Tushee haya MAUMIVU!

Tushee haya MAUMIVU!

Najaribu kuvaa viatu vyako daaah! Aisee hii dunia haina usawa kabisa!

MUNGU akutimizie haja ya moyo wako mkuu

Young kilimanjaro
hahaha mkuu umenifurahisha kajiatu kenyew ninako pea moja na wewe wataka ukavae!!!!

Mkuu nashukuru kwa kujali kwa hakika katika dunia hii haijawahi kuwa sawa wala haitokuwa sawa abadan

Hakika maombi yako kwangu na yawe na kheri niweze timiza hitaji la moyo wangu mkuu,ALAMSIK
 
Kuna settings zinazotakiwa kufanywa, alienda kwa wataalam?
vile vifaa nasikia vina maumivu yake, maana ukikivaa jamaa akikwarua hata kdg unaskia balaa.

kuna jamaa yangu yuko na tatizo ilo baada ya kuugua akiwa kijana huwa anavaa mara 1 sana akisema vinaumiza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda Muhimbili ukawaulize wataalamu, kuna jinsi ya kurekebisha (setting), ila wanachaji kama laki 3 kwa kila sikio (kama unatumia kwa yote).
mkuu hivi vifaa vina matokeo hasi makubwa mno

Ninavyo ila nilitumia mwezi tu nikaweka ndani
-yaan mtu hata akiburuza mguu unamsikia hata akikunja kunja karatasi kibaya zaidi ipite pikipiki mbona utakivua.
-kizunguzungu
-maumivu ya masikio
-unapoteza uwezo wa kusikia kwa rate ya ajabu yaan unazidi kuharibu masikio

So naona havina msaada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habarini wanajamii forum!
Tuingie kwenye mada moja kwa moja..

Mimi ni kijana aged 24 years,katika kipindi fulani cha maisha nikiwa shule ya msingi nilipoteza uwezo wa kusikia (deafness) nasikia lakini si kwa ufanisi so i need special care while talking!

Mwaka uliopita nimehitimu mafunzo ya ualimu Grade A,kufika kitaa kusaka vibarua hapa na pale coz life ni tight mno! Kupata vibarua ikawa msala coz ya hili tatizo unaambiwa tu wewe husikii huwez fanya hii kazi!

Eeh! Unabaki umezubaa tu unajiask sasa kutosikia kwangu na hii kazi kuna uhusiano gani? Mbona kazi haihitaji too much communication?

Anyway unaenda tu kusaka mahala pengine wanakuangaliaaaaa mwisho wanasema sijui tukusaidiaje! Unabaki frustrated mbna me nahitaji ajira instead naulizwa nisaidiwajwe!!!

Baada ya kusota bila mafanikio nikaona life is toi short acha nitumie kataaluma kangu kabla sijafa so nikafind shule binafsi nijitolee majibu yao unaweza tamani ufe! Ardhi ikumeze upotee hii dunia!! Ila unaambiwa uvumilivu ni mafanikio!

Sasa leo nimeenda private moja ya mwisho hapa town nkaandaa barua yangu ya kuomba kujitolea nikapeleka bwana nikatolewa mkuu na kibarua changu tena na sister ambaye ndo msimamizi wa hiyo shule!

Hata kutembea nilishindwa maana ni maumivu tu kosa langu ni nini? Tumeshaambiwa tusihoji maamuzi ya muumba wetu hivyo sina la kumlaumu ila MENGINE HAYA YANAUMIZA SANA!

jaman msiwe mnafanya hivi maana hata sisi tuna mioyo sio chuma sema tu hatuna wa kumlilia!
Ngoja nikwambie Kisa kizuri cha kukutia moyo,

Mkulima mmoja Alikua na Punda wake aliyempenda Sana, kwa bahati mbaya siku moja Wakati wanarejea kutoka Shamba jirani na nyumbani kwake Yule Punda akatumbukia kwenye shimo refu.

Mkulima akawaza namna ya kumtoa akashindwa, akaita majirani nao wakawaza kwa pamoja wakashindwa! Likaja wazo kuwa, wamzike tu maana hata hivyo Punda mwenyewe alikua Mzee Sana!

Punda kusikia vile akalia kwa Uchungu Sana Sana, wanakijiji kwa Umoja wakaanza kuchukua mawe, Mchanga, kokoto, miti na kila kilichokaribu kutupia mle Shimoni.

Punda akajitafakari, Akaona atakufa kizembe saaaana! Akaacha kulia akatumia zile taka na mawe na Mchanga kufanya ngazi ya kupandia juu. Kila walipotupa, Punda alijitingisha japo Kwa maumivu na kupanda juu Kidogo hadi Akaja kutoka nje ya shimo akiwa hai japo ana vidonda.

Wanakijiji wako Leo ni waajiri, taka wanazotumia ni ulemavu wako, acha kulia, acha kulaumu, Tumia akili Aliyekupa Mungu kufanya jambo, sio lazima iwe kufundisha! Mungu ameweka special and unique talent kwa kila mtu.

Japo utaumizwa kama Punda lakini utafanikiwa na kila mtu atashangaa. Samehe na endelea mbele.

