Tusaidie watu wetu kupambana na COVID-19 Kwa Tech

msani

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
1,801
1,191
Wakuu habari za leo!!

Dunia imekumbwa na janga, na sisi kama Watanzania tumekumbwa tayari. Mambo ni mabaya, na shughuli nyingi zimesimama tayari kuanzia Taasisi za elimu, dini n.k na muda sio mrefu yatatoka matangazo mengine ya kuzuia huduma zingine ikiwemo masoko, safari n.k.

Nimeona leo serikali imeanza kutoa namba za wataalamu kama idadi ya 20 hivi na namba zao kwa wanaweza kupigiwa lakini ukweli hilo suala haliwezekani kwahiyo maswali ya watanzania yatakosa majibu.

Idadi yetu ya 58M ni wengi sana kuhudumiwa kwa njia ya simu. Hao wataalamu watachoka.

Nini kifanyike? nimewaza kwamba ile nia ya serikali waliyokuwa nayo wakati wanatoa tangazo lile linaweza kubadilishwa na kuwa kwenye teknolojia na hapo hao wataalamu wakaenda kuendelea na shughuli zingine za kufikia waathirika physically na tech ikaendelea kujibu maswali ya watanzania ikiwa ni pamoja na kuchakata taarifa mapema zaidi ili waathirika wafikiwe kwa haraka kwa alert ya system.

Mimi sio mtaalamu wa computer ingawa nina passion na haya mambo na ndio maana huwa nakaa humu kujifunza. Natamani ningekuwa nimejua yaani hapa ningekuja na solution moja kwa moja badala ya pendekezo.

Naomba kutoa hoja kwa wataalamu wa humu wakiwemo JF pia.

NB: Tunaweza kuongezea mawazo haya na kupata suluhu.

Karibuni jamani hatuna muda tena
 
Back
Top Bottom