Tusaidie watoto hawa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusaidie watoto hawa!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Straight corner, Apr 12, 2011.

 1. Straight corner

  Straight corner JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Habari zenu ndugu?
  Tukiwa katika shughuli za kiofisi wilayani Namtumbo katika kijiji cha Kilimasera, tulikutana na watoto wawili waliohitimu shule ya msingi Kilimasera mwaka 2010!

  Watoto hawa katika kuongea nao walitueleza kuwa walifaulu ila majina yao yaliuzwa wakidai majina yao yalionekana wilayani ila wakati yalipobandikwa hayakuonekana katika orodha. Wenyewe wanaonesha nia ya kuendelea na shule kwani walezi wao wanampango wa kuwapeleka wakasome kozi ya Nursing japo haikuwa kipaumbele chao.

  Naomba kama kuna mtu anayeweza kutupa uhakika kama watoto hawa walifaulu kweli au hawakufaulu ili ukweli ujulikane kwani nahisi kwa shule zetu zilivyo wanaweza kwenda shule na kutopishana saana na waliowatangulia na kama hawakufaulu basi waondoe hilo dukuduku mioyoni mwao!

  Namba zao za mtihani ni PS/1605010/13 na mwingine ni PS/1605010/20. Majina yao ninayo kama kutakuwa na umuhim wa kuyaweka bayana tufahamishane.
   
Loading...