Tusipangiane mtindo wa malezi: Jirani yangu kajaribu kunithibiti nisimtandike mwanangu kisa watoto wake hawachapi

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
1,406
2,000
samaki mkunje angali mbichi

Kwa kawaida ninapoenda kazini, huwa namwachia mtoto wangu wa kiume mwenye miaka 10 majukumu kadhaa ayatekeleze japo kuna house girl na ndugu zake wakubwa ila na yeye lazima ajisaidie baadhi ya vitu kwa manufaa yake na atusaidie baadhi ya vitu kwa manufaa yetu wote.

Majukumu yake:
1. Kutandike kitanda chake
2. Afue nguo zake
3. Chumba chake kiwe kisafi
4. Akila sahani azioshe.
5. Kufanya homework za mwalimu wa tuition niliyemletea katika kipindi hiki cha corona.
6. Kuaga na kutujulisha anakoenda kucheza, mwiko kucheza maeneo nje ya mtaa wetu katika kipindi hiki kibaya.

Majukumu ya kuwa msaada kwenye nyumba
1. Afagie uwanja asubuhi kwa kupokezana na house girl yani yeye leo kesho mwenzake
2. Kutumwa kununua vitu duka la karibu. mfano mafuta, vocha, n.k
3.Kutoa magugu na kumwagilia maji mboga kila jioni.

Sasa naona dogo anataka kupima upepo kwa kijiko nadhani, kaanza kuwa mvivu wa kutandika kitanda, nguo hafui, anategea zamu ya kufagia, akila haoshi sahani anaiacha tu kwenye sinki aoshewe na house girl.

Juzi tulikaa na wife tukamwambia aache hii tabia kwa sababu ni mbaya na madhara yake ni mabaya akiendelea. Jana kaendelea nikampiga mkwara asirudie ila niliporudi chumba chake hajatandika kitanda na hakufagia asubuhi. Leo kafagia ila hajatandika kitanda na kuna vyombo chini ya kitanda.

Nyumbani kwangu nimepanda miti kwajili ya matunda, kupata kivuli jua likiwaka, ila pia hii miti ni dawa kwa mtoto anaeanza kuwa na tabia zisizonipendeza,

Nina mti wa mpera, nilikata kiboko cha wastani na kukikarabati vizuri nikakificha, aliporudi huko anapochezaga na wenzake majirani akaja akanisalimia, ile anavyonipita nikamdaka mkono, tukaenda nilipohifadhi dawa yake.

Kwa kuwa nilishakaa naye na kumuelewesha mara ya kwanza, kumgombeza mara ya pili, hii mara ya tatu ilibidi nimpe dawa. Nilimtandika bakora za mapaja, makalio pamoja na vigimbi, alipoongeza ubishi ndivyo dozi nayo ilipoongezeka. Ghafla jirani akapita na gari yake akiwa ametoka kazini alipoona vile alikuja kwangu fasta akawa ananizuia nisiendeleze kumtia dispilin.

Tumezozana sana na mawazo yake kwamba kizazi hiki hakihitaji fimbo. Yeye watoto wake huwa hawachapi huenda labda ni wakamilifu, ikabidi mada ihamie sebleni tumezungumza nusu saa hivi, ila nikawa natikisa kichwa tu maana ni mtu mzima, miaka 50 hivi.

Alipoondoka, baada ya dakika tano hivi nikaenda kummalizia dozi mwanangu maana haikukamilika kiufasaha. Nikatia za fasta fasta kama tano hivi nadhani jirani aliskia kile kilio, nilipoona simu ya namba yake inaita nikamchana tu kwamba binafsi nachofanya ndicho kilicho sahihi kwa mwanangu.

Kwa sasa chumbani kwake ni kusafi, kuna game yake (Play Station 4) huwa anachezaga kwenye TV siku za weekend, kakuta tunacheza na mdogo wake basi na yeye kaunga, Full tabasamu kama vile hajachezea mboko. Mtoto atabaki mtoto tu 🤣 🤣 🤣

 

1gb

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,840
2,000
Uko Sahihi.
Leo ukikutana na Sir God atakupa mkono wa Pongezi.

MITHALI 23:13-14
Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.

Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu.
 

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
1,406
2,000
Wapo watakao kupinga lakn huo ndio ukwel Kama mtoto hatii maagzo ya mzazi sharti aadhibiwe uzungu na usasa usituharibie watoto
Wazungu wameanza hii style ya kuto chapa watoto wao miaka ya hivi karibuni, Nakumbuka hata interview ya Arnord Schwazeneigar muigizaji maarufu alikiri kwamba walipokuwa wadogo zamani wakileta ujinga viboko havikuzuilika. Matokeo yake watoto wa kizungu wanatukana hadi wazazi wao sasa ukiachana na vituko vingine

Ila adhibu kwa nidhamu ya kimfundisha usimpige ukamuumiza
Viboko vya mpera vya makalioni, vigimbi na mapaja wengi tumechapwa sana udogoni, sijawahi kupata madhara makubwa zaidi ya maumivu ya baraka katika ukuaji wangu hadi nipo mtu mzima.
 

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
1,406
2,000
Mchape mtoto anapokosea ila usisababishe mtoto akuone wewe ni adui yake
Nachapa kosa lilelile anaporudia mara, Ujue malezi ya kiafrika ya ajabu sana, Mama yangu kanichapa sana ila ni kama besti yangu vile.

Mzee alinitandika mara chache sana na kunipa mahitaji lakini kwa mbali kama namuogopa japo simuoni ni adui. Hiki nakitegemea sana hata kwa mwanangu, Baba wa Kiafrika ni baba wa Kiafrika tu.
 

KAYAFA MKUU

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
222
250
Mkuu naunga mkono hoja, ila nitatoka nje kidogo ya mada. Jitahidi kutomruhusu mtoto kuzurura kipindi hiki cha Corona, shule zimefungwa ili wakae nyumbani kwa usalama wao.

Pia huyo mwalimu wa twisheni unayemruhusu aingie kwako anaweza akaleta Corona nyumbani kwako, sijajua huko ulipo hali ya maambukizi ya COVID-19 ilivyo, lakini tahadhari ni muhimu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom