Tupo wawili peke yetu

Tupo wawili peke yetu

abdul39

Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
10
Reaction score
2
TUPO WAWILI PEKE YETU
Padri amekaa katika ki-box cha kuungamisha, kanisani hakuna mtu. Mara muumini mmoja akaingia, akapiga magoti upande wa pili na kufanya ishara ya msalaba akaanza kuungama.

"padri naungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana" "endelea"

"bosi wangu aliniita nyumbani kwake akaniambia amegundua nimeiba shilingi milioni 50, akasema nisipotoa maelezo ya kutosha atanipeleka polisi. Sasa ukweli mimi naogopa kufungwa, nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikachomoa bastola nikamuua. Je, Yesu atanisamehe?"

"utasamehewa" Padri alijibu

"Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa, kutazama loh, mke wa bosi. Akaniuliza nimemfanya nini mume wake. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye. Je, Yesu atanisamehe na hiyo?"

"utasamehewa" Padri alijibu

"nikatoka nje, nikawasha gari niondoke lakini mlinzi akakataa kufungua geti akasema amesikia kama kishindo hivi! Nikaona ananiwekea kiwingu.
Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Je, Yesu atanisamehe?"

"utasamehewa" Padri alijibu

"nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi nikawaza mambo gani tena. Akasema amerudi nyumbani na kukuta yaliyotokea, lakini akanionyesha diary ya baba yake inayoonesha kuwa nilikuwa na appointment naye kabla hajafa. Nikamuuliza nani mwingine anajua, akasema ameanzia kwangu kisha atakwenda polisi.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Diary nikaichoma moto. Je, Yesu atanisamehe na hilo?"

- kimya........

"padri, Yesu atanisamehe kwa hilo?"

- kimya.........

Jamaa kutazama kwenye kibox padri hayupo. Lakini kwenye kona moja akaona kabati la ngou za mapadri kama linatikisika. Kufungua akamuona padre kajificha katikati ya majoho anatetemeka.

"sasa baba mbona umenikimbia?"

padri kwa taabu akajibu

"nilitazama huku na huku nikagundua kuwa tuko wawili peke yetu........"

hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.....................................tuko wawili peke yetu loh!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom