Tushee haya MAUMIVU!

Tushee haya MAUMIVU!

Mpauko

R.I.P
Joined
Jan 19, 2019
Posts
2,323
Reaction score
3,463
Habarini wanajamii forum!
Tuingie kwenye mada moja kwa moja..

Mimi ni kijana aged 24 years,katika kipindi fulani cha maisha nikiwa shule ya msingi nilipoteza uwezo wa kusikia (deafness) nasikia lakini si kwa ufanisi so i need special care while talking!

Mwaka uliopita nimehitimu mafunzo ya ualimu Grade A,kufika kitaa kusaka vibarua hapa na pale coz life ni tight mno! Kupata vibarua ikawa msala coz ya hili tatizo unaambiwa tu wewe husikii huwez fanya hii kazi!

Eeh! Unabaki umezubaa tu unajiask sasa kutosikia kwangu na hii kazi kuna uhusiano gani? Mbona kazi haihitaji too much communication?

Anyway unaenda tu kusaka mahala pengine wanakuangaliaaaaa mwisho wanasema sijui tukusaidiaje! Unabaki frustrated mbna me nahitaji ajira instead naulizwa nisaidiwajwe!!!

Baada ya kusota bila mafanikio nikaona life is toi short acha nitumie kataaluma kangu kabla sijafa so nikafind shule binafsi nijitolee majibu yao unaweza tamani ufe! Ardhi ikumeze upotee hii dunia!! Ila unaambiwa uvumilivu ni mafanikio!

Sasa leo nimeenda private moja ya mwisho hapa town nkaandaa barua yangu ya kuomba kujitolea nikapeleka bwana nikatolewa mkuu na kibarua changu tena na sister ambaye ndo msimamizi wa hiyo shule!

Hata kutembea nilishindwa maana ni maumivu tu kosa langu ni nini? Tumeshaambiwa tusihoji maamuzi ya muumba wetu hivyo sina la kumlaumu ila MENGINE HAYA YANAUMIZA SANA!

jaman msiwe mnafanya hivi maana hata sisi tuna mioyo sio chuma sema tu hatuna wa kumlilia!
 
Siku hizi kuna vifaa wanaweka ili uweze kusikia, ulishawahi jaribu?

Na pia jiunganishe chama cha viziwi ili uweze kupata msaada.
Vile vifaa nasikia vina maumivu yake, maana ukikivaa jamaa akikwarua hata kidogo unaskia balaa.

Kuna jamaa yangu yuko na tatizo ilo baada ya kuugua akiwa kijana huwa anavaa mara 1 sana akisema vinaumiza.
 
Si kwamba ninakusimanga ila kama unaenda kuomba kazi kuwa wewe ni kiziwi unaomba kazi ya ualimu huku huna hata ujuzi wa kusema na viziwi nadhani hapo ndio una shida.
Rudi kasome course ya viziwi nakuhakikishia hutaenda skuli 2 kabla hujapata kazi
 
vile vifaa nasikia vina maumivu yake, maana ukikivaa jamaa akikwarua hata kdg unaskia balaa.

kuna jamaa yangu yuko na tatizo ilo baada ya kuugua akiwa kijana huwa anavaa mara 1 sana akisema vinaumiza.
Hivi kwani sio wanakufanyia oparesheni?
 
Fursa nzuri inakusubiri baadae usiumie kwa hayo unayoyapitia kwa sasa.

MAGA 2020
 
Siku hizi kuna vifaa wanaweka ili uweze kusikia, ulishawahi jaribu?

Na pia jiunganishe chama cha viziwi ili uweze kupata msaada.
mkuu hivi vifaa vina matokeo hasi makubwa mno

Ninavyo ila nilitumia mwezi tu nikaweka ndani
-yaan mtu hata akiburuza mguu unamsikia hata akikunja kunja karatasi kibaya zaidi ipite pikipiki mbona utakivua.
-kizunguzungu
-maumivu ya masikio
-unapoteza uwezo wa kusikia kwa rate ya ajabu yaan unazidi kuharibu masikio

So naona havina msaada
 
Hii ndo kitu nilitaka kumwambia, nunua vifaa vya kusaidia kusikia

Mambo yamekua mengi na Mengi yamekua Mambo
mkuu hivi vidude ninavyo tatizo ni kuwa some vinawakubali Some vinawakataa binafsi havinisaidii
 
Back
Top Bottom