Tusaidiane: Inakuwaje kuna shule Wazazi wamelipishwa ada kipindi cha Corona

Babeli

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
6,660
3,233
Habari JF,

Naomba tufahamishane kulingana na mwongozo wa Wizara ya Elimu, hakuna mzazi atakayelipishwa ada kipindi chote cha Corona ambacho watoto wamekuwa nyumbani, unless unadaiwa huko nyuma.

Ni vipi basi kuna shule zimelipisha wazazi kwa kupunguza mwezi mmoja tu tena kwenye usafiri na sio ada. Na tofauti yake iliyobaki ikagawanywa mara mbili kwa mihula miwili iliyobaki juu ya ada ya kawaida inayotakiwa kulipwa?
 
Mkuu tuendelee kulipa kutimiza wajibu wetu kama wazazi.

Mi nimelipia basi yameisha.
 
Ina maana umeridhika nayo, nataka kujua is it fair? JE ni halali?
, "Hakuna mzazi atakayelipishwa ada kipindi chote cha Corona ambacho watoto wamekuwa nyumbani" Hutalipishwaje wakati watoto walikuwa likizo, ukilipa utakuwa umeliwa kama mwanao hadaiwi usilipe.
 
Wewe mwanaccm lipa ada mtoto asome au mrudishe kwenye elimu ya Bure inayotolewa na CCM, usitupigie kelele. Siku Magufuli anafungua mkutano mkuu wa chama cha walimu alisema atawalipa walimu hata Kama hawafanyikazi na mkamshangilia sana.

Sasa unataka wapunguze ada harafu pesa ya kufidia ujinga uliofanywa na incompetent wenu watazitoa wapi?
 
, "hakuna mzazi atakayelipishwa ada kipindi chote cha Corona ambacho watoto wamekuwa nyumbani"
Hutalipishwaje wakati watoto walikuwa likizo, ukilipa utakuwa umeliwa kama mwanao hadaiwi usilipe.
Wapelekeni watoto wenu shule za bure msitupigie kelele hapa
 
Kama baba ni mzito kuelewa kiasi hicho, sijui watoto wako watakuwa na hali gani.

Katika kalenda ya mwaka ya kawaida watoto wanatakiwa kusoma kwa siku 195, baada ya janga la corona na adjustment iliyofanyika watasoma siku 185, sasa hapo unataka kupunguziwa ada ipi ?
 
  • Thanks
Reactions: Ilu
hivi wee mzee kwaiyo kama korona ilikuepo ulitaka usilipe? Je, huko shule wanakoenda watamaliza silabasi au wataziachia nusu?
hebu tutumieni akili japo kidogo
 
Wewe mwanaccm lipa ada mtoto asome au mrudishe kwenye elimu ya Bure inayotolewa na CCM,usitupigie kelele.Siku Magufuli anafungua mkutano mkuu wa chama cha walimu alisema atawalipa walimu hata Kama hawafanyikazi na mkamshangilia sana.sasa unataka wapunguze ada harafu pesa ya kufidia ujinga uliofanywa na incompetent wenu watazitoa wapi?
Sasa Jomba mazungumzo ya kawaida una leta Matusi daaa kweli Elimu ni shida kwa baadhi ya watu. .umeishia darasani la ngapi Jomba. Hii ni hoja nimeisikia inazungumzwa. Hii inahusianaje na ccm sasa.tumia akili basi walau hata hiyo kidogo uliyonayo kufikiri.
 
Kama baba ni mzito kuelewa kiasi hicho, sijui watoto wako watakuwa na hali gani

Katika kalenda ya mwaka ya kawaida watoto wanatakiwa kusoma kwa siku 195, baada ya janga la corona na adjustment iliyofanyika watasoma siku 185, sasa hapo unataka kupunguziwa ada ipi ?
Kwa bweni, chakula, malazi, maji, na umeme.
 
, "hakuna mzazi atakayelipishwa ada kipindi chote cha Corona ambacho watoto wamekuwa nyumbani"
Hutalipishwaje wakati watoto walikuwa likizo, ukilipa utakuwa umeliwa kama mwanao hadaiwi usilipe.
Nadhani Serikali imejichanganya

mwongozo unasema muhula wa kwanza utaisha mwezi wa nane so obviously ada ya muhula inabidi ikamilike

changamoto ni wale wanaorudisha watoto kwa ada ya muhula wa pili utakaoanza mwezi wa 9
 
Hapa Waziri wa Elimu Joyce kayumba sana labda atangaze interests zake amekosa msimamo thabiti na Rais pia anawajibu katika hili. Uongozi umekosa class ya uongozi ubahili na roho mbaya za kimatamshi.

Awamu hii kauli mbiu ni punda afe mzigo ufike. Implied kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe, they haven't had any recommendable intervention strategies on mass crisis since coming to power.
 
Sasa Jomba mazungumzo ya kawaida una leta Matusi. ...daaa..kweli Elimu ni shida kwa baadhi ya watu. .umeishia darasani la ngapi Jomba. .Hii ni hoja nimeisikia inazungumzwa. Hii inahusianaje na ccm sasa.tumia akili basi walau hata hiyo kidogo uliyonayo kufikiri.
Hao watu ungewaambia wapeleke watoto wao shule za Bure ili kuipa ujiko ccm siyo kutuletea huu utopolo wako hapa
 
Kwa mujibu wa hesabu za siku za Masomo zilizotolewa na waziri,mpska shule zitakapofungwa watakuwa wamefidia siku walizokaa Nyumbani hivyo ni haki kabisa kulipa ada yote.

Ikumbukwe pia waalim Walikuwa wanalipwa kipindi cha COVID, sasa unategemea shule inapata wapi hizo pesa?
 
Back
Top Bottom