Tupunguze "kuisimanga" ATCL, haijengi zaidi ya kukatisha tamaa

Mabasi ya KAMATA yaliwashinda kuendesha wataweza ndege?
Tukubali hizi ni zama za ubinafsishaji na utandawazi,
Serikali haifanyi biashara bali huwajengea wananchi mazingira mazuri ya kufanya biashara kisha hutoza kodi.
Ok. Ikifika kwa wawekezaji kama dangote mnasema MSURURU WA KODI. Kwamba asilipe kodi stahiki.

Sasa tushike lipi?
 
Hamna uwanja wa Kisonge Arusha... Ni uwanja wa ndege Arusha (Kilimo Anga) uliopo eneo la Kisongo Arusha
 
Nenda taratibu wewe, dhamira ya CCM inafaa kuongoza nchi?
mkuu hawa wapnzani wa tanzania tulishajua dhamira yao kwa nchi yetu, kwa hyo hata usisumbuke nao, NAWAAMBIA UKAWA HIVI, KWA NAMNA YA SIASA MLIYOICHAGUA HAMTOKAA KUJA KUKABIDHIWA MUIONGOZE SERIKAL YA TANZANIA HATA KWA DAWA, WATU WAMESHAJUA DHAMIRA YENU.
 
Barafu,
Masuala ya usalama wa anga inabidi yahojiwe sana na siyo masimango. Tunategeme Mamlaka ya usafiri wa anga (Tanzania Civil Aviation Authority), Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania pamoja na ATCL watupatie ripoti kamili juu ya tukio hili.

Ripoti itatupa mwangaza tatizo ni nini inaweza kuwa matatizo ya weledi wa marubani, mafunzo duni , mchoro wa kiwanja, ndege ilivyoundwa, hydraulic power za ndege, spidi kubwa, Control Tower n.k Ni muhimu ripoti itoke ili wananchi wanaotumia ndege hizi za ATCL wajue wapo katika mikono salama.

Na muhimu ripoti ya sakata hii itasaidia wadau wote wa sekta hii ya usafiri wa anga Tanzania na kimataifa yaani ndege zinazoingia anga ya Tanzania.

Tutazame video wenzetu wanavyohifadhi kumbukumbu za matukio za usafiri wa anga na taarifa kuwa wazi kwa umma kupitia media mbalimbali na wataalamu kuongelea tukio halisi lilivyokuwa na siyo '' kutumia uzalendo kuficha mambo'', uzalendo ni uwazi wa tukio Zima na sababu zake ili kupunguza uwezekano wa kutokea tena:

AIR CRASH INVESTIGATION
Air Disasters: Impossible Landing (Season 3 Episode 4)

Source: Air Disaster

Docementary ya kusikitisha hii
 
Hii ni Tabia ya Chadema na Watu mapunguani wasio na staha wala adabu, habari hii aliipost David Silinde, akafuatia Julius mtatiro kabla ya Tanza Giza kuirusha

Asante sana Barafu, Asante sana, hiki ndicho kizazi chetu bwana sasa Tunafanyaje, tulishakizaa.

Nilishangaa sana Jana, watu wanapayuka utadhani hiyo ndege ni ya Magufuli binafsi au CCM binafsi, wanadhani Pesa kukauka mitaani sababu ni nyingine....hawajui kuwa kukauka huku kwa pesa sababu ni hizo ndege, sasa Je ikiharibika halafu tena mwakani tufunge mkanda tena kama wa mwaka huu ili inunuliwe tena ndege nyingine sijui mtalia machizi gani?

Watanzania ni watu wa ajabu sana duniani, sijawahi kuona, tena ingekuwa ni amri yangu nchi hii, ningewashughulikia ipasavyo, hatutaki upumbavu wenu, kama mna stress za maisha ni ninyi huko huko, au mfe tu nyambafu sana

Watu mnaropoka mnoo wakati hamjui kitu.
 
Ndege haina "side mirror",ilimpasa kujiridhisha ili kuiweka ndege ktk sehemu salama.Lakini watu wameanza kusema na mengine ambayo hata hayapo.
Mkuu Barafu, kwanza naunga mkono hoja sio vizuri kulalamika kuhusu kila kitu, Watanzania tuna tatizo la uzalendo kwa nchi yetu, watu tuko tayari kudharau chetu na kuthamini cha mwenzio.

