Tusifurahie uwekezaji wa Rostam Azizi tukasahau tulivyopigwa kupiti Kagoda, Epa na Richmond

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
1,925
2,000
Naona sasa viongozi wa chama dume CCM mmesahau kilichotokea mwaka 2011 ambapo CCM ilijinasibu kujivua gamba.

Ccm ilijinasibu kujivua gamba kwa kuwa ilikuwa imechafuka kwa ufisadi na mafisadi wengi waliokuwa wanaliibia taifa letu walikuwa ni viongozi wa Ccm.

Mmoja wa watu waliosadikiwa kuwa mafisadi nguli nyakati hizo ni Rostam Aziz ambae alihusishwa na kila namna ya ufisadi uliofanyika nyakati hizo. Ufisadi kupitia Epa, Kagoda Agricultural Ltd hadi Richmond huyu mtu alihusishwa.

Je, kama ni kweli huyu mwekezaji aliibia taifa letu kisha kusepa ughaibuni baada ya kujiuzulu ubunge na kurudi kwa mkwara ya kuwa muwekezaji ndio iwe sababu ya kusahau yaliyopita?

Tusisahau kuvua operation ya kuvua gamba ilimfanya akajiuzuru ubunge. Au ndio kusema sasa amekuwa mtu safi?
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,968
2,000
CCM lini iliwahi kuwa safi toka kuanzishwa kwake? Nchi hii hakuna mtu aliefanya ufisadi isipokua alikua kiongozi serikalini au CCM.

Waliofanya ufisadi wa Escrow mbona wawili tu ndio wapo mahabusu na kupelekwa mahakamani mpaka leo, Rugemarila na yule Singa Singa, wakati waliopokea hela hizo list ilitoka zaidi ya watu 40 na account zao za benki na hela ilioingia???

Sioni shida kwa huyu Rostam, atleast anafungua makampuni mengi na kuajiri wa Tanzania wa hali ya chini, kuna wengine wamefisadi na kukimbiza hela zao nje ya nchi. Na wengine wame invest kwenye makampuni yao yalio na waajiriwa wachache (Unakuta kampuni ina thamani ya Billion 50, waajiriwa wapo 10).
 

Patema

JF-Expert Member
May 5, 2019
330
1,000
Mimi sioni kama kuna shida sababu mamlaka zilikuwepo na ndio maana hakuwahi kupatikana na kosa
 

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
28,296
2,000
Kumekucha
Hapo Sasa Ndiyo Mtaelewa Maana Ya
Mupe Muruke, Mupe Muruke
Huyu Mupe Bia, Yule Mupe Wine, Yule Muruke, Huyo Mupe Maji.
Janjajanja Primary School
Imefaulisha Wanafunzi Wote Kwenye Secondary
Lakini Hawajui Kusoma Na Kuandika


Caspian Construction Ltd.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom