Tupe maujanja (part 2) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tupe maujanja (part 2)

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Jaguar, Jun 18, 2011.

 1. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna barua muhimu sana ya kijeshi inatakiwa kusafirishwa toka mji A kwendja mji B.mji A kuna kituo cha mafuta chenye mafuta ya kutosha lakini barabara nzima inayounga mji A na B hakuna kituo cha mafuta njiani.Gari zilizopo mji A ni za aina moja na capacity ya tank zake za mafuta ni kwenda nusu ya safari kati ya A na B.Hizi gari haziwezi kubebana,kuvutana wala kusukumana na pia hakuna uwezekano wa kufungua tank ya gari yoyote na hakuna chombo cha ziada cha kubebea mafuta.Uwezekano pekee uliopo ni wa haya magari kupeana mafuta yakiwa yanasafiri pamoja.(HINT),Hii gari haina sehemu ya ziada ya kubeba mafuta.(SWALI):Tumia magari machache utakavyoweza ili barua ifike mji B.
   
 2. Fayoo

  Fayoo Member

  #2
  Jun 18, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani hayo magari yako mangapi
   
 3. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sikutoa idadi ya magari,assume yapo kumi(10).
   
 4. themagainst

  themagainst Member

  #4
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  sasa,mi nadhani tutumie gari aina ya starlet haili mafuta kabisaa
   
 5. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Ok ngoja nitoe mwanga. assume from town A to town B is 100km and your car fuel tank tank capacity is 50LT so I will start with 3 car ( kama mtu akichukua idea yangu ruksa kuongeza magari) magari mawili yaishie 20Km ili yaweze kurudi point A chukua LT 10 kutoka kwa kila gari (zitakazoishia 20KM, so utakuwa na LT 20 +50 za gari lingine zinakuwa 70LT zitakazokufikisha Km 70 bado 30 tu....... narudi.......
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  We endelea kutoa jibu bana!
  Leo weekend tunapumzisha vichwa
   
 7. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Toa jibu mkuu
   
 8. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Idea ni kama hiyo hapo juu ila magari sasa yanongezeka.... ukiwa na magari 6 yaite A,B,C,D,E,F Gari lako liite C, Gari a na b yaishie 20km from point A chukua lt 10 kutoka kila gari, yatabaki na 20 ya kuwayarudisha point A (kumbuka gari lako litakuwa na nafasi ya kuweka 20 lt tu as far as limetembea 20 Km) utakuwa na 50Lt gari D,E pia yaishie 20km na unatoa tena 20 Lt from D na E yaweke kwenye gari la sita (gari F) gari C na F ziendelee na safari mpaka 30 KM fro point A, take 10 LT from gari F (litabaki na Lt 30 za kurudi Point A,) weka gari C safari yako itaishi Km 80 LESS 20KM to point B.......jamani mwingine basi amalizie....I will be Back...Jaguar get ready to give another senkyuuu...teh teh teh teh..
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  unafaa kuwa waziri mkuu wa tz ww. enhee, baada ya kutumia starlet yale magar orijino tutabebea nyasi ama tufanye y status quo?
   
 10. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #10
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  hebu mwingine amalizie..... nimebakiza only 20KM barua ifike....
   
 11. Omukuru

  Omukuru JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tumia mifano yenye akili. km 100 tanki Lt50 hata kama gari yako ingekuwa inatumia lt 2 kwa km ungefika tu uendako.
   
 12. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Unasubiri nini kuweka mfano wako wenye akili?..... utajuaje kama huo mji magari yanatumia 1LT kwa 1km??
   
 13. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #13
  Jun 20, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Nitarudi baadaye kutoa jibu
   
 14. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #14
  Jun 20, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  umezingua bana
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwani hiyo barua ina ujumbe gani?
   
 16. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #16
  Jun 20, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tumia magari manne (4):jaza gari zote full tank>>Gari zitembee 25% ya umbali,tank zote zitakuwa nusu ujazo>>Gari (2) zifaulishe mafuta kwa gari zingine(2) >>Hizi gari zitajaa full tank tena,zitakwenda mpaka 50% ya safari,tank za mafuta zitakuwa nusu ujazo tena>>Gari moja ifaulishe mafuta kwenda gari nyingine>>Hii gari itajaa full tank tena na itaondoka na barua hadi mwisho wa safari(100%).
   
 17. M

  Masuke JF-Expert Member

  #17
  Jun 20, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Hizo gari zilizotoa mafuta ndo hazitakiwi kurudi au hapo ndo itakuwa mwisho wake.
   
 18. womanizer

  womanizer Senior Member

  #18
  Jun 21, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ujinga pelekeni Jukwaa la Walevi
   
 19. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Unataka zirudi?okay:kuna gari moja iko nusu ya safari na gari zingine mbili zipo robo ya safari>>Tuma gari 2 kwenda pale 1/4 safari,zitafika zikiwa nusu tank>>kila gari ifaulishe 1/4 tank kwenda zile gari mbili>>Baada ya mgao huu,gari zote nne zitakuwa na 1/4 tank na zote zitarudi hadi 1/8 ya safari>>Tuma gari zingine mbili mpaka 1/8 ya safari,zitafika zikiwa na 3/4 tank>>kila gari moja igawe 1/4 tank kwa gari mbili>>Baada ya mgao,gari zote 6 zitakuwa 1/4 tank na zitasafiri mpaka mji A.>>Imebaki gari moja pale 50% au 1/2 ya safari>>Tuma gari mbili zikiwa full tank mpaka 1/4 ya safari>>zikifika hapo zitakuwa 1/2 tank,gari moja ifaulishe mafuta yake yaliyobaki kwenda gari nyingine>>Hii gari itakuwa full tank na itakwenda mpaka 1/2 ya safari pale ilipo gari nyingine,itafika ikiwa 1/2 tank>>itafaulisha 1/4 tank kwenda ile gari nyingine na zote zitarudi mpaka 3/8 ya safari>>Tuma gari zingine mbili mpaka 1/4 ya safari,gari moja ifaulishe mafuta kwa nyingine>>Hii gari itakuwa full tank na ikifika 3/8 ya safari itabaki na 3/4 tank,itagawa 1/4 tank kwa kila gari kati ya zile mbili,baada ya mgao kila gari itakuwa na 1/4 tank na gari zote tatu zitarudi mpaka 1/4 ya safari,to be continued...
   
 20. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Pale 1/4 safari zipo gari 5>>Tuma gari 2 mpaka hapo 1/4 safari,zitafika zikiwa 1/2 tank>>kila gari itoe 1/4 tank kwa gari moja,gari 4 zitarudi mpaka 1/8 ya safari>>tuma gari mbili hadi 1/8 ya safari,zitafika zikiwa 3/4 tank>>kila gari igawe 1/4 tank kwa gari mbili,gari 6 zitakuwa na 1/4 tank na zitarudi mpaka mji A>>tumia the same procedure kwa gari zingine mbili mpaka zirudi A>>Itabaki gari 1 pale 1/4 safari,tuma gari moja ikiwa full tank mpaka pale 1/4 safari>>itafika ikiwa 1/2 tank na zitagawana 1/4 tank na zitarudi mpaka 1/8 ya safari>>Tuma gari moja mpaka hapo 1/8 ya safari,itafika ikiwa na balance 3/4 tank,gawa 1/4 tank kwa kila gari>>gari zote tatu zitakuwa na 1/4 tank na zitarudi back to A,mission accomplished!
   
Loading...