Tusherekee Uhuru wa Tanganyika na shujaa wetu John Samuel Malecela

Lengeri

Senior Member
Jul 3, 2009
180
15
Mzee Malecela kipindi akiwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais alithubutu kutuletea serikali ta Tanganyika akishirikiana na wabunge 55 miongoni mwao Njelu Kasaka na Philip Marmo. Alikubali kukosana na Mwalimu kuwapa watanganyika haki yao, akaminywa na woga wa Mwalimu Nyerere....

Mzee Malecela ni shujaa wa Tanganyika pamoja na G55.
 
Mi nilianzishaga thread humu ndani,ya kuwakumbuka mashujaa kama hao,na wengine waliochakachuliwa na serikali, wakachakachuka. Mfano Njelu,Marmo,Kolimba,...
 
Tanganyika yetu itarudi tu, tushiriki kuandika KATIBA mpya yenye urejesho Tanganyika
 
Yaah!

Hii issue iliwagombanisha kabisa mwalimu na Malecela.

Hii ndo ilimfanya mwalimu akamwita "Muhuni"?
 
Mzee Malecela kipindi akiwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais alithubutu kutuletea serikali ta Tanganyika akishirikiana na wabunge 55 miongoni mwao Njelu Kasaka na Philip Marmo. Alikubali kukosana na Mwalimu kuwapa watanganyika haki yao, akaminywa na woga wa Mwalimu Nyerere....

Mzee Malecela ni shujaa wa Tanganyika pamoja na G55.
Angekuwa marehemu tungekuwa na sababu ya kusema ni shujaa kuwa ni kifo tu kilimzuia kutimiza ndoto zake, lakini leo yupo ule ushujaa umeishia wapi kwa nini asiuendeleze.
 
Pamoja na Nyerere kuivunja hoja ya serikali ya Tanganyika Malecela hajawahi Kujuta kuisimamia. Huyu ni shujaa kwa historia ya Tanganyika.
 
Kwa hoja ya kutaka kuleta serikali ya Tanganyika alithubutu.Tufahamu kwamba wakati ule haikuwa rahisi kama tunavyofikiria na ndio maana ilimgharimu kama ilivyokuwa kwa mzee Jumbe.Anastahili kuwa shujaa.
 
Mzee Malecela kipindi akiwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais alithubutu kutuletea serikali ta Tanganyika akishirikiana na wabunge 55 miongoni mwao Njelu Kasaka na Philip Marmo. Alikubali kukosana na Mwalimu kuwapa watanganyika haki yao, akaminywa na woga wa Mwalimu Nyerere....

Mzee Malecela ni shujaa wa Tanganyika pamoja na G55.

Ah wapi! Unajua maana ya neno "shujaa?" jibu lako unganisha na jibu kwa nini wana CCM wenzake wanamwita Katapila/greda!
 
Kwa hoja ya kutaka kuleta serikali ya Tanganyika alithubutu.Tufahamu kwamba wakati ule haikuwa rahisi kama tunavyofikiria na ndio maana ilimgharimu kama ilivyokuwa kwa mzee Jumbe.Anastahili kuwa shujaa.

Ni kweli kabisa haikuwa raisi kuibua Tanganyika wakati Nyerere akiwa hai.Nathubutu kusema ni rahisi sana sasa hivi,wapi G55 wapi Njelu Kasaka.
 
hana ushujaa wowote huyu mzee,ila ana uchu sana wa madaraka urais

Mbona mwenye uroho na uraisi anajulikana ,usimsingizie mzee wa watu. alishakubali matokeo siku nyingi ndio maana 2005 hakugombea pamoja Nyerere kutokuwapo
 
Impious CCM shouting Tanganyika is dead,finished,kwisha kabisa,dead and buried,but somehow every 9 Dec they smuggle him in through the backdoor to a lavish birthday bash- through out the pomp and brass ,happy bithday Tanzania Bara we sing on! Surely we must be mad.
 
Unamzungumzia Jumanne Saidi Malecela? Hana lolote huyu J4 kwani angekuwa na nia ya ukweli angeendeleza hoja hiyo baada ya mchonga kuvuta.
 
Kwa kweli mzee J.S.Malecela anastahili kupewa heshima ya kuitwa MTANGANYIKA HALISI.:lol::ballchain:
 
Kwa kweli mzee J.S.Malecela anastahili kupewa heshima ya kuitwa MTANGANYIKA HALISI.:lol::ballchain:

Fisadi tu huyo na mroho wa Madaraka! Ndio maana aligaragazwa na kijana wa Drs la Saba, John Lusinde kwenye ubunge wa Jimbo la Mtera! R.I.P. Tingatinga la kuiba kura za Magamba, enzi zako zimekwisha!
 
Mmmh! may be alikuwa na nia kweli lakini mbona baada ya nyerere kufa hatujaona jitihada zake tena
 
hana ushujaa wowote? alikuwa fisadi wa kwanza wa Tanzania na kuhadi wa wajapani kwenye ishu za magari ya wabunge ila Lowasa alimpatia!
 
Back
Top Bottom