Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,313
- 4,750
Wewe fikiria eti vijana 500 wa UKAWA, 700 wa CCM na 50 wa ACT watakuwa wamekizunguka kila kituo cha kupigia kura hapo tarehe 25 Oct kuanzia saa mbili asubuhi hadi kesho yake wakilinda kura za vyama vyao visirubuniwe! Vijana hawa ambao kwa vyo vyote vile wengi wao watakuwa ni wale wasio na kazi (jobless), wakiwemo wavuta bangi, watumiaji wa viroba haramu (gongo), vibaka n.k. Watakuwa wameweka uzio mita 200 toka kituo cha kura. Hakuna huduma choo wala nyingine yo yote kuwahudumia vijana hawa.
Sasa tunaaminishwa kwamba kwa hali hiyo moto hautawaka kweli? Hili wala si jambo la wanasheria, ni suala la usalaama wa wananchi na halina mjadala.
Sasa tunaaminishwa kwamba kwa hali hiyo moto hautawaka kweli? Hili wala si jambo la wanasheria, ni suala la usalaama wa wananchi na halina mjadala.