Binafsi nimeridhika, mtia nia Nyerere ni jibu letu kwenye rushwa na ufisadi, like father like son!

DSN

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,837
1,674
BABA MTU ANASEMA TUKIKUANGALIA SURA TUSEME HUYU NAYE KWELI ANAPINGA RUSHWA NA UFISADI KWELI
nyerere1960somepeopleaimat.jpg
Je Wewe Ni Mla Rushwa Wewe Kweli?
Je Wewe ni Fisadi Wa Nchi Kweli?

11350577_841638995911379_5148806402324488995_n.jpg
KAULI YA JANA TAREHE 1/06/2015-BUTIAMA

Tanzania ni tajiri sana, ina pesa nyingi, wanafunzi hawapaswi kukosa mikopo hasa watoto wa maskini. Madaktari hawapaswi kumwangalia mgonjwa wakamwacha na kuondoka kwa kumriwaza kwa maneno.

Polisi hawatakiwi kuwa na filimbi na bangi mfukoni ili kukamata watu waje kugombolewa, mahakama za chini, mahakimu wakihongwa kuku wanaweza kuhukumu hata wake zao kwa njaa walizokuwa nazo. Wakurugenzi wanapigiwa simu watoe hela usipotoa unahamishwa kwa sababu tu ya makundi ya uraisi.

Pesa hazifiki kwa hawa wafanyakazi, sasa wamezigeuza majina sasa zinaitwa EPA, ESCROW, RICHMOND, na DOWANS. Vibaka wanagawana, tunataka chama chetu cha wakulima na wafanyakazi. Charles Makongoro Nyerere 2015


HIVI SASA WATANZANIA TUNAELEKEA KUPATA MAJAWABU YA MATATIZO YETU KWA MUDA MWAFAKA:



MAKONGORO NYERERE NA UJASIRI HUU WA NADRA CCM!


KINACHOJADILIWA kwa sasa, sehemu mbalimbali nchini, si tena kinachoitwa ‘tiba ya ajabu ya Babu wa Loliondo'; bali ni kilichotokea, hivi karibuni, huko Dodoma kinachoitwa ‘kujivua gamba kwa CCM'.

Mitaani, sokoni, kwenye mabaa, vijiweni na hata maofisini kinachozungumzwa sasa na kinachojadiliwa, ni kuhusu yaliyojiri huko Dodoma ambako CCM ‘kilijivua gamba' kwa kuwatosa viongozi wake maarufu wanaotuhumiwa kwa ufisadi.

Kote huko maswali kibao yanaibuliwa; Je, ni kweli CCM imefanikiwa kujivua gamba? Je, ni kweli Rais Kikwete kawatosa moja kwa moja maswahiba wake – Rostam Aziz, Edward Lowassa na Andrew Chenge au ni ‘usanii' wake mwingine? Je, uamuzi wa Dodoma wa kuwataka watuhumiwa hao wajiuzulu nafasi zao za uongozi katika Chama utafuatiwa na hatua za kisheria za vyombo vya kisheria dhidi yao?

Je, CCM sasa kinaweza kujigamba kwamba ni shwari; ilhali aliyeyalea magamba hayo (Kikwete) bado anaendelea kushikilia hatamu za uongozi?
Je, kina Lowassa, Rostam na Chenge wakishajiuzulu nyadhifa zao CCM, kama walivyotakiwa na NEC, watabaki ndani ya chama hicho kama wanachama wa kawaida au wataanzisha chao au watajiunga na vyama vilivyopo vya upinzani?

Haya ni baadhi tu ya maswali mengi yanayoulizwa hivi sasa na wananchi
kote nchini wanapojadili matokeo ya kikao hicho cha Dodoma. Ni dhahiri ni maswali yasiyo na majibu ya moja kwa moja ya uhakika, na ni dhahiri ni maswali ambayo ni muda tu ndio utatoa majibu yake. Waingereza wanasema; time will tell.

Vyovyote vile; naandika kumpongeza Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere, kwa mchangao wake ndani ya vikao hivyo vya CCM ambao ulikuwa ni wa kijasiri, kiungwana, kifalsafa na usio wa kinafiki. Ni mchango ulioweka mbele maslahi ya Taifa kuliko ya kwake binafsi.
Habari za uhakika nilizozipata kutoka kwa waliohudhuria mkutano huo, zinasema kwamba ni yeye pekee aliyekuwa na ujasiri wa kuuanika mbele ya wajumbe udhaifu wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete katika kuwashughulikia mafisadi ndani ya Chama na ndani ya Serikali.

Ni udhaifu huo wa Kikwete wa kuchelewa kuchukua hatua dhidi yao ambao umekifanya chama hicho kipoteze kwa kasi umaarufu wake kwa CHADEMA. Kwa maneno mengine, kama angelichukua hatua mapema wakati wa awamu yake ya kwanza ya uongozi, pengine mambo ndani ya CCM yasingekuwa shaghalabagala kama yalivyo sasa.
Sitakwenda ndani zaidi kulijadili suala hilo; kwa sababu wachambuzi wengine wamelijadili kwa umahiri mkubwa ndani ya gazeti hili. Isitoshe, kama nilivyoeleza mwanzoni, hoja yangu ya leo ni kupongeza tu ujasiri wa Makongoro Nyerere. Laiti kungekuwa na viongozi wengi jasiri kama yeye ndani ya CCM na ndani ya Serikali…..!

Mtoa habari wetu anasema kwamba wakati wa mkutano huo wa Dodoma, Makongoro alisimama ukumbini na akamtazama, kwa macho makavu, Mwenyekiti Jakaya Kikwete, na kisha maneno yafuatayo yakamtoka kinywani mwake:

"Lowassa ni ndugu yangu. Sina matatizo naye. Najua ananipenda, nami nampenda. Lakini kule ‘site' wanasema hapana. Atoke.
Tena nawe Mwenyekiti ulipokwenda Monduli, ukainua mkono wake juu, ukasema hujapata kuona kama yeye (Lowassa), kule ‘site' wakauliza; sasa hii ndiyo nini?"
Rostam simfahamu vizuri. Ninakotembelea yeye hawezi kuja, na mimi anakotembelea siwezi kwenda. Sina ugomvi naye. Lakini kule ‘site' wanasema naye hapana. Ulipokwenda Igunga ukamuamsha mkono ukasema yeye ni kama timu ya mpira iliyokamilika. Watu kwenye ‘site' wakauliza, sasa hii ndiyo nini?"

"Nasikia Chenge wanamwita Mzee wa Vijisenti. Ni ndugu yangu. Sina hakika kama anavyo vijisenti kiasi hicho. Lakini kwenye ‘site', si mimi, watu wanasema naye hapana.

Ulikwenda pia Rombo, ukamuamsha mkono Mramba, kule kwenye ‘site' watu wakatuuliza; sasa hii ndiyo nini?"


Ndugu zangu, hiyo ni sehemu tu ya mchango
mkubwa wa Makongoro Nyerere alioutoa ndani ya vikao hivyo vya CCM vya kujivua gamba, mjini Dodoma. Nina hakika, mpenzi msomaji, utakubaliana nami kwamba Makongoro alionyesha ujasiri mkubwa kwa kumkosoa kiungwana Rais Kikwete ndani ya kikao hicho. Ni ujasiri ambao ni nadra kuuona siku hizi ndani ya vikao vya juu vya CCM au vya Serikali; kwa maana ya Baraza la Mawaziri. Ni ujasiri mkubwa hasa ukizingatia kwamba wakubwa wetu wengi, hivi sasa, hufurahia kusifiwa tu, na huona raha kuzungukwa na court jesters (waimba sifa na walamba miguu ya wakubwa) ambao hucheka rais anapocheka, hununa rais anaponuna na ambao huwafanya maadui binafsi wa rais kuwa maadui zao pia!

Hawa court jesters hawawezi, kamwe, kumtonya Rais; hata pale inapoonekana dhahiri kwamba anakosea. Ilimradi mambo yao yanakwenda vizuri, watakaa kimya kwa sababu hawataki kumuudhi mkubwa wasijeenguliwa madarakani.
Ndiyo maana anapotokea mtu wa sampuli ya Makongoro Nyerere na kumtazama Rais na Mwenyekiti wa Chama kwa macho makavu, na kisha, kiungwana kabisa na kwa upole kabisa, akamwambia kwamba; "nawe ulikosea", lazima tuupongeze ujasiri wa mtu huyo. Ninasema hivyo; kwa sababu Rais Kikwete si Mungu au malaika asiyekosea. Rais au Mwenyekiti wa Chama naye pia ni binadamu kama sisi, na hufanya makosa kama sisi, na hivyo ni wajibu wetu kumfahamisha, kiungwana kabisa, pale anapokosea. Ni wajibu wetu kutamka "Mfalme yu uchi" inapotokea kweli "yu uchi".

Ni kwa mantiki hiyo Makongoro Nyerere alisimama na kumwambia ‘Mfalme': "Ulipokwenda Monduli ukainua mkono wake juu (Lowassa) ukasema hujapata kuona kiongozi kama yeye , kule ‘site' wakauliza sasa hii ndiyo nini?"…. ulipokwenda Igunga ukamuamsha (Rostam) mkono ukasema amekamilika kama timu ya mpira; watu kwenye ‘site' wakauliza sasa hii ndio nini?"


Kwa hakika, maneno hayo ya Makongoro yanachoma na kupenya nyoyo. Sina hakika Mwenyekiti Kikwete alijisikiaje wakati Makongoro akiyatamka maneno hayo; lakini nadhani alijutia kitendo kile alichokifanya Rombo, Monduli na Igunga; maana kilimuonyesha mbele ya Watanzania wote, ikiwa ni pamoja na kwenye mkutano huo, udhaifu wake kama kiongozi.
Kwa mara nyingine tena nimpongeze Makongoro Nyerere kwa kumkosoa Kikwete kipole, kiungwana na kifalsafa. Kwa Watanzania wengine wote ambao hatukuwemo kwenye ukumbi ule, Makongoro alitusemea, alitufikishia hisia zetu kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wetu.

Makongoro alitumia neno ‘site' (eneo ambako ndiko anakoshinda kusimamia shughuli zake za miradi ya ujenzi) kuwasilisha ujumbe wake, lakini ukweli ni kwamba ‘site' aliyoizungumzia inamaanisha kote nchini. ‘Site' ni sisi sote tulioshangazwa na hatua hiyo ya Kikwete ya kuwakampenia Lowassa, Mramba na Rostam; ilhali wanaandamwa na kashfa nzito za ufisadi.
Wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka kwamba wakati wa kampeni za mwaka jana za Uchaguzi Mkuu nilipata kuandika, kwenye safu hii, kuhusu kitendo hicho cha Rais Kikwete cha kuwakampenia ubunge watuhumiwa hao wa ufisadi.

Niliandika wakati huo kwamba haingii akilini mwangu (kwa mfano) kwa Kikwete kuusifia utendaji kazi wa Mramba kwenye mkutano wa kampeni Rombo; ilhali Serikali yake anayoiongoza tayari ilishamfikisha mtu huyo mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi, na kesi ilikuwa inanguruma!
Niliandika vilevile kushangazwa kwangu na Rais Kikwete kuwaomba wananchi wa Monduli na Igunga wawape kura za kishindo Lowassa na Rostam; ilhali watu hao wanahusishwa na kashfa ya ufisadi wa Richmond na Dowans, na hata mmojawao (Lowassa) kulazimika kujiuzulu uwaziri mkuu kwa tuhuma hizo.

Leo, nafarijika kwamba amejitokeza kijasiri Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa (Makongoro), na bila unafiki akamweleza Rais Kikwete (kwa kiungwana kabisa) udhaifu wake aliouonyesha kiuongozi katika suala hilo la mafisadi.
Ni hoja yangu kwamba kama Kikwete angekuwa na washauri makini, bila shaka, wangemweleza mara moja makosa aliyofanya ya kumsifu Mramba hadharani na kumuombea kura kwenye mkutano wa kampeni Rombo na athari zake za baadaye kwa Chama. Nina hakika, pamoja na u-hambiliki wake, angelifikiria mara mbili mbili kabla hajalirejea tena kosa hilo huko Monduli na baadaye Igunga.

Nina hakika vilevile kwamba ni kosa hilo la kuwapigia debe watuhumiwa wa ufisadi wakati wa kampeni, lililochangia kwenye kura chache alizopata kwenye uchaguzi huo ukilinganisha na za mwaka 2005.
Aidha, ni kwa sababu ya kosa hilo hilo watu sasa wanahoji juu ya uwezo wake wa uongozi, na wengi wanajiuliza; kama na yeye si gamba ambalo katika hali ya kawaida lilipaswa nalo kuvuliwa! Na wananchi wana haki ya kuwa na hisia hizo; maana itakuaje Rais na Mwenyekiti wa CCM (Kikwete) awamwagie sifa kemkem watuhumiwa hao wa ufisadi kwamba ni waadilifu na wachapakazi hodari, na kisha miezi sita baadaye Rais huyo huyo tena aongoze kikao cha chama cha kuwavua uongozi wa CCM watu hao hao kwa tuhuma za ufisadi?!

Kwa nini linapokuja suala la ufisadi tusitilie shaka uwezo wake wa kupima mambo (sense of judgement)? Kiongozi wa nchi anawezaje kuwa na sura mbili katika jambo hilo hilo moja; tena ndani ya kipindi kifupi tu?
Je, tuamini kwamba msimamo wake huu wa sasa (yeye na NEC nzima ya CCM) dhidi ya watuhumiwa hao wa ufisadi, ni wa kudumu na kwamba hataubadili tena huko mbele ya safari? Je, sasa tuamini kwamba kweli CCM imejivua gamba, na haitawakumbatia tena watuhumiwa wa ufisadi katika ngazi zote? Kama nilivyoeleza mwanzo, haya ni maswali ambayo yatajibiwa na muda tu!

Vyovyote vile; nafarijika kwamba ametokea jasiri (Makongoro) kumweleza hadharani Rais Kikwete udhaifu wake na makosa aliyoyafanya ya kuwakumbatia maswahiba wake hao wanaotuhumiwa kwa ufisadi; hata kama ni miezi sita imeshapita tangu ayatende, na hata kama tayari yameshaiathiri CCM.
Kwa hakika, mafanikio ya CCM baada ya kujivua gamba, yatategemea mwelekeo wa Mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete. Sichelei kusema kwamba kama naye hatabadilika (akajivua gamba lake binafsi), CCM itakuwa ile ile ya jana na leo hadi tunaingia uchaguzi mkuu mwingine wa mwaka 2015.
Nihitimishe safu yangu kwa kusema kwamba hata kama kauli zake hizo za Dodoma zitakuja kumponza Makongoro huko mbele ya safari, angalau historia itamtetea kwamba alikuwa na ujasiri wa kutamka: "Mfalme yu uchi" wakati wengine ndani ya ukumbi huo walikwepa kumhusisha na uozo huo wa CCM.

Je; Mheshimiwa Rais kajifunza kitu kutoka katika kosa hilo, na kutoka katika yaliyojiri Dodoma? Ni suala la muda tu tutapata jibu la swali hili.Tafakari.

Nukuu: Johnson Mbwambo: Toleo la 182 20 Apr 2011
 
Naona watu mnazuzuka na hilo jina la Nyerere.....
Sio jina ata ukifuata record yake twambie nani alipata kusema hayo aliyoyasema miaka minne iliyopita kubali kama baba kama mtoto.Tena anasema kwa kumtaja mtu kwa jina ...aahaa ebu nyani ngabu wewe ni mkongwe humu sema basi ukweli ..
 
