Tusipangiane mtindo wa malezi: Jirani yangu kajaribu kunithibiti nisimtandike mwanangu kisa watoto wake hawachapi

Ngoja adedi ndo utaisoma namba,tatizo si LA Mtoto tatizo ni wewe kumfuatafuata,unamchumguza Wa nini?kitanda kinakaa ndani kitandikwe kisitandikwe nani anakiona,atatandika akiwa anaenda kulala(,gari huwashwa kukiwa Na safari) kwanza kwa nini unamzingua kana kwamba aliandika application latter ya kuja huku duniani ili hali ulimleta mwemyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyie ndo wale mababa poa,,sas bila stiki mambo yataenda kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapoenda kuzini nani anakuchapaga,?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mbona sababu zako ni soft Sana. Sorry unawatoto?

Nilitegemea uelezee hasara za kumchapa mtoto, Lakini wewe umeanza kuenda kwenye mada zingine, ulishawahi ona wazazi wanakufuatilia Sana ukishafikisha 18 au 20? Hawakufuatilii kwasababu umekua na unamaamuzi binafsi na wanayaheshimu. Ila ukiwa mtoto wazazi ndio wanaokufanyia maamuzi na kukufundisha kipi Ni sawa na kipi si sawa.

Hebu jikite hapa: kwa nin mtoto asichapwe pindi anapokosea kwa mara kadhaa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwenda21,
Kitu cha kukufurahisha ni kuwa wazazi wenye kufikiri kama wewe wapo wengi sana mkongwe.
Lakini jambo la kusikitisha ni kuwa wazazi wengi wenye kufikiri kama wewe huwa wanakumbuka kuanza kuchunguza watoto wao pindi wanapoona dalili za watoto wao kukosa "malinda", lakini mara nyingi wanakuwaga wameshachelewa.

Usije ukawa miongoni mwao, endelea kushikilia msimamo wako.
 
dudu jeupe, Ninawapenda Sana wazazi wangu, hasa kwa sababu hawakucheka na Mimi nilipokuwa mdogo.

Nakumbuka pindi moja, nikiwa darasa la tatu nilichuka buku ya mama nikijua hajazihesabu. Aisee Jioni yake siji kuisahau kwa kipigo nilichopata, tangu hapo sijawahi kuchukua hata Mia pale nyumbani au kwa mtu yoyote mpaka nimefika utu uzima.

Fimbo zinasaidia Sana, hata Bible imesema ujinga umefungwa kwenye moyo wa mtoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dudu jeupe,
Nyie wazazi wa kanda ya ziwa mnawatendea watoto wenu kama ng’ombe sijui inawasaidia nini kwani mambo yote mabovu yapo huko ikiwa ni pamoja na ukatili mkubwa unaotokana na wazazi kuwaadhibu watoto wao kupindikia. Jirekebisheni kuweni na utu.
 
Tatizo unalo wewe mzazi.
Unajisifia kumchapa mwanao badala ya kumuelekeza pasipo na kuumizana.
Mfundishe kwa upendo mwanao ili apende kufanya hivyo sio afanye by force.

Ukiona huna uwezo wa kumfundisha mtoto bila kumchapa, hiyo kazi haikufai

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata kuchapa Ni kufundisha, na anachapa kwa upendo. Kumbuka alimwelekeza, hakufanya, akamuonya kwa Mdomo, hakufanya, Sasa unataka upendo upi unaousema.

Huoni hapo ilibidi kumpa mapigo, mtoto, Kama kaambiwa amepuuza, amepewa karipio, kapuuza.

Tueleze huo upendo unaousema tuelewe, na kufahamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakuunga mkono mchape mtoto atie adabu achana na hizi familia wababa wanaitwa big dady ni wajinga mno unaweza kuta baba anaangalia sinema ya ngono na watoto kisa ati maisha yamebadilika usiwafiche kitu watoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
....Umetenda Jema. Muache huyo jirani aendelee kukuza watoto watoto wake Kizungu kwa ' kutowakunja Samaki wakiwa wabichi'...!!!!
Kwa kawaida ninapoenda kazini, huwa namwachia mtoto wangu wa kiume mwenye miaka 10 majukumu kadhaa ayatekeleze japo kuna house girl na ndugu zake wakubwa ila na yeye lazima ajisaidie baadhi ya vitu kwa manufaa yake na atusaidie baadhi ya vitu kwa manufaa yetu wote.

