TUJITEGEMEE
Platinum Member
- Nov 6, 2010
- 27,552
- 28,539
Huwe zi kutreini red brigade mia tano walinde kituo kimoja? Hiyo itakuwa ni upotevu wa rasilimali watu. Ninavyodhani redi briged 1 anatosha kwa kila kituo.
wacha kura zilindwe hofu yenu ni nini?
Hivi hufahamu kuwa kwa sasa: Ni Watanzania million 10 tu ndiyo wanachama katika vyama vya siasa vilivyopo Tanzania. Kati ya hao millioni 6 wako CCM, mil 3.5 wako CHADEMA na 0.5 ml wako kwenye vyama vingine. Hivyo hadi sasa CCM ndiyo chama kikuu cha siasa kwa maana ya kuwa na wanachama wengi zaidi. Watazania millioni 40 hawako kwenye chama cho chote cha siasa.
Wewe fikiria eti vijana 500 wa UKAWA, 700 wa CCM na 50 wa ACT watakuwa wamekizunguka kila kituo cha kupigia kura hapo tarehe 25 Oct kuanzia saa mbili asubuhi hadi kesho yake wakilinda kura za vyama vyao visirubuniwe! Vijana hawa ambao kwa vyo vyote vile wengi wao watakuwa ni wale wasio na kazi (jobless), wakiwemo wavuta bangi, watumiaji wa viroba haramu (gongo), vibaka n.k. Watakuwa wameweka uzio mita 200 toka kituo cha kura. Hakuna huduma choo wala nyingine yo yote kuwahudumia vijana hawa.
Sasa tunaaminishwa kwamba kwa hali hiyo moto hautawaka kweli? Hili wala si jambo la wanasheria, ni suala la usalaama wa wananchi na halina mjadala.
nani kakuambia sisi tutakaolinda Kura zetu ni ma jobless? kama Huna taarifa mimi ninaaza likizo rasmi kwaajili ya kupiga Kura na kulinda Kura kwa kukaa mita200 toka kituoni
Hivyo viroba utakua umekunywa wewe