Hilo la side mirror, sio issue, kuna camera ambayo iko linked na GPS ambapo pale kwenye dashboard, pilot anapaswa kuona hadi zile landing lines kama baadhi ya magari ya kisasa ukirudi rivesi, kuna camera inawaka na kukuonyesha nyuma.
Paskali
 
Asante kwa maelezo mazuri mkuu, wengine wamekaa kukosoa tu
Tatizo ni upatikanaji wake unesababisha makundi makubwa kuumia' wanafunzi wanakosa mikopo elimu ya juu, hospitalin madawa hakuna, kodi zimewekwa kila kona, ajira hakuna, watumishi wa umma stahiki zao zimesitishwa! Unadhani hawa wote watafurahia uwepo wa hizo ndege?
 
Mkuu Barafu, kwanza naunga mkono hoja sio vizuri kulalamika kuhusu kila kitu, Watanzania tuna tatizo la uzalendo kwa nchi yetu, watu tuko tayari kudharau chetu na kuthamini cha mwenzio.

Hilo la side mirror, sio issue, kuna camera ambayo iko linked na GPS ambapo pale kwenye dashboard, pilot anapaswa kuona hadi zile landing lines kama baadhi ya magari ya kisasa ukirudi rivesi, kuna camera inawaka na kukuonyesha nyuma.
Paskali
Na hilo ndilo lililomfanya aone landing gears ipo out of Safety lines!!Maana kuna watu walianza kusema kwanini asichungulie nyuma?Ndio maana nikasema "kiutani" kuwa ile si bajaji kwamba ina side mirrors!!Upo sahihi mkuu...Jambo lililotokea ni la kawaida sana,na linatokea kila siku iwe ni Dsm,KIA,Jomo Kenyata au hata huko mbele;hapa tatizo ni ATCL...Na hata Kisongo ingekuwa ina-operate 24hrs,usingeisikia hii issue,maana ndege ingetoka na kusepa;Waliamua kuunganishia sbb sunset ilishafika
 
nmegundua kuwa kuna chuk kubwa kat ya baadh ya wananch na selkar ndo mana wanataman selkar hii ishndwe ktk kila jambo atakama n zur. mfano wale vjana 3000 walositishwa ajira zao, walokosa mikopo, wahtm wa vyuo wa mwaka jana ambao hawajapata ajira, watumish ambao mishaara yao na madalaja hayajapanda, wananch walobomolewa nyumba zao ukiongeza na wanasiasa ambao wamekandamizwa lazma waisimange bombada tu, japo n aibu kama taifa kwan ilitupasa tukae kmya il kulinda shrka letu
 
Na hilo ndilo lililomfanya aone landing gears ipo out of Safety lines!!Maana kuna watu walianza kusema kwanini asichungulie nyuma?Ndio maana nikasema "kiutani" kuwa ile si bajaji kwamba ina side mirrors!!Upo sahihi mkuu...Jambo lililotokea ni la kawaida sana,na linatokea kila siku iwe ni Dsm,KIA,Jomo Kenyata au hata huko mbele;hapa tatizo ni ATCL...Na hata Kisongo ingekuwa ina-operate 24hrs,usingeisikia hii issue,maana ndege ingetoka na kusepa;Waliamua kuunganishia sbb sunset ilishafika
haya ma pangaboi tatizo lake kubwa ni landing gear, ukiona mmetua mshukuru Mungu, google uone
 
Mkuu Barafu, kwanza naunga mkono hoja sio vizuri kulalamika kuhusu kila kitu, Watanzania tuna tatizo la uzalendo kwa nchi yetu, watu tuko tayari kudharau chetu na kuthamini cha mwenzio.

Hilo la side mirror, sio issue, kuna camera ambayo iko linked na GPS ambapo pale kwenye dashboard, pilot anapaswa kuona hadi zile landing lines kama baadhi ya magari ya kisasa ukirudi rivesi, kuna camera inawaka na kukuonyesha nyuma.
Paskali
Pascal Mayalla, haya wameyataka wenyewe. Ndege toka zimezinduliwa siku ile Rais aliligeuza jambo hili kuwa la kisiasa na fahari ya CCM badala ya la kitaifa unategemea nini? Lazima wanasiasa nao watumie kila nafasi ya tatizo kulitumia kisiasa.
Unajua kwa nini Yanga ikicheza na Zamalek inapowakilisha nchi kwa nini Simba inashangilia Zamalek? Ni kwa vile kama Yanga itashinda badala ya kusema tumeleta fahari ya nchi wao watasema sisi ni wakimataifa sio kama wale Simba wamchangani. Kwao kushinda ni furaha zaidi kwamba wameikomoa Simba na sio fahari ya Tanzania.
Ndivyo ilivyo sasa hivi, angalia mgogoro wa kiwanda cha Dangote.
Kiwanda kile kilikuwa kinatoa ajira kwa Watanzania bila kujali itikadi na ni maendeleo ya nchi, lakini ccm walitaka kufanya kiwanda hicho kama chao na kilitumika kama sehemu ya kampeni hivyo kushindwa na migogoro yake wapinzani wanaitumia kama kete na kuuliza kikowapi?
Ndio maana Dr Kafumu kawaambia wenzake waache tabia ya "Uzalendo uchwara" kwenye mambo ya kitaifa.
 