Majukumu yake:
1. Kutandike kitanda chake
2. Afue nguo zake
3. Chumba chake kiwe kisafi
4. Akila sahani azioshe.
5. Kufanya homework za mwalimu wa tuition niliyemletea katika kipindi hiki cha corona.
6. Kuaga na kutujulisha anakoenda kucheza, mwiko kucheza maeneo nje ya mtaa wetu katika kipindi hiki kibaya.

Majukumu ya kuwa msaada kwenye nyumba
1. Afagie uwanja asubuhi kwa kupokezana na house girl yani yeye leo kesho mwenzake
2. Kutumwa kununua vitu duka la karibu. mfano mafuta, vocha, n.k
3.Kutoa magugu na kumwagilia maji mboga kila jioni.

Sasa naona dogo anataka kupima upepo kwa kijiko nadhani, kaanza kuwa mvivu wa kutandika kitanda, nguo hafui, anategea zamu ya kufagia, akila haoshi sahani anaiacha tu kwenye sinki aoshewe na house girl.

Juzi tulikaa na wife tukamwambia aache hii tabia kwa sababu ni mbaya na madhara yake ni mabaya akiendelea. Jana kaendelea nikampiga mkwara asirudie ila niliporudi chumba chake hajatandika kitanda na hakufagia asubuhi. Leo kafagia ila hajatandika kitanda na kuna vyombo chini ya kitanda.

Nyumbani kwangu nimepanda miti kwajili ya matunda na kupaata kivuli jua likiwaka, ila pia hii miti ni dawa kwa mtoto anaeanza kuwa na tabia zisizonipendeza,

Nina mti wa mpera, nilikata kiboko cha wastani na kukikarabati vizuri nikakificha, aliporudi huko anapochezaga na wenzake majirani akaja akanisalimia, ile anavyonipita nikamdaka mkono, tukaenda nilipohifadhi dawa yake.

Kwa kuwa nilishakaa naye na kumuelewesha mara ya kwanza, kumgombeza mara ya pili, hii mara ya tatu ilibidi nimpe dawa. Nilimtandika bakora za mapaja, makalio pamoja na vigimbi, alipoongeza ubishi ndivyo dozi nayo ilipoongezeka. Ghafla jirani akapita na gari yake akiwa ametoka kazini alipoona vile alikuja kwangu fasta akawa ananizuia nisiendeleze kumtia dispilin.

Tumezozana sana na mawazo yake kwamba kizazi hiki hakihitaji fimbo. Yeye watoto wake huwa hawachapi huenda labda ni wakamilifu, ikabidi mada ihamie sebleni tumezungumza nusu saa hivi, ila nikawa natikisa kichwa tu maana ni mtu mzima, miaka 50 hivi.

Alipoondoka, baada ya dakika tano hivi nikaenda kummalizia dozi mwanangu maana haikukamilika kiufasaha. Nikatia za fasta fasta kama tano hivi nadhani jirani aliskia kile kilio, nilipoona simu ya namba yake inaita nikamchana tu kwamba binafsi nachofanya ndicho kilicho sahihi kwa mwanangu.

Kwa sasa chumbani kwake ni kusafi, kuna game yake (Play Station 4) huwa anachezaga kwenye TV siku za weekend kakuta tunacheza na mdogo wake basi na yeye kaunga, Full tabasamu kama vile hajachezea mboko. Mtoto atabaki mtoto tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazungu wameanza hii style ya kuto chapa watoto wao miaka ya hivi karibuni, Nakumbuka hata interview ya Arnord Schwazeneigar muigizaji maarufu alikiri kwamba walipokuwa wadogo zamani wakileta ujinga viboko havikuzuilika. Matokeo yake watoto wa kizungu wanatukana hadi wazazi wao sasa ukiachana na
Wazungu wameanza hii style ya kuto chapa watoto wao miaka ya hivi karibuni, Nakumbuka hata interview ya Arnord Schwazeneigar muigizaji maarufu alikiri kwamba walipokuwa wadogo zamani wakileta ujinga viboko havikuzuilika. Matokeo yake watoto wa kizungu wanatukana hadi wazazi wao sasa ukiachana na vituko vingine

Hata wazungu wenyewe sio kwamba wanaipenda sema tu sheria ndio zinawabana, ndo maana maadili yanazidi kupolomoka huko kwao
 
Back
Top Bottom