Job Richard
JF-Expert Member
- Feb 8, 2013
- 3,875
- 2,201
Ndoa ni tamu kama utachagua mwenza sahihi, pili ukumbuke hamkuzaliwa na kulelewa nyumba moja kwahiyo kila mmoja ana tabia zake, ni vyema kusomana tabia ili kuepuka mikwaruzano, KIKUBWA UPENDO, Ukiwa na upendo wa kweli kwa nyote wawili basi ni rahisi kuvumiliana, na kingine ni USIKIVU ukikosea uwe tayari kuambiwa na kusikiza na kuomba msamaha na wewe unapokosewa sema na hata kama unataka kuombwa msamaha na mume hana tabia ya kuomba msamaha mwambie mie napenda ukinikosea uniombe msamaha, kuna vitabia vidogo dogo vinakera ila ni vyema ukawa unasema kuliko kulimbikiza moyoni kwahiyo KUAMBIANA NA KUSIKIZANA NI VYEMA,
Kila mtu kujua nafasi yake na wajibu wake, yani uvumilivu uwe kwenye mambo madogo madogo na sio unamletea mwenzako mwanamke ndani halafu unasema ndoa UVUMILIVU nope. kwa uchache HII LABDA ITASAIDIA KWA WALE AMBAO HAWAJAINGIA KWENYE NDOA,
mh umeongea mama mumeo anafaidi kweli kweli ningekuwa single ningekuja kizuri haupo single nawe