Dar/MBI Ni Tshs 350,000! Ha, nitaendelea kukwea fastjet.. kubana matumizi kwanza, uzalendo baadaye..
 
Yale maneno ya mpangaji wa magogoni akiutambulisha mpango wa kununua ndege hizi (bombadier) yalikuwa na bado yanaukakasi.

Huu ni mwangwi unaopaswa kumfikia mpangaji. Ajue kuwa wanaweza kuisusia idea yake kwa kukaa kimya au kuhifadhi kicheko chao kwa siku kama hii (bombadier kutua kimizengwe)

Ukiona hivi ujue kuwa hata kama kitu ni chetu (kinatokana na kodi zetu) lakini kutoka moyoni kabisa hatukipendi.

Mpangaji wa magogoni aache kuendesha meli yetu kimipasho mipasho.

Hata mzee Yusufu kaachana na taarabu!!! Pumba aige mfano huo.
 
Lazima wakosoe kwa sababu ni ndege zilizonunuliwa kwa Pesa(kodi) zao na kibaya kuna watu wamekosa mikopo ili tu ndege zinunuliwe.

Hivyo wana Uchungu nazo na kuona zile ni sehemu ya matatizo yao.

Tatizo lenu nyie mnaosifia kila mara mnazidisha Sukari.
Mawazo kama yako ni yanaweza tu kutolewa na mtu asiyejiamini kabisa na kutokujitambua.

Unadai "kuna watu wamekosa mikopo ili tu ndege zinunuliwe" hao wanaosomesha watoto wao kwenye shule binafsi kwa fedha nyingi na hata chekekea wanalipiwa ada ya mamilioni, siyo Watanzania!

Unalaumu kwamba "Hivyo wana Uchungu nazo na kuona zile ni sehemu ya matatizo yao". Hao waliokosa mikopo wanajua chanzo cha mapato ya Serikali!

TAFAKARI CHUKUA HATUS
 
Pascal Mayalla, haya wameyataka wenyewe. Ndege toka zimezinduliwa siku ile Rais aliligeuza jambo hili kuwa la kisiasa na fahari ya CCM badala ya la kitaifa unategemea nini? Lazima wanasiasa nao watumie kila nafasi ya tatizo kulitumia kisiasa.
Unajua kwa nini Yanga ikicheza na Zamalek inapowakilisha nchi kwa nini Simba inashangilia Zamalek? Ni kwa vile kama Yanga itashinda badala ya kusema tumeleta fahari ya nchi wao watasema sisi ni wakimataifa sio kama wale Simba wamchangani. Kwao kushinda ni furaha zaidi kwamba wameikomoa Simba na sio fahari ya Tanzania.
Ndivyo ilivyo sasa hivi, angalia mgogoro wa kiwanda cha Dangote.
Kiwanda kile kilikuwa kinatoa ajira kwa Watanzania bila kujali itikadi na ni maendeleo ya nchi, lakini ccm walitaka kufanya kiwanda hicho kama chao na kilitumika kama sehemu ya kampeni hivyo kushindwa na migogoro yake wapinzani wanaitumia kama kete na kuuliza kikowapi?
Ndio maana Dr Kafumu kawaambia wenzake waache tabia ya "Uzalendo uchwara" kwenye mambo ya kitaifa.
Upo sahihi mkuu Chakaza na ndio maana nikasema tatizo la ndege hizi ni "Siasa".Zimekuja wakati wa siasa za majigambo na tambo!!Huku kukiwa na siasa za kuviziana na kuparuana
 
Lets not be negative for everything including our carrier like ATC,it was the 1st trip to Arusha yesterday and the pilot made a mistake after landing on the airstrip which precision Air is landing very easy .
 
Hizi ndege hata marubani wanaziogopa!!!Maana zipo "kisiasa" sana.Kila mtu anatafuta pa kupatia "kick" linapokuja suala la ATCL.Kilichotokea Kisonge ni jambo la kawaida sana ktk usafiri wa anga.

