Tushee haya MAUMIVU!

Tushee haya MAUMIVU!

Siku hizi kuna vifaa wanaweka ili uweze kusikia, ulishawahi jaribu?

Na pia jiunganishe chama cha viziwi ili uweze kupata msaada.
hili la chama cha viziwi ni mara 4 nmeenda ofisi zao kwa huu mkoa (MTWARA) sikifanikiwa kuwakuta hili ni moja ya mambo nayotaka kuyafanya
 
Pole sana ndg.. Mie pia nina rafiki yangu alipata hilo tatizo akiwa sekondari school, kadri siku zinavyosonga anapoteza kabisa uwezo wa kusikia vyema. Mungu kamuongoza kafika chuo Kikuu (Education) mwaka wa pili mambo yakagoma, tatizo likazidi ikabidi ahairishe masomo....Baada ya muda kashauriwa kusomea ualimu wa viziwi...Mwaka huu Mungu akijalia atahitimu masomo yake.

Endapo nawe mambo yataendelea kuwa magumu katika upatikanaji wa ajira jaribu kufanya hivyo..
Mungu akutangulie [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120].
 
vile vifaa nasikia vina maumivu yake, maana ukikivaa jamaa akikwarua hata kdg unaskia balaa.

kuna jamaa yangu yuko na tatizo ilo baada ya kuugua akiwa kijana huwa anavaa mara 1 sana akisema vinaumiza.
ni kweli mkuu vinasaidia kidogo sana huku vina madhara makubwa zaidi
 
mkuu hivi vidude ninavyo tatizo ni kuwa some vinawakubali Some vinawakataa binafsi havinisaidii
Jinsi kukusaidia inaweza kuwa Ngumu yaani unavyojibu ni kama mtu ambaye 'mgonjwa yeye na Daktari ni yeye yeye' Basi watu wa dizaini hiyo wana tabu hao..! Hawashauriki.
 
Si kwamba ninakusimanga ila kama unaenda kuomba kazi kuwa wewe ni kiziwi unaomba kazi ya ualimu huku huna hata ujuzi wa kusema na viziwi nadhani hapo ndio una shida.
Rudi kasome course ya viziwi nakuhakikishia hutaenda skuli 2 kabla hujapata kazi
mkuu mimi ni mwalimu wa kawaida si viziwi!

Nina uzoefu na uwezo mkubwa wa kufundisha wanafunzi wa kawaida bila shida yoyote!

Shule nilizoomba zote ni za kawaida si viziwi!

Nimewah kujitolea kufunfisha shule ya viziwi na hapo ndipo nilipojifunzia lugha ya alama so lugha alama naifahamu kwa kiasi chake
 
Basi jikite katika kuelewa lugha ya alama, hiyo ndio fursa uliyonayo mkuu.

Tuna upungufu mkubwa wa wataalamu wa lugha ya alama.
 
mkuu hivi vidude ninavyo tatizo ni kuwa some vinawakubali Some vinawakataa binafsi havinisaidii
Pole saana, jaribu kutafu high ended kwenye Alibaba

Mambo yamekua mengi na Mengi yamekua Mambo
 
Pole sana ndg.. Mie pia nina rafiki yangu alipata hilo tatizo akiwa sekondari school, kadri siku zinavyosonga anapoteza kabisa uwezo wa kusikia vyema. Mungu kamuongoza kafika chuo Kikuu (Education) mwaka wa pili mambo yakagoma, tatizo likazidi ikabidi ahairishe masomo....Baada ya muda kashauriwa kusomea ualimu wa viziwi...Mwaka huu Mungu akijalia atahitimu masomo yake.

Endapo nawe mambo yataendelea kuwa magumu katika upatikanaji wa ajira jaribu kufanya hivyo..
Mungu akutangulie [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120].
asante sana kaka nami pia huko ndiko niendako!

Masharti ya kusomea elimu maalumu ni kuwa mhitimu wa Grade A kwa bahati mbaya kuna matatizo yalitokea kwa walezi wangu so hawana uwezo wa kuniendeleza kwa sasa!

Lakini lengo la kusomea ualimu ni kuelekea huko huko elimu maalum mkuu!
 
Jinsi kukusaidia inaweza kuwa Ngumu yaani unavyojibu ni kama mtu ambaye 'mgonjwa yeye na Daktari ni yeye yeye' Basi watu wa dizaini hiyo wana tabu hao..! Hawashauriki.
samahani kama nimekukwaza mkuu!

Vifaa hivi ninavyo bahati mbaya havinisaidii mkuu nikivaa:

-napata maumivu ya kichwa
-maumivu ya sikio lenyewe
-kizunguzungu
-napoteza zaidi uwezo wa kusikia
-nakosa utulivu kwa maana mtu akikwaruza kitu sauti yake inasikika kwa nguvu hadi unaumia sikio licha ya kuwa in low volume

Hivyo havinisaidii
 
Basi jikite katika kuelewa lugha ya alama, hiyo ndio fursa uliyonayo mkuu.

Tuna upungufu mkubwa wa wataalamu wa lugha ya alama.
ni kweli nadhani inabidi nikajiendeleze katika lugha ya alama si ndio!?
 
Si kwamba ninakusimanga ila kama unaenda kuomba kazi kuwa wewe ni kiziwi unaomba kazi ya ualimu huku huna hata ujuzi wa kusema na viziwi nadhani hapo ndio una shida.
Rudi kasome course ya viziwi nakuhakikishia hutaenda skuli 2 kabla hujapata kazi

Wewe mwenzetu umesomea hiyo taaluma uliyoitaja?// Halafu kuita vi...ni lugha ya 'kuwabagua' au 'kuwanyanyapa' wenye matatizo hayo...lugha sahihi ni 'wenye ulemavu wa kusikia'
 
nashukuru. Sana ndugu yangu!
Kuna wakati tunalazimika kuweka matatizo yetu pembeni na kumshukuru Mungu, Baadae mambo yakiwa Sawa Utatazama ulipo toka na Mapito uliyopitia na kufurahia kwamba hukukata tamaa, Mungu akupe faraja katika kipindi hiki kigumu.
 
Back
Top Bottom