Nilishawahi kusema Kuwa watanzania ni viumbe adimu duniani. Kwanza kwa kisahau na kuridhika kwa maneno. Naona watanzania wakiliwazwa na mbwembwe za muda huu wa uchaguzi na kushobokea visiki vilivyotufikisha hapa tulipo. Ni hatari sana kuingiza Kwenye demokrasia mtu anaetumia pesa na mtandao wa matajiri nyuma yake kwani madhara yake hayakwepeki kamwe.

Haya magamba tunayoyaona leo yasingekuwa sugu kama mwenyekiti wetu yasingemsaidia kuingia Kwenye system na madhara yake ni hayo kuyaonea Aibu na dhana yote Ya utawala bora kufutika yanapokomaa na kuota mizizi. Nawapa watanzania wakiwa na ndoto za kurudia makosa Yale yale.

Kinachoshangaza zaidi ni pale mtanzania mwenzetu anapokuja kifua mbele kupinga ukweli na uhalisia. Basi unajiuliza huyu ni mwenzetu ?

Anaishi Kwenye haya haya matukio Ya CCM ? Ni ukweli usiopingika Kuwa Kati ya watia nia wote nikimwangalia makongongoro ni yeye pekee naweza kumpa kura nyingi kwa nia Ya dhati Ya kuchukia rushwa. Watanzania wengi hawajatembea nchi za watu japo hapo Rwanda waonje raha Ya kuishi katika corruption free zone.

Wengi wamezaliwa na rushwa kukua na rushwa sasa rushwa ni sehemu Ya utamaduni wetu. Watanzania wanaojitambua kama DSN endeleeni kuelimisha kwani kuna siku wataamka na kujitambua.

Otherwise nawaona watanzania wangu wakirudia makosa Ya miaka yote. Nami nasema kwa Kuwa kipaumbele chetu pekee ni Rushwa basi makongoro historia yake , dhamira yake vinatosha Kabisa kutusaidia kuondokana na hii Kansa mengine yote watanzania tutamsaidia ndugu yetu makongoro
 
Makongoro ni bidhaa adimu sana kwa taifa hili.

Hakuna mwingine mwenye nguvu ya kukemea mafisadi zaidi ya makongoro pengine na muhongo ila makongoro the best.
 
Nilishawahi kusema Kuwa watanzania ni viumbe adimu duniani. Kwanza kwa kisahau na kuridhika kwa maneno. Naona watanzania wakiliwazwa na mbwembwe za muda huu wa uchaguzi na kushobokea visiki vilivyotufikisha hapa tulipo. Ni hatari sana kuingiza Kwenye demokrasia mtu anaetumia pesa na mtandao wa matajiri nyuma yake kwani madhara yake hayakwepeki kamwe.

Haya magamba tunayoyaona leo yasingekuwa sugu kama mwenyekiti wetu yasingemsaidia kuingia Kwenye system na madhara yake ni hayo kuyaonea Aibu na dhana yote Ya utawala bora kufutika yanapokomaa na kuota mizizi. Nawapa watanzania wakiwa na ndoto za kurudia makosa Yale yale.

Kinachoshangaza zaidi ni pale mtanzania mwenzetu anapokuja kifua mbele kupinga ukweli na uhalisia. Basi unajiuliza huyu ni mwenzetu ?

Anaishi Kwenye haya haya matukio Ya CCM ? Ni ukweli usiopingika Kuwa Kati ya watia nia wote nikimwangalia makongongoro ni yeye pekee naweza kumpa kura nyingi kwa nia Ya dhati Ya kuchukia rushwa. Watanzania wengi hawajatembea nchi za watu japo hapo Rwanda waonje raha Ya kuishi katika corruption free zone.

Wengi wamezaliwa na rushwa kukua na rushwa sasa rushwa ni sehemu Ya utamaduni wetu. Watanzania wanaojitambua kama DSN endeleeni kuelimisha kwani kuna siku wataamka na kujitambua.

