sifongo
JF-Expert Member
- Jun 5, 2011
- 4,896
- 5,302
Habari wanajamvi,wiki chache zilizopita nilikuwa Mkoani Arusha katika wilaya ya Loliondo na huko nilitembelea vijiji kadhaa na nilipata bahati ya kuongea na baadhi ya wazee wa kimasai kuhusu mgogoro wao na Kampuni ya Kiwindaji (OBC) kutoka Oman inayomilikiwa na familia ya kifalme, wengi wenu munajua kilichotokea mwaka 2009 pale serikali ilipowachomea wanakijiji makazi yao ili kuwapisha hao OBC wafanye kazi zao za uwindaji.
Wamasai wanalalamika kwamba inavyoonekana ni kama vile Serikali inataka kuwapotezea utamaduni wao kwani wamekuwa hawathaminiwi japo kwa kiasi fulani serikali inanufaika na wao kwani sio watalii wote wanakuja kuangalia wanyama bali na wamasai pia.
Niliwauliza au munatakiwa kuondoka hapa kwasababu munakaa katika hifadhi ya Taifa, walinijibu sio kweli walipo sio hifadhi Taifa bali ardhi ya kijiji na kwa uthibitisho walinionyesha vyeti vya umiliki wa Ardhi na inayowatambua wao kama wanakijiji halali na kwamba hao OBC ndio wanaowinda katika ardhi ya kijiji.
Nikawauliza tena au munafukuzwa kwasababu nyinyi munawinda wanyama kinyume cha sheria, wakaniambia hatujawahi kuwinda wanyama wa porini hata siku moja na wala hatuwatumii kama chakula isipokuwa tunawaona kama *marafiki zetu, na ukitaka kuamini subiri mpaka jioni wakati watoto wanarudisha mifugo unaweza kubahatika ukaona kundi la mbuzi linarudi na swala lakini tunawazuia kuingia zizini.(siku hiyo sikubahatika kuona ila huko njiani niliwaona pundamilia na swala wakiwa karibu kabisa na ngombe kama vile na wao wanachungwa).
Nilipotaka kujua hao OBC wanawinda kwa ruhusa ya nani ikiwa wao wanakijiji hawajaridhia, jibu nilopata ni kwamba wao walikataa lakini viongozi wa wilaya pamoja na aliyekuwa mbunge wao Marehemu kwela ndio walisaini kwa niaba ya kjijij.
Nimeleta hii mada hapa maana nimesikitika kuona vyombo vyetu vya habari na jamii yetu ni kama hatujihangaishi sana na huu mgogoro na badala yake mashirika ya Nje hasa shirika moja linaitwa avaaz ndio limekuwa linapiga kelele nyingi juu ya Wamasai kutoondolewa katika ardhi yao ili tu kupisha waarabu wawinde na kupoteza kabisa utamaduni wa Mmasai, Watanzania wenzangu nadhani ni muda wa kuamka na kuwatetea Watanzania wenzetu juu ya hiki wanachotendewa na sio mpaka tuonewe huruma watu wa nje(KUMBUKA SWALA LA RADA).
Mambo ni mengi juu ya Loliondo na umhuhimu wa kabila hili la Kimasai na nina hakika wapo wanaojua mengi zaidi watasaidia katika haya machache niliyoandika.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.