Tupeane Taarifa benki zinazosuasua ili tutoe fedha zetu kabla hazijatangazwa mfilisi

Baada ya kupata taarifa ya haya mabank kufilisiwa niliamua kufatilia.
Kiasi kinacho ongelewa kinatolewa na bima ya amana kupitia bodi ya bima ya amana.
Bima ya amana ni kiasi kilichowekwa kisheria kinacholipwa na mabenki yote nchini kuelekea bodi ya bima ya amana ili kuweza kuwafidia wateja banki inapotangazwa kufilisika...
Sasa sheria ya Bima ya amana inaeleza wazi kuwa kiasi kinacho lipwa na Bima ya amana kisizidi million na nusu.
Hivyo basi kama uliweka laki tano basi utalipwa laki tano yote na bima ya amana.
Kama uliweka million 20 utapewa million moja na nusu na kiasi kilicho baki utalipwa na bank husika baada ya kukusanywa kwa mali na madeni yote ya wateja wa bank na orodha ya madai kupitia utaratibu maalum hivyo hakuna pesa ya mtu inayopotea bank inapo filisika.....
Pia bima ya amana hii ni ya serikali hivyo ni bima tofauti na zingine ambazo bank inaweza kuwa nazo
.
Hili hata mimi nalijua. Imagine nimekuja ku-draw 30m nilipie mzigo China wanitumie BL yangu niutoe, mzigo ushatumwa utafika ndani wa siku chahe, nafika benki nakutana na hali hii! Nitapewa 1.5m hio ingine kwa taratibu za kisheria blah blah blah unafikiri nitaipata kabla ya mzigo kufika?!
 
Tujuzane benki zilizo kwenye hali mbaya ambazo serikali inaziangali kwa jicho la tatu ili tukachomoe visenti vyetu haraka

Hili swala linaumiza sana mtu umejibana miaka kadhaa halafu ghafla inatangazwa benki yako imefilisika haina mtaji...

Pamoja na kwamb ulihifadhi milioni zako kadhaa lakini unalipwa milioni moja na laki tano tu...

Huku ni kupunguziana miaka ya kuishi.

Tujuzane na njia zingine za kuhifadhi fedha.

Huu uchumi unavyowayawaya haijulikani kesho benki gani itatangazwa mfilisi.
Mkuu wiki ijayo wanafunga
CRDB
NMB
NBC
Standard chartered
Ni mambo ya 5 kila wiki
 
Hili hata mimi nalijua. Imagine nimekuja ku-draw 30m nilipie mzigo China wanitumie BL yangu niutoe, mzigo ushatumwa utafika ndani wa siku chahe, nafika benki nakutana na hali hii! Nitapewa 1.5m hio ingine kwa taratibu za kisheria blah blah blah unafikiri nitaipata kabla ya mzigo kufika?!
Sasa hii ni hoja nyingine.
Hoja ilikuwa ni hofu ya kupoteza kabisa pesa....
 
Tujuzane benki zilizo kwenye hali mbaya ambazo serikali inaziangali kwa jicho la tatu ili tukachomoe visenti vyetu haraka

Hili swala linaumiza sana mtu umejibana miaka kadhaa halafu ghafla inatangazwa benki yako imefilisika haina mtaji...

Pamoja na kwamb ulihifadhi milioni zako kadhaa lakini unalipwa milioni moja na laki tano tu...

Huku ni kupunguziana miaka ya kuishi.

Tujuzane na njia zingine za kuhifadhi fedha.

Huu uchumi unavyowayawaya haijulikani kesho benki gani itatangazwa mfilisi.

Haki za mteja bank inapo filisiwa

Benki inapokua inafilisiwa, Deposit Insurance Board (DIB) ambayo ipo kwa mujibu wa kifungu cha 36 na 37 cha Sheria Na. 5 ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, hufanya utaratibu wa kuwalipa wateja amana zao.

Members wa bodi hiyo ni Gavana wa BOT (Mwenyekiti), Makatibu Wakuu wa Hazina wa Tanzania Bara na Visiwani, na Wajumbe wengine watatu ambao huteuliwa na Waziri wa fedha ambao ni wajuzi na wabobezi k atika masuala ya kibiashara, utaalamu au taaluma na wenye tabia na mwenendo mzuri na uzoefu ktk sekta ya zinazohusiana.

Bodi hutoa malipo ya awali kwa wateja wote ambayo kiwango cha kuanzia huwa Tsh milioni moja na nusu. Hii ni kwa mujibu wa tangazo la Serikali Na. 198 la mwaka 2010.

