Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,200
- 10,948
Hii ni benki ya mwanzo nchini kuendesha huduma zake kwa misingi ya sharia za kiislamu. Pia ni muendelezo wa mfumo bora wa kibenki unaofanya kazi nchi nyingi duniani.
Benki hii ilipoanza kazi nchini kulikuwa na maneno kutoka kwa baadhi ya watu lakini hatimae ikaanza shughuli zake na kuonekana kukua kwa kasi. Hata hivyo katika siku za karibu kwa mtazamo wa kimteja nimeona kuna shida zisizotatulika.
Katika pita pita yangu nimekutana na jamaa mwenye taarifa za ndani ambaye amethibitisha kuna hujuma za ndani kwa ndani zinazoendeshwa na wafanyakazi ambao kama wametumwa wafanye kazi hiyo.Kwa upande mwengine kuna benki nyengine ambazo zinakiuka sheria za BOT na kuacha ushirikiano na benki hii tena bila kukemewa.
inajulikana benki yoyote ya kiislamu duniani haiwezi kufilisika kwa njia za kawaida.Hata hivyo panapokuwa na hujuma zinazoendelea ndani kwa ndani hilo si ajabu kutokea.
Kuna tetesi kuwa wale waliopigania uanzishwaji wake na kupelekea furaha kwa jamii ya kiislamu na faida kubwa kwa wananchi kwa jumla walipoona wimbi la ufisadi na mbinu zao kuzidiwa na watu hao waliamua kukaa pembeni kuliko kuangalia kinachotokea.
Moja ya matawi muhimu ya benki ya Amana ni pale Tandamti ambapo awali wafanyabiashara wakubwa wa kiislamu walijazana kuweka fedha zao. Mara kadhaa nimekwenda nikakutana na wenzangu na mie wanaokwenda kutoa sh.10,000 za kununulia fungu la muhogo na dagaa. Inasemekana wengi wamekerwa na uzembe unaondelea wanapohitaji huduma kwenye benki hiyo.
Ushauri kama wapo wakereketwa wa benki ya Amana waliobaki katika uongozi wa juu basi wafukuze wapuuzi wote wanaotaka kutukanisha benki hiyo hasa kwenye vitengo ya teknohama na kila inapowezekana waanze kuajiri waislamu wenyewe kwanza wenye taaluma ya vitengo husika mbali mbali vya benki hiyo.
Salamu hizi zimfikie raisi Samia ili apeleke watu wake wakafuatilie mhimili huu wa uchumi iii mwaka wowote atakaondoka asije akaondoka na benki imekufa. Atabezwa kama alivyofanyiwa Kikwete aliyeondoka madarakani akiwawaacha masheikh wamerundikwa kwa makosa yasiyo na mbele wala nyuma.