Tusiime P/School punguzeni ada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusiime P/School punguzeni ada

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by AG, Aug 30, 2009.

 1. A

  AG Member

  #1
  Aug 30, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 70
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 25
  Shule ina mihula mitatu. Kila mhula shilingi 325,000 sio bweni, usafiri 70,000 kwa mhula computer studies 30,000. Huyo ni mwanafunzi wa msingi. Gharama hizi ziko juu sana. Hiyo bodi ya shule sijui kama wanaelewa mateso wanayopata wazazi. Tunaomba zipitiwe upya ikibidi na mamlaka zinazohusika. Wazazi wanaumia sana hawana pa kusemea tu. Kama elimu ni biashara, basi hawa jamaa wafungwe gavana. Itakuwaje mwanafunzi wa msingi alipe sawa na mwanafunzi wa sheria chuo kikuu? Huku ni kukomoana. Nawasilisha
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,000
  Trophy Points: 280
  maisha bora kwa kila Mtanzania
   
 3. K

  Kenge (Eng) JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2009
  Joined: Dec 7, 2006
  Messages: 502
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kwani ni lazima mtoto wako asome Tusiime Primary School?
  Acha wivu wa kike. Mbona usemi Academy nyingine? Kila sehemu na kila kona kuna vibao wanatangaza nafasi za masomo katika shule zao, peleka mwanao huko. Ukiona shule ni bora kuna nguvu imewekwa pale. How possible mtu awekeze halafu utoke pembeni udandie kirahisi. Hapo sipo nawe kabisaaa. Kataa kupeleka watoto wenu hakiukosa wanafunzi automatically atapunguza bei. Hupo? Jipime ubavu wako, usipende bora kuliko uwezo wako, naona hiyo shule ipo masafa ya uwezo wako. Ushauri wa bure amisha mtoto wako tafuta shule inayolingana na kipato chako.
   
 4. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Serikali yetu ina vituko!
  Nilishawahi kushauri iundwe Regulatory Authority kama ilivyo SUMATRA,EWURA,TACRA nk ili kusimamia elimu na kiwe chombo huru. Hakuna nchi hata moja hapa duniani ukiachia za kiafrika ambazo zinachia sekta nyeti kama elimu iendeshwe kama biashara ya wamachinga!!

  Najua fika shule nyingi za serikali sio shule bali ni mabanda ya kufugia kuku lakini wao wanayaita shule. Kama akiwepo Regulator nyingi zitafungwa kwani hazifikii kiwango.

  Sitaki kudumaza mawazo yenu lakini kumwambia mtu anyelalamikia ulanguzi wa karibu Milioni moja na ushee ili mtoto apate elimu ya msingi kwenye hiyo shule japo siifahamu lakini kwa hilo jina linafanana kama kuna asili ya Kiganda kama nakosea kunisahihisha ruksa.

  Panahitajika kuwepo na Regulator vinginevyo elimu Tanzania inaelekea kuzimu tuache kuganga njaa the same applies kwenye sekta ya Afya!

  Huu mzaha na CCM hautufikishi mbali kuna siku mtanikumbuka!!
   
 5. K

  Kibongoto JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wanaotakiwa kucontrol mambo hayo ndio wenye mishule ya namna hiyo. Hakuna kitu hapo. Wizi mtupu!
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  TUSIIME!!!?????

  mwenye shule mhaya?
   
 7. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hatuhitaji hizo regulatory authority, kwani sisi walaji ndio tunaoishia kuzilipia. Kinachohitajika ni kuwepo kwa bidhaa kede kede katika maghala tofauti, halafu nguvu ya soko itahamua.

  Kwa kifupi, wahamisheni watoto wenu katika hiyo, shule na mara moja bodi ya shule itapitia bei zao.
   
 8. A

  AG Member

  #8
  Aug 30, 2009
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 70
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 25
  Kenge kweli kenge, hiyo ni sample tu ulanguzi kwenye elimu umefikia kiwango cha kustaajabisha. Ungejua sokomoko la kuhamisha mtoto shule, usingejibu kama kenge!
   
 9. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Nono!

