Tusemezane: Umuhimu wa kuomba msamaha

Mla Bata

JF-Expert Member
Jan 24, 2013
6,749
13,765
Wasalaam.

Tusemezane kidogo,

Hii inawahusu sana wadada/wanawake lakini wanaume wenzangu tunaweza kujifunza kitu pia.

"Samahani",
Neno lenye herufi nane lakini lenye maana kubwa sana linapotamkwa na mkoseaji kwa mkosewa.

Tuelewane hapa, si lazima uwe umekosea au mkoseaji ili uombe msamaha lahasha! Omba msamaha pale unapohisi kuwajibika kwa kosa ama jambo fulani, lakini pia kuepusha "mambo yasiwe mengi".

Kwenye kuomba msamaha epuka kutumia neno "basi samahani", badala yake sema "nimekosea mpenzi wangu/mama angu (n.k), naomba nisamehe sana" Hii inasound vizuri zaidi, ikiwezekana hata facial, body expression yako ionyeshe au kumaanisha kile unachokitamka.

Hii si tu itakutofautisha na watu wengine, lakini pia itaonyesha uungwana wako mbele za watu.

Wasalaam!
 
Hii niikazie waielewe sana Wanaume mana wapo baadhi wanaonaga wakisema hilo neno ni kama suruali aliyovaa itabadilika na kuwa sketi.

Yaani yupo radhi azunguke weee ila sio kusema samahani. Utasikia tu
- basi yaishe
- basi nisamehe
-basi nimekosa. Lol
 
Well, ni kweli na niombe radhi kwa kuuelekezea uzi huu hasa kwa dada zetu badala yake uwe kwa walengwa wote both men & women ambao ni wagumu kuomba radhi.

Asante!
 
Nilimwambia demu nisamehe, alinitukana wee mwanaume fala Sana unaniomba msamaha kwani Mimi Mama yako? Ungekuwa lKaka yangu ningekuzabua mabao. Unamuombaje mwanamke samahani?
Nikawa mdogo Kama punje ya chumvi ya mezani

😂😂, that was so cruel, Nishapata hisia za mkoa anaotokea huyo binti/dada.

Siamini kama kuna tatizo kwa jinsia fulani kuiomba msamaha jinsia tofauti, au mtu ambae hayupo related nae.
 
Asante kwa ushauri OP.
Lakini kwanini hii post ipo chitchat?

Nilidhani inafit zaidi kuwa kwenye "general chat" badala ya kuweka kwenye jukwaa la mahusiano ama vinginevyo kwasababu hii inagusa mazingira yote.

Well, ningependa kufahamu ni wapi unafikiri inaweza kufit zaidi madam?

Karibu!
 
Labda kwenye mapenzi mahusiano na urafiki. Nikisoma dictionary yangu inaniambia chit chat ni kama maongezi yasiyo muhimu.
 
Hii niikazie waielewe sana Wanaume mana wapo baadhi wanaonaga wakisema hilo neno ni kama suruali aliyovaa itabadilika na kuwa sketi.

Yaani yupo radhi azunguke weee ila sio kusema samahani. Utasikia tu
- basi yaishe
- basi nisamehe
-basi nimekosa. Lol

Hapa nakazia zaidi yaani mtu kosa lake lakini atakavyoligeuza atakavyolizungusha ili mradi tu asiseme samahani, tena bora hata aseme hiyo basi nisamehe utasikia tu basi yaishe
 
Labda kwenye mapenzi mahusiano na urafiki.
Nikisoma dictionary yangu inaniambia chit chat ni kama maongezi yasiyo muhimu.

Oops! 😤, sikufikiria hilo, au sikuipa uzito mada husika. Shukrani kwa kuliona hilo, nadhani unafaa sana kuwa content manager hapa JF 😉 mods wakuongeze kwenye team, (kidding)

Well nadhani mods walio online wanaweza kunisaidia kuweka kwenye jukwaa husika zaidi Diversity Wand
 
apa nakazia zaidi yaani mtu kosa lake lakini atakavyoligeuza atakavyolizungusha ili mradi tu asiseme samahani, tena bora hata aseme hiyo basi nisamehe utasikia tu basi yaishe

Inaonekana huu ugonjwa wa kushindwa kuomba radhi ni mkubwa zaidi ya tunavyoufikiria, shida ni nini hasa, kuogopa kuonekana inferior, au nini zaidi??
 
Back
Top Bottom