Tusimlaumu Rais Samia, tukumbuke tulikotoka

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
16,969
Reaction score
26,058
Tafakuri ya Askofu Benson Kalikawe Bagonza

Rais Samia ameweka rekodi. Tutasahau barabara, madaraja, madarasa na teuzi anazofanya. Lakini hili la kukutana na Chadema katika maadhimisho ya BAWACHA hatutalisahau kirahisi.

Wapo walionuna pande zote mbili za CCM na Upinzani. Ni budi wawepo ili watukumbushe tulikotoka. Hata kuku wa pande mbili hizo hawakuruhusiwa kujamiiana. Leo twakumbatiana!

Mwaka jana 2022 nilihutubia Bawacha Kitaifa kule Iringa. Nilisema tunahitaji Tanzania mpya siyo CCM mpya wala Chadema mpya.

Niliporudi DSM nilikutana na kiongozi wa CCM kitaifa nikamwambia; “Awamu ya Tano imeimarisha upinzani kwa namna ambayo ni vigumu kuubomoa bali kuuruhusu ujibomoe.”

Sasa Rais Samia ameanzisha mchakato wa upinzani kujibomoa wenyewe, si kuruhusu Rais mwingine kama yule aje kuubomoa. Tumuunge mkono Rais Samia anapotumia hoja kuunganisha nchi kuliko kutumia fedha na mabomu kugawa nchi.

Napenda kushauri mambo 10:
1. Kila upande una wahafidhina (Zealots).
Kazi ya kiongozi si kuwapuuza wala kuwafukuza. Ni kujadiliana nao bila kupigana nao. Wakiondoka vyama vitalala.

2. Kufukuzana ni hulka ya viongozi madikteta na walevi wa madaraka.
Rais Samia na Mbowe wajiepushe na hulka hiyo.

3. Kuna mpito unakuja kitaifa.
Mbuzi atalala na chui zizi moja bila kuumizana. Bungeni, serikalini, na hata kwenye kamati. Tujifunze kuishi na hali tusiyoweza kuibadilisha.

4. Ukweli wa yaliyopita ni muhimu kuliko haki kwa yajayo.
Tujifunze kusamehe kosa lililo wazi. Hata marehemu akiacha madeni huwa yanalipwa na warithi.

5. Tusisahau tulipopitishwa.
Si CCM wote waliokubaliana na hali ile. Si wapinzani wote walioichukia hali ile. Ili tusirudi huko tuungane kusema NEVER and NEVER again.

6. Ili tusirudi huko, mifumo imara na taasisi imara ni muhimu kuliko super woman au super mwamba.
Hata kama hatuipendi; KATIBA MPYA ni hitaji la jana kuliko leo na wanaihitaji watawala kuliko watawaliwa.

7. Kiwango cha rushwa bado kiko juu na kinastawisha kiburi cha watawala dhidi ya wananchi.
Wenye fedha wanaanza kujiona juu ya sheria. Rushwa hii ikiingia ndani ya vyama, tutampata mwenye roho isiyo ya Samia na mbaya kuliko Bwana yuleee.

8. Jukumu la Rais ni kuongeza uhuru wa wananchi; si kuupunguza.
Watanzania tuunge mkono jitihada za Rais kuthamini na kuvumilia maoni tofauti. Rais hawezi kufa wala kuugua kwa kuambiwa asiyopenda kusikia.

9. Siku ya wanawake imefana, bado safari ya ukombozi wao ni ndefu.
Maadui wao ni wengi. Hata mwanamme anayekandamizwa na mkewe lakini anajifanya mbabe mbele ya wanaume wenzake asaidiwe na wanawake!

10. Wapinzani wa maridhiano ni wale walioshindwa ndani na nje ya vyama vyao.
Maridhiano yanawanyima uhalali. Lakini wapo wanaotaka maridhiano yaondoe tofauti za mtazamo na maoni tofauti. Hatutaki makasuku wa taifa. Tuheshimu tofauti bila kupigana.