  It was said "never argue with a fool people might not notice the difference"
  Wewe kijana nimekusamehe kwa sababu kwanza hujawahi kuwa na mtoto ukaanza kumhamisha shule kila kukicha ada inapopandishwa kiholelea! after all hujui hata kinachoongelewa. Namshukuru aliyenijibu kwamba ni ya Mhaya kwa hiyo sio mbali na hisia zangu Kagera inapakana na Uganda!

  Kuhusu regulatiory authorities hapa tunazilipia kwa sababu CCM ni wachovu wa kubuni hazipaswi kuwa na utitiri wa wafanyakazi wa kudumu. Lakini hawa washenzi wamezigeuza ni ajira mbadala tena kwa watu ambao ukichunguza walikuwa kwenye mfumo rasmi wakakimbilia mishahara minono huko.Ajira yenyewe ni rushwa na mizengwe isiyokuwa na kifani na wala haziwekwi on perfomance basis.

  Kwa bahati mbaya wamehamia huko na hangover waliyotoka nayo huko serikali kwa hiyo sio wabunifu bali wababe. Kazi ya Regulator sio enforcement bali ni mizania tu. Wengine wamekuwa mbadala wa Tume ya Bei again ni hangover ya CCM. Zinahitajika na sio kuhusu bei tu hata na kuweka viwango!!! Hebu fikiria huduma ya Afya!!!!
   
 10. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hivi TEA (Tanzania Education Authority) ina majukumu gani?
   
 11. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kama sikosei kuna limit ya ada kwa hizi academies. Hawa wamevuka hiyo limit? Fuatilia wizara ya elimu uweze kufahamu ili hatua zichukuliwe
   
 12. M

  Magezi JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Uliza kwanza shareholders wa hiyo shule unaweza kuta ndo hao hao mawaziri/mafisadi. Lakini pia serikali iko likizo.
   
 13. M

  Magezi JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145

  Mwl. Nyerere angeruhusu haya hata wewe usingsema hayo matapishi.
   
 14. M

  Magezi JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145

  shule ni wahaya na waganda
   
 15. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Haya ndio mambo ya International school, hizi skul ukifuatilia sana zote ada zao zipo juu tu. Kama mtu unaona mfuko wako hautoshi vizuri ni vizuri kumpeleka mtoto kwenye skul za kawaida tu kama olympio, bunge na nyinginezo.
   
 16. M

  Magezi JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni kwamba hatuna regulatory authority yoyte ktk masuala ya elimu, kuna agencies kama TEA n.k. lakini sijua hata kazi yao ni nini. Kingine kikubwa ni kwamba wenye shule hizi ndo hao hao mawaziri (joseph mungai - enzi zake), wabunge, mafisadi wengine n.k. kwa hiyo wanapata super profit kwa kuwa kamua watanzania.

  Mimi nina imani kabisa kwa nchi changa kama TZ si busara na haki mtoto wa primary umlipie ada tshs. milioni moja kwa mwaka sawa na ada ya mwaka university!!!!
   
 17. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #17
  Aug 30, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu AG,

  Kuna kitu kinaitwa homeschooling, je umekwisha kisikia? Kwa vile elimu itolewayo na shule za serikali ni bomu, na vile vile elimu itolewayo na academies ni too expensive, fundisha watoto wako kutokea nyumbani kwako. Unaweza kuwafunmdisha wewe mwenyewe kama una uwezo huo, au unaweza kuajiri matutor wa kukufundishia. In fact ukaiajiri matutor ambao ni walimu kwenye shule za serikali, watafundisha vizuri sana kuliko huko kwenye academies tena kwa gharama nafuu sana.
   
 18. M

  Magezi JF-Expert Member

  #18
  Aug 30, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli nafikiria kuajiri walimu wanifundishie watoto wangu hapo hapo nyumbani badala ya kuwapeleka sijui tuition za mitaani
   
 19. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #19
  Aug 30, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwali shule hiyo ni ghali. Kwani shule hiyo ipo wapi?
   
 20. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #20
  Aug 30, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Ipo mitaa ya Tabata.
   
Loading...