Kaka yako

Elli wa JF

Ifakara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole mkuu kwa mtihani huo.pia shukrani zikufikie kwakua umetambua m/mng ndio mjuzi na mpangaji wa kira jambo.pia lazima ujue kabla ujafa ujaumbika,hivyo ucjishangae wara ucckitike kwa kua umepoteza uwezo wa kusiki.kubwa uckati tamaa ktk kutafuta ajira,kira unahisi unaweza kwenda kupeleka maombi peleka,kwani cku isiyo na jina utafanikiwa.m/mng akupe imani na uvumilivu ktk mapitio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe mwenzetu umesomea hiyo taaluma uliyoitaja?// Halafu kuita vi...ni lugha ya 'kuwabagua' au 'kuwanyanyapa' wenye matatizo hayo...lugha sahihi ni 'wenye ulemavu wa kusikia'
Lugha haimuongezei utu wala chochote ni nyie mnao watafutia majina ndio mnaowanyanyapaa
 
Aisee Pole sana ndugu kwa hayo unayoyapitia.Hii dunia yetu imejaa tabu na mateso mda mwingi.Kila mmoja ana jambo linalomuumiza haswa maishani.Msingi usikate tamaa endelea ku fight Mungu anakuona atakubarikia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
embu jaribu kufanya issue ambayo itaendana na hali yako..... YAANI JARIBU BIASHARA LABDA AU KITU KINGINE.
 
Ngoja nikwambie Kisa kizuri cha kukutia moyo,

Mkulima mmoja Alikua na Punda wake aliyempenda Sana, kwa bahati mbaya siku moja Wakati wanarejea kutoka Shamba jirani na nyumbani kwake Yule Punda akatumbukia kwenye shimo refu.

Mkulima akawaza namna ya kumtoa akashindwa, akaita majirani nao wakawaza kwa pamoja wakashindwa! Likaja wazo kuwa, wamzike tu maana hata hivyo Punda mwenyewe alikua Mzee Sana!

Punda kusikia vile akalia kwa Uchungu Sana Sana, wanakijiji kwa Umoja wakaanza kuchukua mawe, Mchanga, kokoto, miti na kila kilichokaribu kutupia mle Shimoni.

Punda akajitafakari, Akaona atakufa kizembe saaaana! Akaacha kulia akatumia zile taka na mawe na Mchanga kufanya ngazi ya kupandia juu. Kila walipotupa, Punda alijitingisha japo Kwa maumivu na kupanda juu Kidogo hadi Akaja kutoka nje ya shimo akiwa hai japo ana vidonda.

Wanakijiji wako Leo ni waajiri, taka wanazotumia ni ulemavu wako, acha kulia, acha kulaumu, Tumia akili Aliyekupa Mungu kufanya jambo, sio lazima iwe kufundisha! Mungu ameweka special and unique talent kwa kila mtu.

Japo utaumizwa kama Punda lakini utafanikiwa na kila mtu atashangaa. Samehe na endelea mbele.

Kaka yako

Elli wa JF

Ifakara

Sent using Jamii Forums mobile app
ahsante sana kaka Elly kwa fundisho mzuri!

binafsi nimejifunza jambo kupitia kisa chako,daima sina muda wakulia nitalia mpaka lini? nimekubali matokeo na kupuuza yote ndio maana hadi sasa naendelea na juhudi bila kuchoka!

napenda nikufahamishe kuwa jitihada zangu zipo katika kila fursa iliyo mbele yangu hivyo nakutana na masuala haya ya kukatisha tamaa pande zote si ualimu tu!
naamini juhudi zangu Mungu anaziona IPO siku ataniinua nami
 
embu jaribu kufanya issue ambayo itaendana na hali yako..... YAANI JARIBU BIASHARA LABDA AU KITU KINGINE.
nashukuru kwa ushauri,naamini kuna issue nyingi za kufanya

mojawapo ni kujiajiri katika biashara au huduma,solution ambayo ni very alternative, bahati mbaya hali hairuhusu ndio maana unaweza kuna nikihangaika na kutafuta vibarua hivi.
 
Aisee Pole sana ndugu kwa hayo unayoyapitia.Hii dunia yetu imejaa tabu na mateso mda mwingi.Kila mmoja ana jambo linalomuumiza haswa maishani.Msingi usikate tamaa endelea ku fight Mungu anakuona atakubarikia.

Sent using Jamii Forums mobile app
ameen naamini Mungu atanigusa tena nami,cha msingi ni kumkumbuka Mungu
 
Pole mkuu kwa mtihani huo.pia shukrani zikufikie kwakua umetambua m/mng ndio mjuzi na mpangaji wa kira jambo.pia lazima ujue kabla ujafa ujaumbika,hivyo ucjishangae wara ucckitike kwa kua umepoteza uwezo wa kusiki.kubwa uckati tamaa ktk kutafuta ajira,kira unahisi unaweza kwenda kupeleka maombi peleka,kwani cku isiyo na jina utafanikiwa.m/mng akupe imani na uvumilivu ktk mapitio.

Sent using Jamii Forums mobile app
ameen ahsante sana kwa kunibariki kaka
 
mkuu hivi vifaa vina matokeo hasi makubwa mno

Ninavyo ila nilitumia mwezi tu nikaweka ndani
-yaan mtu hata akiburuza mguu unamsikia hata akikunja kunja karatasi kibaya zaidi ipite pikipiki mbona utakivua.
-kizunguzungu
-maumivu ya masikio
-unapoteza uwezo wa kusikia kwa rate ya ajabu yaan unazidi kuharibu masikio

So naona havina msaada
Kuna watu wana madhaifu makubwa japo hayaonekani wala hayana cheti cha daktari, wanalia na nafsi zao tu daily lakini bado hawachoki kuliangalia life katika angle nyingine

Angalia zaidi ulichobakiza kuliko ulichopoteza maana kama viungo vingine vinafanya kazi bhasi amini ,Hakuna litakaloshindikana

nashukuru kwa ushauri mkuu,nipo natazama mbele mkuu that's why thread hii hailaumu nilichopoteza Bali inaonyesha juhudi za kuyakabili maisha.
 
Back
Top Bottom