Tusaidiane jamani kuhusu fursa hii

Matendo Andrew

JF-Expert Member
Apr 1, 2014
748
365
Nimekuwa nikijaribu kupitia pitia mitandaoni nikitaka kujua ukweli juu ya biashara hii ya tax kwa njia ya mtandao kwasababu nafikiria kuingia huko.

Nimekuwa pia nikitafuta madereva wa kazi hizo kupata uzoefu lakini naona ngoma droo. Sipati majibu ya matumaini moja kwa moja, kuna ambao wanasema kazi ngumu, kuna ambao wanasema sio kazi mbaya endapo huna cha kufanya na wachache wanaosema sio mbaya ni nzuri.

Najaribu kupiga kura naona ngoma droo, nikawaza kutumia majukwaa haya makini kupata uzoefu zaidi ili nione kama vimilioni 7 au 8 naweza kuweka huku? (Gari nitaendesha mwenyewe) ndio plan yangu, na nina vimiradi vingine ambavyo tayari vinatembea.

Karibu.
 
Ingia upime upepo mwenyewe.. kuna watakao kukatisha tamaa coz wanaona utafaidika sana pia kuna ambao wataka uje ule hasara kama wanayopata wao si unajua wa Afrika tena mtu akipatwa na baya fulani lile baya likipata mwingine tena anafurahi kwakua anaona hayupo pekee yake!

Ingia ujipe muda kiasi huko ukifanya utafiti tena Suka uwe mwenyewe hata kwa wiki 2 kama una nafasi
 
Mkuu Ni watu wachache Sana wa kukuonesha ukweli wa jambo flani .. kila unaemuuliza atakwambia Hali Ni tete ...

Mimi naongea with empirical evidence kwamba Uber Ni nzuri ... Najua watakuja wa kuponda ila amini nakwambia ukisema ukomae wewe Kama wewe kwa siku hutakosa 35-60 Kama faida baada ya kutoa gharama ya mafuta.

Hapa nilipo muda huu ninaoandika hii meseji rafiki yangu ananionesha leo mapato ya Jumla ni 75,000 .. Na hapo alianza kazi saa 6 mchana na amemaliza saa tatu usiku .. Kama angekomaa leo pato la Jumla lingekuwa 100,000+

Uber Kama ukiweza kupiga kazi mida yenye Rates nzuri hela ipo mzee.. midaa yenye rates nzuri huwa Ni kuanzia saa 11 alfajiri mpaka saa 2 asubuhi... Ukipiga kazi huo muda mchana unaweza hata kurelax maana hata rates huwa zinashushwa (madereva wa Uber ) watakuwa wanaelewa.
 
Biashara ya vyombo vya Moto ni pasua kichwa.Kabla hujaanza kutumbua m8 yako tafakari tena
 
Mkuu Ni watu wachache Sana wa kukuonesha ukweli wa jambo flani .. kila unaemuuliza atakwambia Hali Ni tete ...

Mimi naongea with empirical evidence kwamba Uber Ni nzuri ... Najua watakuja wa kuponda ila amini nakwambia ukisema ukomae wewe Kama wewe kwa siku hutakosa 35-60 Kama faida baada ya kutoa gharama ya mafuta.

Hapa nilipo muda huu ninaoandika hii meseji rafiki yangu ananionesha leo mapato ya Jumla ni 75,000 .. Na hapo alianza kazi saa 6 mchana na amemaliza saa tatu usiku .. Kama angekomaa leo pato la Jumla lingekuwa 100,000+

Uber Kama ukiweza kupiga kazi mida yenye Rates nzuri hela ipo mzee.. midaa yenye rates nzuri huwa Ni kuanzia saa 11 alfajiri mpaka saa 2 asubuhi... Ukipiga kazi huo muda mchana unaweza hata kurelax maana hata rates huwa zinashushwa (madereva wa Uber ) watakuwa wanaelewa.
Mkuu appreciate you maneno yako yapo sawa na maneno ya MDAU mmoja niliunganishwa nae ili nipate experience alisema hvyohvyo nashukuru kwaukarimu wako man umenisogeza hatua 2 mbele zaidi. Naendelea na mchakato shukran.
 
Nilikua na Uber mbili....kwahio nakushauri ninachokijua. Ukimpa dereva ni hasara ila ukitaka kupata faida nakushauri komaa mwenyewe! Kuna jamaa yangu anafanya na yeye anazungukia maeneo ya airport kule. Anapata kwa kweli si mbaya, nilimshauri afanye mwenyewe baada ya mkataba wa kazini kwake kuisha akiwa kama dereva!
 
Shukran #eli of course nitafanya mwenyewe.
 
Mkuu appreciate you maneno yako yapo sawa na maneno ya MDAU mmoja niliunganishwa nae ili nipate experience alisema hvyohvyo nashukuru kwaukarimu wako man umenisogeza hatua 2 mbele zaidi. Naendelea na mchakato shukran.
Kweli Mkuu Komaa
 
Kwakweli usiogope wala usihofu kuwekeza, kumbuka uwekezaji wowote lazima macho yote yawepo hapo, ukiifanya mwenyewe lazima faida utaiona, ukimkabizi mtu lazima hasara utaipata, nakuombea kila la kheri katika uwekezaji huo,ubarikiwe sana mkuu.
 
Ameen
 
Back
Top Bottom