Otherwise nawaona watanzania wangu wakirudia makosa Ya miaka yote. Nami nasema kwa Kuwa kipaumbele chetu pekee ni Rushwa basi makongoro historia yake , dhamira yake vinatosha Kabisa kutusaidia kuondokana na hii Kansa mengine yote watanzania tutamsaidia ndugu yetu makongoro
Wapo watu wanaokula chakula cha mafisadi,wanakunywa chai ya mafisadi, na kupanda magari ya mafisadi ukweli huu hawataweza kuusadiki kwani ni ukweli mchungu.
 
Nimeisoma hotuba yake ya jana na nimejifunza kitu.Ameonesha uhalisia wa hali ilivyo haswa,sijamwona aliweza kusema Maneno haya zaidi ya watu kuahidi kurudia "uchumi imara,uchumi kukua n.k pasipo kudadavua uchumi unakwama wapi.M.Nyerere kutamka wakurugenzi wanapigiwa simu na wakikataa wanahamishwa,VIBAKA wanagawana n.k,hakika anaelewa nini kinaendelea huku chini,naiona sauti kali,kutumia neno vibaka ni kuonesha hasira iliyozidi na isiyo njema sana,inamaana kuna watu anawaona waziwazi kuwa vibaka na anaona wanagawana madili,ole wao.Hata kama hatafanana sana na baba yake ila tukumbuke it always runs in the blood,kuna vitu lazima vitamtambulisha kwamba yeye ni damu ya ukoo Wa Nyerere,na kwa hiyo,misingi ya malezi aliyolelewa katika familia kwa yale wanayoyaamini,naamini malezi ya kifamilia yana mchango mkubwa sana,mfano ukilelewa katika familia ambayo watu hawaamini wizi ni dhambi ikawa hivyo katika maisha pia hili linaweza likakuandama ukubwani hata kinyume chake.Sasa tukielewa misingi ya malezi ya familia ya Mwalimu Nyerere tunaweza pia kuelewa kirahisi kama familia wamelelewa katika misingi yenye kuamini nini in nini
 
Kaka right ungejua system zinavyo fanya kazi duniani,usinge thubuti kusema hvyo maana hapa duniani kila mtu ana boss au wajanja wake na mnyonge wake.usidhani huyo makongoro anaweza shinda uraisi kwa kusimama peke yake.eg leo Dr.slaa awe raisi unadhani anaweza mwambia chochote mbowe.siku zote hao ni figure tu desicion na mambo mengine anaambiwa.kumbuka hata raisi ana mwili na nyama anaweza pinduliwa au kuuwawa hasa ukienda tofaut na wadau wako.cha msingi wapatikane watu wenye mlengo sawa vngnevyo arudi nyerere orijino na ujamaa urudi watu wasitawaliwe nafsi zao na tamaa
 
Kuna mawazo mazito kwenye uzi huu JF. Kutangaza nia ni kitu kimoja kuwa na utashi wa kisiasa ni kitu kingine. Nchi yetu viongozi hawana utashi wa kisiasa. Wanaotangaza nia wengi wao hushiriki kwenye baraza la mawaziri ambako maamuzi yote ya kisiasa hufanyika. Inakuwaje leo hao hao wanalalamikia maamuzi hayohayo waliyoyafanya! Wana JF mnisaidie kunipa jina la mmoja wao tu ambaye katika hilo baraza la mawaziri amekuwa mwiba katika kukubali maamuzi yasiyo na tija wala utashi wa kisiasa!
 
Makongoro kweli ukimwangalia machoni pasi na shaka kabisa unapata jibu la vyema. Sululisho la masikini na matajiri katika utu na haki ya kibinadamu
 
Hivi ukawa mbona wanachama wengine hawatangazi nia zaidi zaidi ya slaa+mbowe, kula siku hao hao, au hakuna uhuru wa katiba
 
Back
Top Bottom