Tupo Huru Uraiani: Mapambano Yanaendelea Rombo

Tupo Huru Uraiani: Mapambano Yanaendelea Rombo

Chademakwanza

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2014
Posts
6,346
Reaction score
1,873
Na nukuu

Wadau kwanza niwashukuru saana kwa sala na maombi yenu hapa jukwaani ambayo naamini yalisaidia saana kutuweka huru.

Mambo yalikuwa hivi, mimi kama Mkt wa chama(W) nilialikwa na Mkt Wa Kijiji cha Mbomai(TARAKEA) kuhudhuria mkutano wake mkuu wa kijiji uliofanyika jana ijumaa.

Ikumbukwe kuwa Kijiji hiki cha Mbomai ndicho chenye mji wa Tarakea ambapo Mkt Wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo ndg Tesha ni diwani wa kata ya Tarakea Motamburu yenye vijiji viwili vya Kikelelwa na Mbomai.

Kijiji cha Mbomai kina mgogoro mkubwa sana wa ofisi ulioanza tu mara baada ya CHADEMA kushinda kiti hicho cha kijiji. Chama cha Mapinduzi CCM kinadai ofisi hiyo ni mali yake huku wananchi wakidai ofisi ni mali ya kijiji kwani waliijenga wao.

Baada ya sakata hili kuendelea Mkurugenzi alimwagiza Afisa Mtendaji wa kijiji ahame ofisi hiyo mara moja na akakodishe ofisi anakojua.

Baada ya hapo Afisa Mtendaji Wa Kijiji alihama bila hata kumtaarifu Mkt wa kijiji na kuhamia kwenye ofisi ya karani wa soko.

Baada ya kuhama,Chama cha Mapinduzi CCM kilishusha bendera ya Taifa iliyokuwepo kwenye ofisi ile ya kijiji na kupandisha bendera ya CCM na kuweka makofuli pale mlangoni.

Tarehe 18/02/2015 siku ya Alhamisi Mbunge wetu alifanya mkutano pale Mbomai na kuwaongoza wananchi kuvunja makofuli yaliyowekwa mlangoni na kuweka mengine na funguo zake alikabidhiwa Mwenyekiti wa kijiji.

Bendera ya CCM ilibaki ikipepea pamoja na kibao kilichokuwa kimewekwa kwenye mbao ya paa la ofisi hiyo kilichokuwa kimeandikwa"ofisi ya CCM tawi la Mbomai" pia kilibaki. Afisa Mtendaji pia aliendelea kubaki kwenye ofisi aliyoahamia ambayo haitambuliwi na wananchi.

TUKIO LA JANA IJUMAA.

Siku ya jana ijumaa ndipo ikabidi tuwaongoze wananchi wakamilishe kazi ya kuirejesha ofisi ya kijiji katika milki yao. Katika kuhakikisha wananchi wanajimilikishia ofisi yao waliazimia na kutekeleza yafuatayo;

1.Bendera ya CCM ishushwe mara moja na zichangwe fedha za kununulia bendera ya taifa ili ipandishwe pale mbele ya ofisi.

Katika azimio hili bendera ya CCM ilishushwa na wananchi na hapo hapo wananchi walichanga jumla ya sh.50,000 kwa ajili ya kununua bendera ya taifa.

2.Afisa Mtendaji wa kijiji akabidhi funguo za ofisi aliyohamia ili vifaa vya ofisi ya wananchi virejeshwe ofisini.

Katika utekelezaji wa azimio hili ndipo Afisa Mtendaji wa kijiji alitakiwa kukabidhi funguo za ofisi aliyohamia na yeye bila hiyana alitekeleza amri hiyo.

Wananchi walichukua funguo na kwenda moja kwa moja kwenye ofisi hiyo aliyokuwa akiitumia Afisa Mtendaji wa kijiji. Wananchi walifungua ofisi na kuchukua kila kitu yaani meza, viti,kabati na mabenchi kadhaa na kuvipeleka kwenye ofisi yao ya kijiji.