Tumuunge mkono Rais Samia. Tumpinge kwa hoja. Tusisahau kirahisi tulikotoka.
 
1. Tunatakiwa kufahamu kuwa nchi hii ni ya wote na sio ya CCM au CDM au chama kingine chochote.

2. maridhiano ni muhimu kwa ustawi wa Taifa ili tuondokane na ule utawala wa shetani!

3. Tutambue kuwa hata vitabu vitakatifu vinanena kuwa; haki uinua Taifa na dhuluma huangamiza taifa.
(mfano mzuri angalieni utawala wa awamu ya 5 ulivyokuwa umeangamiza shetani)
 
Sumu ya haya maridhiano ni KATIBA MPYA maana hapo Chadema ndipo wataanza kununa. Dr Bagonza (Askofu wa KKKT), unasahau kuwa Katiba Mpya haiwezi kuandaliwa na wanaotamani madaraka bali wasiotaka madaraka. Hiyo haitakuwa katiba bali uozo. Yangu macho nasubiri siku hiyo itimie kama ya JK (ati nyie Wabunge hamtaki kuwa mawaziri!!!).
 
Hatua ndio imeanza, Katiba inaundwa kikosi kazi na itakuja tu, usiwe na mawazo ya wahafidhina , kuwa na imani na Mama .
 
1. Tunatakiwa kufahamu kuwa nchi hii ni ya wote na sio ya CCM au CDM au chama kingine chochote.
2. maridhiano ni muhimu kwa ustawi wa Taifa ili tuondokane na ule utawala wa shetani!
3. Tutambue kuwa hata vitabu vitakatifu vinanena kuwa; haki uinua Taifa na dhuluma huangamiza taifa.
(mfano mzuri angalieni utawala wa awamu ya 5 ulivyokuwa umeangamiza shetani)
CHADEMA wamechukua hatua kwakuwa ACT ya ZITTO hawataki katiba wanataka tume huru.
CUF hawataki Katiba wala Tume,wao wanataka GNU-
Vyama vingine ni vya msimu na vingi ni mapandikizi vinasubiri uchaguzi waombee msaada huko magharibi.
 
Wananchi watakula huo mkutano na maridhiano? Uchumi unaporomoka, watu hali ni mbaya, maji umeme mgao bidhaa bei juu bado mnashabikia huu upuuzi?
 
Hatua ndio imeanza, Katiba inaundwa kikosi kazi na itakuja tu, usiwe na mawazo ya wahafidhina , kuwa na imani na Mama .
Wewe nawe sawa na hao. Nitatoa mfano mmoja tu. Chadema inataka katiba ambayo matokeo ya urais yatapingwa mahakamani. Je Samia atakubali hilo? Chadema inataka katiba ambamo madaraka ya Rais yatapunguzwa, Je, Samia atakubali hilo?
 
Umesikia SAMIA hataki matokeo kupingwa? Uchaguzi ukiwa chini ya tume huru na ukiwa fair kwanini uogope Kesi?
Unafikir kila mtu atafungua kesi kisa tu hajashinda? Kesi za uchaguzi kuna pre -filling, kabla ya kuwa admitted lazma uonyeshe kuna ukiukwaji, tatizo lishe mbovu ya wabongo na elimu duni ya CCM kwa miaka 60 ndio maana hata wewe unayetaip hapa mambo mdogo kama haya hujui.
 
Wananchi watakula huo mkutano na maridhiano? Uchumi unaporomoka, watu hali ni mbaya, maji umeme mgao bidhaa bei juu bado mnashabikia huu upuuzi?
NINI KIFANYIKE?
Nenda basi wewe kagawie watu chakula na maji, maana mmekaa miaka 60 watoto wanavuka kwa mitumbwi kwenda shule wakati Mwigulu akizunguka na elikopta kuzindua sensa.
 
