Uzalendo unaanzia ndani, ukianza kubagua watoto wako usitegemee uzalendo utakuwepo,
Wapinzani wanabaguliwa utazani sio Watanzania, mbunge kaenda kuchangia mifuko ya cement jimbo jirani anakamatwa wakati yule wa CCM anazunguka bara na visiwani hafanywi kitu halafu unataka uzalendo.
Juzi Sumaye kanyang'anywa shamba lake eti hajaliendeleza wakati kuna viongozi wa CCM wana hadi ekari elf moja ni mapori tupu, kila siku wabunge wa upinzani wanawekwa ndani hakuna anayekemea, leo unakuwa na gutz gani kumwambia Bulaya awe mzalendo?