Kwa wateja ambao kiwango cha amana zao wakati wa ufilisi ni chini ya na hakizidi tshs 1.5m hao watalipwa amana zao zote kulingana na kiasi walichokuwa wameweka.

Kwa wateja ambao kiwango cha amana zao kitakuwa kimezidi 1.5m hawa kwanza watapokea hiyo 1.5m kama malipo ya awali kisha kiasi kilichobakia watalipwa baada ya mali zote za benki kuthaminishwa na kufilisiwa.

Ni wajibu wa yeyote anayeidai benki inayofilisika kuwasilisha maombi ya madai ukiambatanisha ushahidi wa nyaraka kwa hiyo bodi.Ili fedha ziweze kulipwa kutoka kwenye "protected deposit" ya bodi ambayo vyanzo vyake vya fedha hutokana na michango ya kila mwaka kutoka kwenye hayo mabenki nk.

Ikifikia hatua ya liquidation na kuteuliwa kwa mfilisi bodi itachukua au kupokea kiwango kilichozidi kutoka kny assets za benki kilichofidiwa kwa depositors. Hii kiutaalamu tunaiita "subrogation right".

Hivyo kiwango cha 1.5m ni kiwango cha awali na sio kiwango cha mwisho,baada ya kulipwa 1.5m ,unaandika maombi ya madai ukiambatanisha nyaraka zote kwa board ambapo utalipwa pesa zako zote kupitia protected deposits.

Chanzo: Maelezo kutoka Wataalamu wa Fedha/ Uchumi

SIGNATUREReport
Like
 
Mkuu vipi crdb na Azania mwendo wao ukoje.!
Standard Charter nayo haijui saa wala dk atakapo kuja mwana wa Adam kumnyakua.....

Mm hela zangu zote nimeziingiza kwenye miradi, hela niyo baki nayo ni ya kula na kununua vocha....

Kama unajiweza kuepuka na kuweka hela beki kiasi kikubwa halafu mwisho wa siku uambiwe ukachukue milion moja na laki tano bora ukafungue a/c nje ya nchi

Bank iliyo salama ni NMB
 
Acheni kurusha watu roho!
 
Mi naona dawa yao ni moja kwanza hela zangu natia kenye simu kisha nyingine nazifunga ndani kwenye kabati
 
Hakuna atakayepoteza hela yake hata kama bank ikifilisika kuna mambo mnachanganya...
Wee jamaa shenzy kweli! Mambo ya kuja kuzungushana mjini na midocument nani anataka? Hivi ulishawahi kusumbuliwa wakati unachodai ni chako? Ulishawahi kuchomoa kitu ummalize mtu then Mungu akapitisha mbali?

Hela huwa haipotei ila pia ujue kuwa mdaiwa kama hana unatakiwa kusubiri. Mtu aje anunue, wafanye evaluation uje uanze kuambiwa ulete documents za uhakiki hujafa tu mkuu? Kwa maisha haya ndiyo umeweka tumilioni twako 20 bank then tunafungiwa lockup unasumbuka nakuhakikishia kama una roho ndogo utakufa na hela hutaifaidi! Yote hayo ya nini?
 
Mbona BOT wamesema vizuri kua utalipwa mwisho 1.5mil
Ni sawa na gari limepata ajali na wakafanya valuation na ukapewa 1.5 tu, hakuna mwingine atayekupa zaidi
 
Hili hata mimi nalijua. Imagine nimekuja ku-draw 30m nilipie mzigo China wanitumie BL yangu niutoe, mzigo ushatumwa utafika ndani wa siku chahe, nafika benki nakutana na hali hii! Nitapewa 1.5m hio ingine kwa taratibu za kisheria blah blah blah unafikiri nitaipata kabla ya mzigo kufika?!
Mkuu achana na huyo kigagula .... kama u mkubwa kidogo unakumbuka ya meridian biao? Haha pia soma kidogo sheria za mabenki ujionee.
 
Mtu ulikuwa na say million 70. Ghafla bin vuu unaambulia 1.5M na iliyobaki utapaswa kuiomba kwa barua na attachments za kutosha huku hujui utalipwa lini na kama kweli watakulipa zote. Kwa nini hakukuwa na utaratibu mzuri watu wavute zao mapema? Huu sio uungwana hata kidogo.
 
Kuna benki kadhaa ziliwahi kufungwa hapo zamani:Greenland Bank, Meridian Biao bank, Twiga etc. hakuna mtu aliyepoteza hela zake. kukosa maarifa/taarifa huleta hofu isiyo lazima. bank ni sehemu salama kutunza pesa yako.
 
Back
Top Bottom