Umesikia SAMIA hataki matokeo kupingwa? Uchaguzi ukiwa chini ya tume huru na ukiwa fair kwanini uogope Kesi?
Unafikir kila mtu atafungua kesi kisa tu hajashinda? Kesi za uchaguzi kuna pre -filling, kabla ya kuwa admitted lazma uonyeshe kuna ukiukwaji, tatizo lishe mbovu ya wabongo na elimu duni ya CCM kwa miaka 60 ndio maana hata wewe unayetaip hapa mambo mdogo kama haya hujui.
Akili yako mbovu, nani hajui kama kuna Tume Huru CCM haiwezi kufua dafu! Hii ni kawaida kwetu wanadamu, kitu ukiwa nacho unasema cha nini ingawa wasionacho wanasema tutakipata lini. Ndiyo maana nchi kama Zambia au Malawi kubadili uongozi ni rahisi
 
well said
 
well said
Mambo si rahisi kama tunavyofikiria! Njia ya kufanya ni kuwa na sheria ambayo wote watakaohusika na uandaaji pamoja na kupitisha hiyo katiba mpya, wasigombee uongozi katika nchi hii kwa miaka 20 ijayo. Hapo tutapata katiba nyie Chadema muipendayo la sivyo msahau.
 
Wassira , Makongoro yaani ni viongozi zaidi ya miaka 50 na hawataki kuachia, ukisema katiba ije na vigezo vikali hawawezi kubali.
 
Uzuri wa bwana yule upo katika hoja namba 7.

Na hayo ndio wananchi wa kawaida walikuwa wanataka yasiwepo ndio maana bwana yule ana nguvu sana hata sasa!

Bagonza mwenyewe ana kili kwenye hoja namba 7 kwamba mambo ya hovyo yameanza kushamiri, je ni lini yaliondoka? Bila shaka ni kipindi cha bwana yule.

[emoji23][emoji23][emoji23]Hawa watu huwa wanajitia madole na kujinusa wenyewe!
 
Tafakuri ya Askofu Benson Kalikawe Bagonza

Rais Samia ameweka rekodi. Tutasahau barabara, madaraja, madarasa na teuzi anazofanya. Lakini hili la kukutana na Chadema katika maadhimisho ya BAWACHA hatutalisahau kirahisi.

Wapo walionuna pande zote mbili za CCM na Upinzani. Ni budi wawepo ili watukumbushe tulikotoka. Hata kuku wa pande mbili hizo hawakuruhusiwa kujamiiana. Leo twakumbatiana!

Mwaka jana 2022 nilihutubia Bawacha Kitaifa kule Iringa. Nilisema tunahitaji Tanzania mpya siyo CCM mpya wala Chadema mpya.

Niliporudi DSM nilikutana na kiongozi wa CCM kitaifa nikamwambia; “Awamu ya Tano imeimarisha upinzani kwa namna ambayo ni vigumu kuubomoa bali kuuruhusu ujibomoe.”

Sasa Rais Samia ameanzisha mchakato wa upinzani kujibomoa wenyewe, si kuruhusu Rais mwingine kama yule aje kuubomoa. Tumuunge mkono Rais Samia anapotumia hoja kuunganisha nchi kuliko kutumia fedha na mabomu kugawa nchi.

Napenda kushauri mambo 10:
1. Kila upande una wahafidhina (Zealots).
Kazi ya kiongozi si kuwapuuza wala kuwafukuza. Ni kujadiliana nao bila kupigana nao. Wakiondoka vyama vitalala.

2. Kufukuzana ni hulka ya viongozi madikteta na walevi wa madaraka.
Rais Samia na Mbowe wajiepushe na hulka hiyo.

3. Kuna mpito unakuja kitaifa.
Mbuzi atalala na chui zizi moja bila kuumizana. Bungeni, serikalini, na hata kwenye kamati. Tujifunze kuishi na hali tusiyoweza kuibadilisha.

4. Ukweli wa yaliyopita ni muhimu kuliko haki kwa yajayo.
Tujifunze kusamehe kosa lililo wazi. Hata marehemu akiacha madeni huwa yanalipwa na warithi.