SAKATA LA KUKAMATWA LILIVYOKUWA.

Wakati wananchi walipovifikisha vifaa vyao vya ofisi kwenye ofisi yao ya kijiji, tulimkuta Mkuu wa kituo cha polisi Tarakea akiwa pale kwenye ofisi ya kijiji. Baada ya kumkuta pale,alituagiza mimi,Mwenyekiti wa kijiji na Afisa Mtendaji wa kijiji tuende kituoni. Sisi tulimsihi asubiri kwanza ili tumalizie zoezi la kuwaongoza wananchi katika kupanga vifaa vile kwenye ofisi yao jambo ambalo aliridhia ingawa kwa shingo upande.

Baada ya wananchi kumaliza kupanga vifaa kwenye ofisi yao,Mwenyekiti wa kijiji alifunga ofisi ile na tuliwaaga wananchi na kuwaambia tunaelekea kituoni kuzungumza na OCS.

Wananchi walitaka kuandamana na sisi kituoni lakini tuliwasihi wasifanye hivyo kwani jambo hilo lingetafsiriwa kuwa wamevamia kituo cha polisi. Wananchi waliridhia ingawa kwa shingo pande pia.

Basis baada ya hapo tulifika ofisini kwa OCS ambapo tulizungumza kwa muda kidogo na alikuwa akitaka tumtaje mwananchi aliyeshusha bendera jambo ambalo sisi tulimjibu kuwa hatumfahamu kwani wananchi walikuwa wengi mno.

Baada ya hapo OCS alipigiwa simu na OC-CID wa Wilaya ambapo alimtaka anipe simu ili aongee na mimi. Huyu OC-CID anafahamika kwa jina la Majebele. Nilipopokea simu tulisalimiana na baada ya hapo ndipo akanitaka nimtajie jina la mtu aliyeshusha bendera ya CCM.

Katika kujibu swali lake,msimamo wangu ulikuwa ule ule kwamba bendera ilishushwa na wananchi. Majibu yangu yalionekana kumkera ambapo baada ya kutofautiana lugha alinitishia kwamba itabidi niwekwe ndani mpaka aliyeshusha bendera atakapojulikana.

Na mimi nikawa nimeudhika kwa kiasi fulani na vitisho vyake jambo ambalo nilijikuta nimebadilisha mpaka lugha ambapo nilimwambia,ninanukuu "For this I have to be very clear Mr. OC-CID. If you think you can maintain peace and harmony just by holding me in custody, fine, am ready!"

Baada ya majibu yangu hayo alikata simu na baada ta dakika kama mbili hivi alimpigia OCS simu na kumwambie kwamba tupelekwe Makao Makuu ya polisi pale Mkuu.

Baada ya hapo tuliingia kwenye gari ya polisi huku tukisindikizwa na polisi wawili ambapo tulianza safari. Lakini tulipofika ya Usseri pale kwenye kile kilima cha Mamtukuna gari ilizima na ilikataa kuwaka kabisa.

Basi ilibidi tushuke na kuanza kuisukuma sisi pamoja na wananchi wengine waliotusaidia lakini bado haikuwaka. Tuliendelea kuisukuma gari ili iwake bila mafanikio. Baada ya mateso mengi ya kujaribu kuwasha gari bila mafanikio ndipo polisi mmoja alipoghafilika na kusema " Hivi ninyi UKAWA mkishika nchi mtatukumbuka kweli angalao mtupatie gari mpya?" Na mimi nikamjibu kuwa msijali ili mradi na ninyi mshiriki katika ukombozi huu kwa nafasi zenu.

Wakati tukiwa tumeshakata tamaa huku tukiwa tumesimama tunapga tu stori ndipo polisi alisimamisha gari moja aina ya Helux Double Cabin ambapo alimwomba dereva wa gari ile atusaidie kuwasha gari yetu. Ndipo yule dereva akaingia kwenye gari na sisi tukaanza tena kuisukuma. Baada ya muda kidogo ndipo gari yetu(ya polisi) ikawaka na safari ikaendelea.

