Tusiime P/School punguzeni ada

Kwali shule hiyo ni ghali. Kwani shule hiyo ipo wapi?

Unapoongelea ughali wa shule inategemea unaliganisha na nini. Tusiime siyo ghali ukilinganisha na shule za kimataifa au au kama ile ya FEZA. Lakini ukiilinganisha na shule za kajamba nani za akina Kayumba ni aghali sana. Ukitaka upate ulingao sahihi ilinganishe na shule zinazofanana nayo kama Esaacs, Academic, etc.
 
Ni kweli hiyo shule ni ghali sana hata mimi naifahamu, lakini kwenye ulimwengu wa soko huria kama huu, nadhani kuna watu wenye uwezo wa kununua huduma hiyo na ndio maana hata hiyo shule pamoja nagharama kubwa, bado inapata wanafunzi. Mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake.
 
Misuse of money..shule ya msingi kwanini mtoto asisome shule za serikali za kawida.
 
taabu ya shule za dar za serikal,darasa lina wanafunz 200,mwl.hajui hata wanafunz wake,ndio maana watu wanaamua kujifunga mkanda kwenda huko tusiime kuibiwa!
 
Acheni watu watumie pesa wewe hali ngumu unaona ajabu yeye mwenye pesa kutoa hiyo ada kitu cha kawaida....ushauri; kama huna kitu mpeleke mwanao shule zao hizo za ndala ndefu ili baadae akiletwa kwenye ulimwengu wa ushindani asande.
 
Serikali yetu ina vituko!
Nilishawahi kushauri iundwe Regulatory Authority kama ilivyo SUMATRA,EWURA,TACRA nk ili kusimamia elimu na kiwe chombo huru. Hakuna nchi hata moja hapa duniani ukiachia za kiafrika ambazo zinachia sekta nyeti kama elimu iendeshwe kama biashara ya wamachinga!!

Najua fika shule nyingi za serikali sio shule bali ni mabanda ya kufugia kuku lakini wao wanayaita shule. Kama akiwepo Regulator nyingi zitafungwa kwani hazifikii kiwango.

Sitaki kudumaza mawazo yenu lakini kumwambia mtu anyelalamikia ulanguzi wa karibu Milioni moja na ushee ili mtoto apate elimu ya msingi kwenye hiyo shule japo siifahamu lakini kwa hilo jina linafanana kama kuna asili ya Kiganda kama nakosea kunisahihisha ruksa.

Panahitajika kuwepo na Regulator vinginevyo elimu Tanzania inaelekea kuzimu tuache kuganga njaa the same applies kwenye sekta ya Afya!

Huu mzaha na CCM hautufikishi mbali kuna siku mtanikumbuka!!

..well said buddy, hii shule imezidi sana. Kila kukicha wao ni kuongeza ada tu. Mbaya zaidii ukitaka ufafanuzi kuhiusu ongezeko hilo hawa ndugu zangu kina Nshomile wana malingo ni balaaa! Dawa hapa ni kuwa na regulatory authority kama ilivyoelezwa na GT wengine.

Kwa wale wanaodhani kuwa kwa vile ni soko huria hivyo watu hawana haki ya kuhoji naomba mtofautishe elimu na biashara nyingine. Ikiwa kwa mfano unga wa mahindi kwenye duka la mangi umepanda bei ukilinganisha na duka la mpemba siku hiyo hiyo nita-switch na kuanza kununua kwa mpemba. Baada ya siku moja mpemba nae akipandisha nitaacha kununua kwake ntahamia duka la Lwikunulo. Kwenye suala la shule sio rahisi hivyo ni gharama na usumbufu sana kuhamisha watoto lakini pia unamfanya mtoto aanze kazi ya ku-adapt mazingira mapya kila mara na hii inaweza kumuathiri kimasomo.
 
Feza boys almost 4 million per year that's o level education, na nafasi watu wanagombania kupata
 
shule ni wahaya na waganda
Hapana shule ni ya Mhaya hana ubia na mganda mwenye shule anakwambia alianzia ahule ya chekechea sebuleni kwake mpaka hapo alipo!!na alikataza hiyo nyumba yake aliyokuwa anaishi na akaanzisha chekeche ibaki kama makumbusho!!..........Kimsingi zina bei kubwa sana mfano ni kama shule ya St Anne Marie wao wana mihula minne(4) bei ni 385,000/-+Transport sasa fikiria hapo!!na kwa nini kuwepo na mihula minne(4)?? Nadhani nitakuwa nimekujibu vema ndugu Magezi
 
Last edited by a moderator:
Mzazi anayepeleka mtoto shule binafsi namshangaa sana anapolalamika.... Hivi hakuna vikao vya wazazi hapo tusiime.. Malalamiko ya private yanapaswa yatatuliwe na private wenyewe sio kama zilivyo za umma
 
It's a private school for God's sake! Hutaki mtoe mwanao hapo shule zipo kibao
 
Mbona ada yao kwa mhura ni ndogo ukilinganisha na wengine wengi ndg, gharama kubwa kwa wazazi ipo kwenye usafiri. Ushauri mpeleke mwanao shule iliyo jirani nawe. Hizi shule taaluma yake uwa inakaribiana karibiana tu! Hivyo usijitwishe mzigo mkubwa wa mamilioni kwa mwaka. Wangu mimi hawapandi gari kwani shule walizopo ni mwendo wa mguu toka home. Good enough shule hizi zimetapakaa kila mtaa siku hizi na zenye ubora wa hali ya juu. Epuka kitu kinaitwa school bus! Uwa nina shangaa mtu anaishi Segerea anampeleka mwanawe Mbezi beach kwa school bus!
 
Shule ina mihula mitatu. Kila mhula shilingi 325,000 sio bweni, usafiri 70,000 kwa mhula computer studies 30,000. Huyo ni mwanafunzi wa msingi. Gharama hizi ziko juu sana. Hiyo bodi ya shule sijui kama wanaelewa mateso wanayopata wazazi. Tunaomba zipitiwe upya ikibidi na mamlaka zinazohusika. Wazazi wanaumia sana hawana pa kusemea tu. Kama elimu ni biashara, basi hawa jamaa wafungwe gavana. Itakuwaje mwanafunzi wa msingi alipe sawa na mwanafunzi wa sheria chuo kikuu? Huku ni kukomoana. Nawasilisha

du wako chini sana nenda Moga schools Bunju uulize... darasa la saba nimelipa takriban mil. 3 huko nyuma tulilipa almost 19000000... ndugu elimu aghali sana
 
Back
Top Bottom