5. Tusisahau tulipopitishwa.
Si CCM wote waliokubaliana na hali ile. Si wapinzani wote walioichukia hali ile. Ili tusirudi huko tuungane kusema NEVER and NEVER again.

6. Ili tusirudi huko, mifumo imara na taasisi imara ni muhimu kuliko super woman au super mwamba.
Hata kama hatuipendi; KATIBA MPYA ni hitaji la jana kuliko leo na wanaihitaji watawala kuliko watawaliwa.

7. Kiwango cha rushwa bado kiko juu na kinastawisha kiburi cha watawala dhidi ya wananchi.
Wenye fedha wanaanza kujiona juu ya sheria. Rushwa hii ikiingia ndani ya vyama, tutampata mwenye roho isiyo ya Samia na mbaya kuliko Bwana yuleee.

8. Jukumu la Rais ni kuongeza uhuru wa wananchi; si kuupunguza.
Watanzania tuunge mkono jitihada za Rais kuthamini na kuvumilia maoni tofauti. Rais hawezi kufa wala kuugua kwa kuambiwa asiyopenda kusikia.

9. Siku ya wanawake imefana, bado safari ya ukombozi wao ni ndefu.
Maadui wao ni wengi. Hata mwanamme anayekandamizwa na mkewe lakini anajifanya mbabe mbele ya wanaume wenzake asaidiwe na wanawake!

10. Wapinzani wa maridhiano ni wale walioshindwa ndani na nje ya vyama vyao.
Maridhiano yanawanyima uhalali. Lakini wapo wanaotaka maridhiano yaondoe tofauti za mtazamo na maoni tofauti. Hatutaki makasuku wa taifa. Tuheshimu tofauti bila kupigana.

Tumuunge mkono Rais Samia. Tumpinge kwa hoja. Tusisahau kirahisi tulikotoka.
Hiyo ndo priority ya wanachi huku mchele kilo moja ukiwa umefika 4000
 
Hakuna jambo linaloanza bila chanzo. Kabla hujaisema serikali ya samia na wapinzani au magufuli na wapinzani ni vema ukaangalia JK na wapinzani.

Wanachokiona wapinzani kina maana leo ndicho ambacho kilifanywa na JK ila wao walitaka kuwa juu ya JK. Sote ni mashahidi ambapo arusha haikuisha maandamano.

Ilienda mbali hadi JK kupopolewa mawe kule Tegeta ila ni matunda ya upinzani. Maneno kama nchi haitatawalika ilikuwa kitu cha kawaida. Kila mtu aliibuka hadi kina sheikh Ponda wakaifanya Ijumaa siku ya maandamano.

Muendelezo ule chadema wakauhamishia kwa Magu. Magu alitekeleza malalamiko yote ya chadema ikiwemo;
1. Kuboresha huduma za afya.
2. Kufufua shirika la ndege
3. Kuondoa wafanyakazi wabadhirifu badala ya kuwahamishia maeneo mengine.
4. Safari zisizo na tija.
5. Kuboresha huduma ofisi za uma.
6 Kukomesha rushwa na ufisadi.
7. Kuondoa ukwepaji kodi.
8. Kushughulika na mafisadi.

Haya na mengine Magu alipoyafanya wakaanza kupita kumchafua na kudhania watamfanya kama JK, wakamuita dikteta uchwara. Jamaa aliwasihi sana wakae wajenge nchi. Hata nao walikiri Magu anapiga kazi wakiwa kwenye vijiwe vyao akiwemo msigwa na zitto.

Tofauti ni kuwa mama kawapa asali, lakini Magu hakutaka huo ujinga. Hapo ndipo walipopishana. Wakakaza nae akakaza. Magu yupo kwenye mpini wao wapo kwenye makali. Unategemea nini??

Magu aliwafundisha tu namna ya kuvumiliana na kuheshimiana. Na sasa umekuwa wimbo kwao. Maana wanajua madhara yake.
 
Back
Top Bottom