Tusipangiane mtindo wa malezi: Jirani yangu kajaribu kunithibiti nisimtandike mwanangu kisa watoto wake hawachapi

Naunga mkono hoja aisee viboko ndo dawa mausia waachie wazungu me mwenyewe wakwangu nikija kupata vimbo ni moja ya lifestyle yake na yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Wazungu wenyewe wameanza hivi vitu miaka ya karibuni, Interview moja ya Arnold Schwarzenegger alikuwa anashangaa malezi ya kisasa, namnukuu "If we did something bad or we disobeyed our parents, the rod was not spared. "

Madhara yake ndio watoto tunasikia wanapiga na kutukana hadi wazazi wao kitu ambacho ni nadra sana huku kwetu
 
Tatizo unalo wewe mzazi.
Unajisifia kumchapa mwanao badala ya kumuelekeza pasipo na kuumizana.
Mfundishe kwa upendo mwanao ili apende kufanya hivyo sio afanye by force.

Ukiona huna uwezo wa kumfundisha mtoto bila kumchapa, hiyo kazi haikufai

Sent using Jamii Forums mobile app
Akili za mtoto sio kama za mtu mzima, ndio maana alimuonya mara nyingi lkn bado alirudia. Kumnyima mtoto fimbo pale anapokosa ni kutomtendea haki, huko mbele atakuja kukulaumu kwa kushindwa kumtia adabu.Kama watu wazima wenyewe wanaadhibiwa kwa jela na faini sembuse mtoto!

Vv



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akili za mtoto sio kama za mtu mzima, ndio maana alimuonya mara nyingi lkn bado alirudia. Kumnyima mtoto fimbo pale anapokosa ni kutomtendea haki, huko mbele atakuja kukulaumu kwa kushindwa kumtia adabu.Kama watu wazima wenyewe wanaadhibiwa kwa jela na faini sembuse mtoto!

Vv



Sent using Jamii Forums mobile app
Point nzito hii, wenzetu hata wezi wakikamatwa huwa wanapelekwa polisi, huku mwizi anachomwa,
 
Mimi namfundisha mwenyewe na siku ya kwanza namfundisha bila shida na Namwambia asinidanganye sasa kwa kuwa shule ni wanapiga viboko Mimi ni makonzi tu yaani konzi moja anatamani kuniuliza baba jina lako la utoto ni uliitwa nani...hawa vijana nilichogundua hawawaheshimu wala kuwaogopa mama zao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fimbo ni safi za kumnyoosha ila zisizidi usipige kama unaua mbwa I remember my dady alikuwa akinipa kichapo heavy alinivua nguo kipigo cha uchi duh kiskie yaani
 
Ulichofanya ni sahihi kabisa mkuu, ila kwa ushauri next time jaribu kumwambia mkeo(Mama wa mtoto) atoe hiyo adhabu ili kumuondolea picha mtoto kwamba Baba ni katili-
 
Kuna katoto kandugu yangu nilikuwa nakaambia usipande kwenye hayo matofali utaumia ,hakaelewi .Siku moja kakapanda kakaanguka naambiwa mpaka kalizimia.Baada ya kupona nilikapandisha kwenye hayo matofali nikakachapa fimbo tano tu .Sasa hivi hata uje na crane hukapandishi na hakapandi wala kusogea kwenye matofali.Jibu ni moja uncle hapendi.Naunga mkono mara moja moja kiboko kichukue nafasi.
 
samaki mkunje angali mbichi

Kwa kawaida ninapoenda kazini, huwa namwachia mtoto wangu wa kiume mwenye miaka 10 majukumu kadhaa ayatekeleze japo kuna house girl na ndugu zake wakubwa ila na yeye lazima ajisaidie baadhi ya vitu kwa manufaa yake na atusaidie baadhi ya vitu kwa manufaa yetu wote.

Majukumu yake:
1. Kutandike kitanda chake
2. Afue nguo zake
3. Chumba chake kiwe kisafi
4. Akila sahani azioshe.
5. Kufanya homework za mwalimu wa tuition niliyemletea katika kipindi hiki cha corona.
6. Kuaga na kutujulisha anakoenda kucheza, mwiko kucheza maeneo nje ya mtaa wetu katika kipindi hiki kibaya.

Majukumu ya kuwa msaada kwenye nyumba
1. Afagie uwanja asubuhi kwa kupokezana na house girl yani yeye leo kesho mwenzake
2. Kutumwa kununua vitu duka la karibu. mfano mafuta, vocha, n.k
3.Kutoa magugu na kumwagilia maji mboga kila jioni.

Sasa naona dogo anataka kupima upepo kwa kijiko nadhani, kaanza kuwa mvivu wa kutandika kitanda, nguo hafui, anategea zamu ya kufagia, akila haoshi sahani anaiacha tu kwenye sinki aoshewe na house girl.

Juzi tulikaa na wife tukamwambia aache hii tabia kwa sababu ni mbaya na madhara yake ni mabaya akiendelea. Jana kaendelea nikampiga mkwara asirudie ila niliporudi chumba chake hajatandika kitanda na hakufagia asubuhi. Leo kafagia ila hajatandika kitanda na kuna vyombo chini ya kitanda.

Nyumbani kwangu nimepanda miti kwajili ya matunda, kupata kivuli jua likiwaka, ila pia hii miti ni dawa kwa mtoto anaeanza kuwa na tabia zisizonipendeza,

Nina mti wa mpera, nilikata kiboko cha wastani na kukikarabati vizuri nikakificha, aliporudi huko anapochezaga na wenzake majirani akaja akanisalimia, ile anavyonipita nikamdaka mkono, tukaenda nilipohifadhi dawa yake.

Kwa kuwa nilishakaa naye na kumuelewesha mara ya kwanza, kumgombeza mara ya pili, hii mara ya tatu ilibidi nimpe dawa. Nilimtandika bakora za mapaja, makalio pamoja na vigimbi, alipoongeza ubishi ndivyo dozi nayo ilipoongezeka. Ghafla jirani akapita na gari yake akiwa ametoka kazini alipoona vile alikuja kwangu fasta akawa ananizuia nisiendeleze kumtia dispilin.

Tumezozana sana na mawazo yake kwamba kizazi hiki hakihitaji fimbo. Yeye watoto wake huwa hawachapi huenda labda ni wakamilifu, ikabidi mada ihamie sebleni tumezungumza nusu saa hivi, ila nikawa natikisa kichwa tu maana ni mtu mzima, miaka 50 hivi.

Alipoondoka, baada ya dakika tano hivi nikaenda kummalizia dozi mwanangu maana haikukamilika kiufasaha. Nikatia za fasta fasta kama tano hivi nadhani jirani aliskia kile kilio, nilipoona simu ya namba yake inaita nikamchana tu kwamba binafsi nachofanya ndicho kilicho sahihi kwa mwanangu.

Kwa sasa chumbani kwake ni kusafi, kuna game yake (Play Station 4) huwa anachezaga kwenye TV siku za weekend, kakuta tunacheza na mdogo wake basi na yeye kaunga, Full tabasamu kama vile hajachezea mboko. Mtoto atabaki mtoto tu

Ila jihadhari na mama yake. Akikugeuka atamharibu mtoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usimsikilize huyo jirani yako Kuna usemi unasema Mchelea mwana kulia hulia yeye
Maana yake usipomuadhibu sasa akiwa mkubwa hutakuwa na uwezo wa kumchapa na akiwa mkorofi anaweza kukugeuzia kibao akawa anakupa wewe kichapo mfano akiwa mvuta bangi
 
Back
Top Bottom