Tushauriane kuhusu water pump

napenda

JF-Expert Member
Jul 14, 2015
485
90
Mimi ni mdau wa kilimo, naomba mwenye uelewa na kama picha ipo tupia hapa, lengo la kuanzisha maada ni kurahisisha kupatikana kwa taarifa muhimu kuhusu water pump hivyo inaweza kuhamasisha vijana tukatumia fursa ipasavyo na kwa wakati . Nimesikia kuwa zile mashine za kusaga zinazo tumia dizel huwa zinauwezo wa kuvuta maji, mwenye uelewa na picha tupia hapa, pia kwa shamba la hecta moja aina gani ya pump inafaa.
 
Hili wazo jema sana, tuachane na kilimo cha mazoea, Kama tukipata aina mbalimbali za waterpump na jinsi zinavyo fanya kazi itapendeza sana
 
Mkuu Water Pump nzuri ni za Honda tu basi. Tena kama unataka kutoka fasta na shamba lipo kwa ajiri ya bustani(2-10acres)basi water pumb ya Honda "2-3 ndio mpango mzima babake. Nyingine michosho tu.
 
Zinabei gani?
 
Nilihitaji sana kufahamu lakin maelezo ya wataalamu hayajajitoshereza kwa mtu anayejifunza
 
Mm ni mkulima na natumia waterpumps katika shuhuli zangu,waterpumps zipo za aina nyingi,uwezo na ubora tofauti. Vitu muhimu vya kujua ni kuwa unahitaji water pump kwa ajili ya kusukuma maji umbali kiasi gani kutokea kwenye source ya maji na pia kuna umbali kiasi gani kutoka kwenye maji na utakapoweka pump. Pump zinazopatikana tanzania sanasana ni za kichina na japan. Pump za china ni bei rahisi,spare na matengenezo yake ni rahisi ila ubora na nguvu yake ni duni. Pump za japan ni bei ghali kidogo ila ni imara sana na zinanguvu ya kutosha. Asante
 
Mkuu Water Pump nzuri ni za Honda tu basi. Tena kama unataka kutoka fasta na shamba lipo kwa ajiri ya bustani(2-10acres)basi water pumb ya Honda "2-3 ndio mpango mzima babake. Nyingine michosho tu.

Sasa mkuu hebu tupe details, kwa mfano mimi nahitaji pampu kwa ajili ya kumwagilia ekari tatu hadi nne. Na maki nitayavuta kutoka chini (kisima) hebu dadavua nahitaji pampu yenye specification gani ili kazi yangu iwe rahisi.
 
Mimi ni mdau wa kilimo, naomba mwenye uelewa na kama picha ipo tupia hapa, lengo la kuanzisha maada ni kurahisisha kupatikana kwa taarifa muhimu kuhusu water pump hivyo inaweza kuhamasisha vijana tukatumia fursa ipasavyo na kwa wakati . Nimesikia kuwa zile mashine za kusaga zinazo tumia dizel huwa zinauwezo wa kuvuta maji, mwenye uelewa na picha tupia hapa, pia kwa shamba la hecta moja aina gani ya pump inafaa.

Kama upo dar nenda pale mtaa wa nkurumah uliza duka. linaitwa auto sokoni kuna pump nzuri sana pale, kama una shamba kubwa unaweza kutumia zile machine za kusaga za diesel then unafunga pump pale auto sokoni zipo nyingi tu kuanzia 10 horse power na pump za inch mpaka kumi,mfano hiyo kwenye picha inauzwa 1.1 mil na pump yake ya 6 inch inauzwa 750,000,hiyo ni 24 HP
 
Attachments

  • 1464736285179.jpg
    1464736285179.jpg
    68.5 KB · Views: 295
  • 1464736305280.jpg
    1464736305280.jpg
    68.6 KB · Views: 284
Sasa mkuu hebu tupe details, kwa mfano mimi nahitaji pampu kwa ajili ya kumwagilia ekari tatu hadi nne. Na maki nitayavuta kutoka chini (kisima) hebu dadavua nahitaji pampu yenye specification gani ili kazi yangu iwe rahisi.
Mkuu kwanza niambie maji yapo umbali gani kutoka chini?
 
Mkuu Water Pump nzuri ni za Honda tu basi. Tena kama unataka kutoka fasta na shamba lipo kwa ajiri ya bustani(2-10acres)basi water pumb ya Honda "2-3 ndio mpango mzima babake. Nyingine michosho tu.

Nauliza je water pump zinazopatikana ulaya hazifai?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom