Tupeane mrejesho juu ya punguzo la bei ya bia mahali ulipo

caine

JF-Expert Member
Jul 4, 2015
563
1,275
Wasalaam

Kwa watumiaji na wapenzi wa bia hakika tarehe 1 Agust ni siku tuliokua tunaisubiri kwa hamu kubwa maana matumizi yetu juu ya bidhaa hii pendwa yalikua yanatuumiza sana.

Kama kawaida yangu mdau wa hii bidhaa leo mida ya saa 8 mchana nimeingia pande zangu nikaagiza 3 baridi ikiwa ni sehemu ya kuenjoy punguzo hili maradufu la bidhaa yetu pendwa.

Mara baada ya kupata bia zangu 3 balaa likaja kwenye malipo nashangaa naletewa bill isiokuwa na punguzo lolote. Ilnibidi kuuliza lakini sikupata majibu yalioridhisha.

Naomba kuuliza kwa wadau wangu wengine mliopo humu vp huko kwenu bia zimeshuka au bado. Kama bado tatizo ni nn? Na lini hasa tutaanza kufurahia punguzo hili?

Lakini pia tunaweza tukatumia uzi huu kupeana updates ni wapi tayari wanapata punguzo hili ili tuweze kujumuika wote na kufurahia punguzo hili.

Nawasilisha....
 
Mkuu uzi huu ni maalumu kwa watumiaji na wapenzi wa bidhaa hii pendwa. Nenda kwenye uzi wa bei ya sukari utoe ushauri wako huko. Hapa ushauri wako ni irrelevant.
huo ni ushauri nimekupa siku ya kiama ukituona wenzako tunapepea kwenye uzima wa milele tuko na malaika wewe uko jehanam unachomwa moto usije ukalalamika sikukuonya...
 
Back
Top Bottom