Hapo ni suala la kawaida sana,wakati wa kutua rubani alikuwa anataka kupiga turning ili aingie Apron(sehemu ya maegesho ya ndege)kwa ajili ya kushusha abiria,lkn bahati mbaya tairi moja la nyuma likatoka nje ya runway.

Sasa kwa sbb hizi ni ndege mpya;jamaa akaona isiwe tabu,ni bora asubiri "Towing Car" ili aweze kuitoa.Angeweza kuitoa hata kwa ku-tax,lkn amechukua tahadhari ili kuepuka lawama.

Na kwa sbb uwanja wa Kisongo ni 12hrs,hufunguliwa na kufungwa wakati wa mawio(sunrise) na wakati wa machweo(sunset),kwa muda iliofika Kisongo na kutaka kuondoka ndege isingeweza sbb muda wa kufungwa uwanja ulishafika,na Kisonge haina taa za sehemu ya kutua na kurukia,kama ingalikuwapo "dear bombadia" ingerudi Dsm usiku kwa usiku.

Hali hii ipo Mtwara,Kigoma,Tabora na hata Mbeya.Ndio maana kuna safari ikitokea itilafu kidogo tu na ikafika saa kumi jioni Fastjet bado ipo Dsm haiwezi kwenda tena Mbeya.

Safety First,hiki ndicho rubani kazingatia,angeweza kulazimisha kukata kona na kuitoa,lkn alitaka kuhakikisha kuwa abiria wote wanashuka kwanza ili kupunguza uzito.Yangetokea mengine ndio watu wangelaumu sana.

Incidence za kubasti tairi,kuchepuka nje ya runway au taxway ni za kawaida sana,ni kwa sbb huwa haziripotiwi au ni kwa vile zimetokea kwa ATCL ndio maana zinashika kasi na heading mitandaoni.
Rubani kafanya maamuzi sahihi...

Na hii ni incidence ya kawaida sana ktk usafiri wa anga.Hapa juzi kati huko Nairobi ndege ilipata tatizo kwenye Runway na uwanja ukafungwa zaidi ya masaa 6,ndege zote za Jomo Kenyata zikawa diverted KIA na Dsm hadi uwanja ulipofunguliwa.

Siku kadhaa zilizopita zililetwa habari za Oman Air kupata mpasuko wa tairi huko Dsm.Waarabu wa Oman walikaa kimya huku wakiendelea na uchunguzi,hawakupiga mayowe ili wasipoteze abiria wa ndege zao ambao wamekuwa wakizitumia kufika Asia na mashariki ya mbali.Kusafrisha mahujaji nk.Walikaa kimya sbb,basti ni kitu ya kawaida,na kwao ndege ni sehemu ya utalii na kipato cha nchi.Sasa sisi kuchepuka tu kwenye taxway/runway ni maneno ya kejeli tupu.

Masaa sita ni mengi;kwanza yanaonyesha pengine nchi husika haijajiandaa kukabiliana na dharula,majanga ya moto na ajali.Lakini vyombo vya Kenya wala havikushobokea habari hii,ilipita kimyakimya sbb wanajua madhara yake.Hii si "habari" kwa maana ya ndani ya Taifa la kwao.Linawashushia heshima ya utayari ktk majanga na uokozi.Wakaipiga "pini" na kujadili mambo mengine.

Sisi Bombadia rubani kafanya tahadhari ya kuepusha majanga kwenye "landing gears" basi kila mahali usiku huu n maneno na "kuiponda" ATCL!!Ebooooo!!Tabia gani hii ya kutokilinda vya kwenu?Ndege haina "side mirror",ilimpasa kujiridhisha ili kuiweka ndege ktk sehemu salama.Lakini watu wameanza kusema na mengine ambayo hata hayapo.

Hii ni kitu ya kawaida,ndio maana kuna incidence na accident!!Ila kwa sbb ni ATCL,watu wataongea sana saanaaa.Lkn hao hao wapiga kelele ndio wa kwanza kukuomba uwafanyie booking ya ATCL.Loooh!!Pole sana ATCL...Unaonekana "yatima" hata ktk ardhi ya mama yako Tanzania.Huu sasa sio ukosoaji,ni MASIMANGO!!Kutwa kucha kuisimanga ATCL...Duuuh!!
Unafiki wa watanzania utauweza.....kujua mambo hawajui kuzusha sasa ndio kazi wanayoiweza,ndege ni za nchi wala sio za mtu mmoja huo ni ukosefu wa akili hizo siasa zenu za vijiweni msiziweke kwenye mambo ya msingi,kuwa NYUMBU kazi sana.
 
Back
Top Bottom