Tulipofika kituoni polisi walianza kurushiana mpira juu ya ni nani atupokee kwani aliyeagiza tuletwe haonekani. Lakini pia wakadai kuwa mbona ishu yenyewe ilitakiwa kushughulikiwa kule kule Tarakea?

Basis ndipo Afande mmoja aliyefahamika kwa jina la Omari akawaita askari wengine watatu ambapo kila askari alipangiwa mtu kumhoji. Basis wote tuliandika maelezo yetu ambapo tulimaliza majira ya saa 2.45 usiku.

Baada ya hapo polisi walisema kuwa kwa kuwa Mwenyekiti wa kijiji ndiye msemaji mkuu Wa kijiji basi itabidi yeye achukuliwe kama suspect wa kwanza hivyo nimdhamini ili Jumatatu asubuhi turejee kituoni majira ya saa 3.00 asubuhi ili kila mmoja ajue hatma yake baada ya uchunguzi wa Polisi.

Ndivyo mchezo mzima wa jana ulivyokuwa makamanda wenzangu. Lakini ieleweke tu kwamba jana ndipo tulipoufunga rasmi mgogoro wa ofisi ya kijiji cha Mbomai kama tulivyofanya juzi kule kijiji cha Mengwe Chini.

NAOMBA KUWASILISHA

MKT-CHADEMA(W)
ROMBO.
 
Chadema ni janga zaidi ya ufikiriavyo. Hapo ni kijiji tu, je wakupewa nchi itakuwaje?
 
Chadema ni janga zaidi ya ufikiriavyo. Hapo ni kijiji tu, je wakipewa nchi itakuwaje?
 
Kamanda piga moyo konde hakuna ukombozi ulionyooka kama rula,misukosuko lazima ila inchi ya ahadi tunayoipigania haipo mbali!
 
OC-CID Majebele,ilikuwa ni halali aingie mitini...Polisi wa Tz na lugha ya Malkia ni kama mbingu na ardhi...jamaa aliona kamanda akifika ataendelea Ku urgue naye kwa kimombo..kudhibitisha hakuacha taarifa yoyote kituoni asiitwe
 
Chadema ni janga zaidi ya ufikiriavyo. Hapo ni kijiji tu, je wakipewa nchi itakuwaje?

tukipewa inchi 2015,mashoga kama wewe mnaenda mahakama ya kimataifa mkasafishwe uchafu ndo mrudi kwenye inchi mpya.
 
Bravo CHADEMA. Full kukaza mpaka hao wezi magamba waombe Poo wenyewe
 
Kazi nzuri kamanda. Haki ya mtu haitolewi kwenye sahani, bali inatafutwa. Myafanyayo ni halali yenu na mtapata haki yenu, kwa wakati wake ambao ni sasa.
 
Safi sana makamanda tuko nyuma yenu hatolala mtu mpaka tufikie kilele..
 
Huu ujingaujinga wa CCM utatuletea balaa jamani manake hakika wananchi tumechoka kuonewa, ohooo..!
 
Tuko pamoja Mwenyekiti. Mimi ni wa huko Rombo, na pamoja na kwamba niko mbali, ni muhimu niandike ili mjue tunawaunga mkono.

Baadhi ya mapolisi ni wa kusikitikia sana. Wanafanya wasiyopenda kwa kushinikizwa na wezi na wanyanganyi wanaotutawala.
 
Kazi nzuri kamanda. Haki ya mtu haitolewi kwenye sahani, bali inatafutwa. Myafanyayo ni halali yenu na mtapata haki yenu, kwa wakati wake ambao ni sasa.
Ccm walishazoea vyakunyonga sasa vyakuchinja hawaviwezi
 
Back
Top Bottom