papa na kuomba kuachana na upadre,anajitenga na kiapo cha upadre na kazi za kipadre kama kutoa sakramenti ya ubatizo,kumunio,kitubio na mpako wa wagonjwa.Baada ya muda Papa humjibu na kumuondolea madaraka ya daraja la UPADRE.Padre hutoa sababu za kuacha na zinapimwa kama zina uzito.
Baada ya kuwa "laicized",padre husika anapoteza "title" kama ile ya kuitwa "Father/Baba (wa kiroho).
Hawajibiki wala kufungwa na utaratibu wa "Canonical hours",yaani ile hali ya kuhakikisha anazingatia sala za siku nzima katika mpangilio wa masaa,kuanzia masifu ya asubuhi,misa ya asubuhi,sala ya malaika wa bwana ya mchana (angelus),masifu ya jioni yenye zaburi na antifona,na ile sala ya usiku maarufu kama "completo".(Kwa waislam tungesema suala tano).Sala hizi ni muhimu kwa waumini wakatoliki,lakini ni wajibu wa padre kuzitimiza kila siku.
Haruhusiwi kuvaa mavazi ya kipadre kama casula,amito,stola,chingulumu,alba nk.Kuongoza misa na kuhubiri inakuwa ni moja ya makatazo yake baada ya kuenguliwa.Wakati mwingine huzuiwa hata kufundisha katika vyuo na taasisi za elimu masomo yahusuyo theolojia au mafundisho ya kikanisa hata kama atakuwa na elimu ya kiwango cha Phd.
Hii ndio aliifanya hata Dr Slaa,hii ndio huitwa "Laicization".
Katika mazingira kama ya ajali au mtu akiwa katika hatari ya kufa akiwepo mtu kama Dr Slaa au Karugendo wanaweza kutoa sakramenti kama kitubio,ubatizo na mpako wa wagonjwa kwa sbb ile "sacramenti" ya Upadre haifutiki ndani yake.Wanasema "Once you are a priest,you are always a priest".
Kwa takwimu za Vatican,mwaka 2014-2015 Mapadre zaidi ya 500 dunia nzima waliomba "Laicization" ili kuachana na upadre na kuwa walei na si wacleri.
Hii hulazimishwi kuamini na kuipokea kama wewe si mkatoliki.Hii ni kwa waamini wakatoliki waliokubali na kuamua kukiri imani yao chini ya "Kanuni ya Imani".
Nafikiri tunavyozidi kwenda mbele,kanisa lina wajibu wa kutoa elimu na nafasi kwa walei kupata uelewa wa hapa na pale juu ya baadhi ya mienendo ya kanisa chini ya "Canon Law".Miaka ya nyuma kanisa liliona hatari ya Lugha ya Kilatini kuwa kama Lugha ya mawasiliano na lugha ya ibada katika kanisa lote duniani.
Kupitia "Inculturation" yaani "utamadunisho",kanisa liliamua kuhimiza lugha mahalia kuwa sehemu ya ibada na mawasiliano ya kikanisa.Hapo ndio biblia na maandiko mengi yakawa yanatafsiliwa katika lugha mahalia kama kiswahili ili kurahisha uelewa.Biblia enzi za kale ilisomwa na wateule wachache tu,kiasi waamini wa kawaida hakuwa na ruhusa kushika biblia takatifu na kuisoma na kutafsiri.
Baadae ikaruhusiwa hata wasio na ujuzi na maandiko matakatifu (Scriptures) nao washike biblia na kuisoma.Hapo ndio hata kina Mwanjabili wa Kyera wakaishika biblia na kuanza kutafsiri kwa "hisia" zao na kuanzisha makanisa kama uyoga.
Alilolifanya Karugendo si ajabu,ndio maana na kanisa limeamua kumpa sacramenti ya ndoa.Tunaona ajabu sbb hatujipi muda wa kufuatilia mienendo na sheria za kanisa.Ikumbukwe kuwa Upadre si sheria ya Mungu,bali sheria ya kanisa inayolindwa na "Canon Law 290-293"
Nimeambatanisha barua iliyoandikwa na Padre mmoja (Jina kapuni) mwaka 2003,akimuomba Papa aidhinishe ombi lake la kujiweka kando na Upadre.Baada ya miaka kadhaa,Papa alilidhia ombi hilo na sasa Padre anaishi kama mlei.