Tupeane Taarifa benki zinazosuasua ili tutoe fedha zetu kabla hazijatangazwa mfilisi

Nina mdogo wangu alikuwa na 40M anazungushwa kutoa ngoja nimstue nilikua sifahamu Hilo..
Pale ela yake haiwezi kupotea, ila aachane nayo, kuna benki watu wanapitishia mishahara tu, lakini ukiwa serious na huduma za kibenki ni lazima ujibananishe walipo watu wengimfano hai ni kama Crdb na Nmb kwa sasa hawa ndio wamba wa Tanzania, na Kimei akiondoka Nmb itakuwa ndio nambari one Tanzania.
 
Nimejibanaa we nikasave tupesa twangu 8million kwa miaka 3 afu naambiwa bank imefilisiwa napewa 1.5million nadhani nitafariki tu kwa pressure na umaskini wangu
Duh Pole sana Mkuu, hizi sheria ni vyema wangekuwa wanatupa tosome kabla hatujafungua akaunta
 
Kwa kuwa sina pesa mingi Mara nyingi siweki hela bank,naiweka barabarani au Chini,bank nabakiza ya kununua Luku tu not more than elfu 12.
Mkuu unakaa wapi inabidi niwe natembelea mitaa yako
 
Kwa wanoijua equity bank wadau, vijisenti vyetu visije vikapotea
Equity wafanyakazi wenyewe tu wakikopaga mikopo hawalipi utaona majina na picha tu vimerushwa gazetini, hivi ni vibenki uchwara vinaishi kwa kuwaongezea umaskini Watanzania kwa mikopo uchwara tu na riba kubwa.

Unapotokea mtikisiko wa kiuchumi vibenki uchwara kama hivi ni lazima vife maana vinasurvive kwa kuwakamuwa maskini, sasa maskini wakiishiwa kabisa watapata wapi pesa? ni sawa na pride kwa sasa inapumulia mipira.
 
Kaweke NMB. Huko Mkuu hatogusa. Kama vipi kaziweke BoT kabisa.

Nyie hamjui mchezo unaochezwa...kufilisi benki ndogo ndogo ambazo ndo zina afueni ya moja kwa moja kwa wananchi ni mkakati wa serikali na mabenki makubwa ili ukaweke hela zako NMB au CRDB ili uwape hati wafilisi nyumba....so huja pa kukimbilia.

Kwasasa nimetoa hela zangu zote pale NMB samora, kama milioni 82 hivi cash kwa mpigo hadi Teller akaanza kurembua kumbe mm nahamishia kwangu..nimezitandaza chini ya godoro, nikiamka asubuhi nachomoa elfu 10 yangu ya kutwa naingia mtaani
 
Kama kitu kinakuzidi upeo wa ufahamu ni vyema ukakaa kimya ili uelimishwe, unafahamu kitu kinachoitwa Gorvernment bonds?
 
Nyie hamjui mchezo unaochezwa...kufilisi benki ndogo ndogo ambazo ndo zina afueni ya moja kwa moja kwa wananchi ni mkakati wa serikali na mabenki makubwa ili ukaweke hela zako NMB au CRDB ili uwape hati wafilisi nyumba....so huja pa kukimbilia.

Kwasasa nimetoa hela zangu zote pale NMB samora, kama milioni 82 hivi cash kwa mpigo hadi Teller akaanza kurembua kumbe mm nahamishia kwangu..nimezitandaza chini ya godoro, nikiamka asubuhi nachomoa elfu 10 yangu ya kutwa naingia mtaani

:D:D:D:D
Shikamoo mchumi
Je hauoni kuwa kuweka hela ndani kunaindolea usalama wa pesa zako?
 
Back
Top Bottom