Tusijidanganye: Watanzania hawatavumilia fisadi na ufisadi 2020

kinje ketile

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
616
1,000
Watanzania kuna vitu wanaweza kuvivumilia na kusahau ifikapo nyakati za uchaguzi mfano ni rahisi sana kuwasamehe waliodhira na kususa na kutangaza kuzirudia tena nyazifa zao ikiwa tu watu hao ni waadilifu.

Lakini watanzania wengi ngumu sana kuvumilia ufisadi. Watanzania hawa wanaweza siku za kampeni wakawa wanajaza sana mikutano ya kampeni shida siku ya kupiga kura ‘machale’ huwa yanawacheza na kujikuta kura wamempa MUADILIFU.

Sasa tunapoelekea kufunga mwaka ushauri kwa vyama vyote iwe ni tawala, NCCR-Mageuzi, ACT-wazalendo, NLD, JAHAZI, ADC na vingine msije mkajaribu kuwaleta kwetu mafisadi eti wapeperushe bendera zenu mtakuwa mnajimaliza.

N.B: Hili ni Onyo na ushauri !asietaka kusikia asubiri kuona akiangukia pua.
 
TEACHER FRANK MSIGWA

JF-Expert Member
Oct 19, 2016
537
500
Mafisadi wapo ndo mana fimbo ya umma inawashughulikia wakati wa uchaguzi!!kwani wewe mwenzetu mafisadi unawapenda?
Kama hukumu ya mafisadi ni fimbo ya umma wakati wa uchaguzi mahakama ya mafisadi iliwekwa kama pambo??...alafu mafisadi wapi unaoniuliza nawapenda...wale waliohonga hawara zao nyumba za serikali or wale waliotafuna na kutokomea na rambirambi juzi???
 
number41

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,009
2,000
2020 tutawasikia mafisadi watatajwa na ccm mana wamechukua sera kwa chadema imekua yao na ndo mana usikii wimbo huo kuimbwa tena na ccm utumika kwa kampeni
 
kinje ketile

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
616
1,000
Kama hukumu ya mafisadi ni fimbo ya umma wakati wa uchaguzi mahakama ya mafisadi iliwekwa kama pambo??...alafu mafisadi wapi unaoniuliza nawapenda...wale waliohonga hawara zao nyumba za serikali or wale waliotafuna na kutokomea na rambirambi juzi???
Hee sasa ndo umeandika nini?FISADI NI FISADI TU!awe alihonga nyumba (isivyo halali) au alihusika na mambo ya umeme kipindi kile ni FISADI tuUsijaribu kumpa kura yako kwenye uchaguzi
 
bne

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
1,574
2,000
Ni kweli mafisadi wasikubaliwe hata kidogo hasa mafisadi HAWA waliibuka sasa.
Mafisadi wa sasa ni hatari zaidi tuwakatae 2020.
Haiwezekani watanzania wanakufa kwa kipindupindu kwa kunywa maji machafu,
Watu wanakosa dawa hospitali,
Elimu iko mahututi,
Umaskini umeongezeka, halafu MTU mmoja kwa utashi anachukua mabilioni ya fedha anakwenda kujenga kiwanja cha ndege cha kimataifa kijijini kwake, anaweka trafficlight kijijini kwake, anaendesha nchi kwa ubaguzi,ukabila,uchama,na ukanda..
Hakika hatutawasamehe na hatutawasahau
2020.
 
kinje ketile

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
616
1,000
2020 tutawasikia mafisadi watatajwa na ccm mana wamechukua sera kwa chadema imekua yao na ndo mana usikii wimbo huo kuimbwa tena na ccm utumika kwa kampeni
Hao Chadema wamedisapoint watu wengi sana..!!UFISADI hawauzungumzii tena ,Hoja ya katiba hakuna kama tumerogwa vile tumebaki tumebung'aa macho kumwangalia M/kiti atasema nini..!matamko mepesi mepesi mara UKUTA,KATA FUNUA yasiyo na tija
 
number41

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,009
2,000
Hao Chadema wamedisapoint watu wengi sana..!!UFISADI hawauzungumzii tena ,Hoja ya katiba hakuna kama tumerogwa vile tumebaki tumebung'aa macho kumwangalia M/kiti atasema nini..!matamko mepesi mepesi mara UKUTA,KATA FUNUA yasiyo na tija
Siasa ya bongo ngumu akuna haki naona defence ya ccm ni hatar kwa uhai wao ndo mana kwa kushindwa kujitetea wanatumia mbinu za attacking kutumia power sasa jeshi la upinzani wale frontline wamepungua na njia ya kununua figure leaders na itazidi coz aim ni kuvunja ukawa na kutotaka sauti moja ya upinzani ndo kitu kikubwa kwa ccm nw sasa uwezi ona nn wanafanya chadema na hii pia mbaya kwa ccm coz ndo inafanya upinzani kupata wapinzani hatar kwa ccm na wanaweza fanya ACT kupata sababu ya kuunga nguvu kwenye umoja wa upinzani ambayo ni matokeo ya chuki tu nionavyo mi lkn ila hoja yako pia nzito kwa kujenga upinzani
 
kinje ketile

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
616
1,000
Ni kweli mafisadi wasikubaliwe hata kidogo hasa mafisadi HAWA waliibuka sasa.
Mafisadi wa sasa ni hatari zaidi tuwakatae 2020.
Haiwezekani watanzania wanakufa kwa kipindupindu kwa kunywa maji machafu,
Watu wanakosa dawa hospitali,
Elimu iko mahututi,
Umaskini umeongezeka, halafu MTU mmoja kwa utashi anachukua mabilioni ya fedha anakwenda kujenga kiwanja cha ndege cha kimataifa kijijini kwake, anaweka trafficlight kijijini kwake, anaendesha nchi kwa ubaguzi,ukabila,uchama,na ukanda..
Hakika hatutawasamehe na hatutawasahau
2020.
Define development! Kwa hiyo viwanja vikiwa Kilimanjaro na Dsm sawa sawa nongwa vikipelekwa nangwanda sijaona na kamsamba
 
bne

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
1,574
2,000
Define development! Kwa hiyo viwanja vikiwa Kilimanjaro na Dsm sawa sawa nongwa vikipelekwa nangwanda sijaona na kamsamba
Acha uwongo kitu chochote kinachofanywa kwa ajili ya nchi hufanywa kwa kuangalia faida yake.
Uwanja wa kimataifa uanapojengwa chato, chato kunashughuli ghani za kiuchumi ambazo ni endelevu ambazo hata ya yeye kuondoka kwenye uwongozi zitaendelea kuliingizia taifa faida?
Kwanini tunashindwa kuupanua uwanja wa mwanza kuwa wa kimataifa ambapo unalipa hadi tukimbilie chato?
Huo ni ubadhilifu wa mali za umma na matumizi mabaya ya madaraka na itakua ni haki kwa vizazi vijavyo kuja kuhoji kwa hili.
Kwani anatofauti gani na Mabutu Seseko aliyejenga uwanja wa kimataifa kijijini kwake ambapo sasa umekua pori? Alijenga kanisa kubwa kama lile la roma kijijini kwakwake ambapo sasa limegeuka mahame?
Hakika Mungu anamuona.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom