Tusimame kidete kuwatetea wamasai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusimame kidete kuwatetea wamasai

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sifongo, Sep 19, 2012.

 1. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,597
  Likes Received: 2,408
  Trophy Points: 280
  Habari wanajamvi,wiki chache zilizopita nilikuwa Mkoani Arusha katika wilaya ya Loliondo na huko nilitembelea vijiji kadhaa na nilipata bahati ya kuongea na baadhi ya wazee wa kimasai kuhusu mgogoro wao na Kampuni ya Kiwindaji (OBC) kutoka Oman inayomilikiwa na familia ya kifalme, wengi wenu munajua kilichotokea mwaka 2009 pale serikali ilipowachomea wanakijiji makazi yao ili kuwapisha hao OBC wafanye kazi zao za uwindaji.

  Wamasai wanalalamika kwamba inavyoonekana ni kama vile Serikali inataka kuwapotezea utamaduni wao kwani wamekuwa hawathaminiwi japo kwa kiasi fulani serikali inanufaika na wao kwani sio watalii wote wanakuja kuangalia wanyama bali na wamasai pia.

  Niliwauliza au munatakiwa kuondoka hapa kwasababu munakaa katika hifadhi ya Taifa, walinijibu sio kweli walipo sio hifadhi Taifa bali ardhi ya kijiji na kwa uthibitisho walinionyesha vyeti vya umiliki wa Ardhi na inayowatambua wao kama wanakijiji halali na kwamba hao OBC ndio wanaowinda katika ardhi ya kijiji.

  Nikawauliza tena au munafukuzwa kwasababu nyinyi munawinda wanyama kinyume cha sheria, wakaniambia hatujawahi kuwinda wanyama wa porini hata siku moja na wala hatuwatumii kama chakula isipokuwa tunawaona kama *marafiki zetu, na ukitaka kuamini subiri mpaka jioni wakati watoto wanarudisha mifugo unaweza kubahatika ukaona kundi la mbuzi linarudi na swala lakini tunawazuia kuingia zizini.(siku hiyo sikubahatika kuona ila huko njiani niliwaona pundamilia na swala wakiwa karibu kabisa na ngombe kama vile na wao wanachungwa).

  Nilipotaka kujua hao OBC wanawinda kwa ruhusa ya nani ikiwa wao wanakijiji hawajaridhia, jibu nilopata ni kwamba wao walikataa lakini viongozi wa wilaya pamoja na aliyekuwa mbunge wao Marehemu kwela ndio walisaini kwa niaba ya kjijij.

  Nimeleta hii mada hapa maana nimesikitika kuona vyombo vyetu vya habari na jamii yetu ni kama hatujihangaishi sana na huu mgogoro na badala yake mashirika ya Nje hasa shirika moja linaitwa avaaz ndio limekuwa linapiga kelele nyingi juu ya Wamasai kutoondolewa katika ardhi yao ili tu kupisha waarabu wawinde na kupoteza kabisa utamaduni wa Mmasai, Watanzania wenzangu nadhani ni muda wa kuamka na kuwatetea Watanzania wenzetu juu ya hiki wanachotendewa na sio mpaka tuonewe huruma watu wa nje(KUMBUKA SWALA LA RADA).

  Mambo ni mengi juu ya Loliondo na umhuhimu wa kabila hili la Kimasai na nina hakika wapo wanaojua mengi zaidi watasaidia katika haya machache niliyoandika.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 2. Konda wa bodaboda

  Konda wa bodaboda JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2016
  Joined: Jul 18, 2014
  Messages: 8,080
  Likes Received: 3,212
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa.
   
 3. m

  mjax Senior Member

  #3
  Sep 25, 2016
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 178
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Duuuuh nchi kuwa na rasilimali na huku viongozi ni walafi kama mafisi SHIDA KWELI-KWELI.....
   
 4. L

  LENDEYSON JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2016
  Joined: Sep 27, 2013
  Messages: 2,163
  Likes Received: 1,093
  Trophy Points: 280
  Suala la Loliondo ni Aibu kwa viongozi wa Kiafrika. They are ready to kill their own people for the interests of the Rich Foreigners ( no difference with colonial eras)!
   
 5. kisu cha ngariba

  kisu cha ngariba JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2016
  Joined: Jun 21, 2016
  Messages: 20,263
  Likes Received: 44,085
  Trophy Points: 280
  Viongozi wa Ccm wako radhi kuua ili wapate hela.
   
 6. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2016
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,597
  Likes Received: 2,408
  Trophy Points: 280
  Mambo ya Nchi hii mengine unaweza pata gonjwa LA moyo ukiyawaza.
   
 7. 1

  1954 JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2016
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 4,301
  Likes Received: 2,189
  Trophy Points: 280


  SWALA>>>>>>>>>>>>>>>>>SUALA


  Swala ni aina ya mnyama na maana nyingine ni ibada
   
 8. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2016
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,597
  Likes Received: 2,408
  Trophy Points: 280
  Shukrani chief........kwa usahihisho.
   
 9. Kilaga

  Kilaga JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2016
  Joined: Feb 23, 2013
  Messages: 1,803
  Likes Received: 860
  Trophy Points: 280
  Kwenye mada swala ni mnyama, wewe umeelewaje? Ulitaka amuite suala?
  Kiswahili hiki jamani...
   
 10. Beira Boy

  Beira Boy JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2016
  Joined: Aug 7, 2016
  Messages: 11,288
  Likes Received: 9,991
  Trophy Points: 280
  Lowasa yuko wapi si ni mumasai yahe
   
 11. 1

  1954 JF-Expert Member

  #11
  Sep 25, 2016
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 4,301
  Likes Received: 2,189
  Trophy Points: 280

  Jamani hii JF ina mambo kwa hakika....yaani ina mambo kweli kweli....

  Kwa hiyo hapa kwenye bold (KUMBUKA SWALA LA RADA) una maana mleta uzi alikuwa anamanisha mnyama???? Why can't you analyze issues you people??? Mleta uzi alielewa mapema hoja yangu na ameshajibu na kunishukuru kwa sahihisho langu lakini wewe bado uko 'ngangari' kwa suala ambalo limekwisha....Duh
   
Loading...