Nikasababisha kifo cha mke wangu kwa sababu ya penzi la kahaba………….! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nikasababisha kifo cha mke wangu kwa sababu ya penzi la kahaba………….!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jul 24, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jul 24, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Bado inaniumiza sana moyoni, japo siku zimepita,. Mimi ni mwanaume mwenye miaka 46 hivi sasa, kazi yangu ni udereva wa malori yanayosafirisha mizigo nje ya nchi. Naomba niwasimulie habari yangu ili nanyi mpate kujifunza zaidi, ili msije mkafanya makosa niliyofanya mimi.

  Nilioa mwaka 1996 na kufanikiwa kupata mtoto wa kwanza mwaka 1998 na katika ndoa yangu na mke wangu tulikuwa tunaishi kwenye nyumba yetu tuliyojenga kwa amani na upendo. Tukiwa na mtoto wetu huyo wa kiume ambaye tulimpenda na kumpa malezi mema, Mungu alitujalia tena na ilipofika mwaka 2001 mwishoni wakati mtoto wetu wa kwanza akiwa na miaka mitatu na nusu mke wangu alipata ujauzito mwingine na ilipofika mwaka 2002 mke wangu alipokuwa akikaribia kujifungua, alikwenda kwao Turiani Morogoro.

  Baada ya mke wangu kipenzi kuondoka na mtoto wetu wa pekee kwenda kusubiri muda wa kujifungua, ndipo hapo yalipoanza matatizo ambayo yalisababishwa na mimi mwenyewe. Matatizo hayo ndiyo yaliyosababisha kifo cha mke wangu ambacho hadi leo bado kinaniumiza sana moyoni. Baada ya mke wangu kwenda kwao, nilianza uhusiano wa kimapenzi na Binti mmoja wa Kichaga, ambaye baada ya mwezi mmoja tu tangu mke wangu kuondoka nilijikuta tumezoeana na kumhamishia nyumbani kwangu kama mke halali, huku nikijua kabisa mke wangu ambaye alikwenda kujifungua huko kwao Turiani hakuwahi hata mara moja kunisaliti.

  Japokuwa nilikuwa nikiishi na mwanamke mwingine ndani, lakini nilimkumbuka kumtumia pesa za matumizi mke wangu mara kwa mara, na kumjulisha kwamba sitaweza kwenda kuwatembelea kama nilivyoahidi kwa sababu nimebanwa kazini kwangu, kumbe nilikuwa nimebanwa na mwanamke na huyo ambaye naweza kumwita shetani. Lakini kadiri siku zilivyozidi kwenda nilijikuta nikiacha kabisa kumtumia pesa mke wangu na hata barua nikawa sizijibu. Lakini mke wangu mpenzi hakijali hilo, alijua niko safarini, kwani anaelewa kazi yangu ilivyo, ya kusafiri sana.

  Baada ya miezi mitatu kupita tangu mke wangu aondoke, nililetewa taarifa za kujifungua kwake, lakini sikujali wala kutaka kujua hali ya mtoto na mama. Niliendelea kula raha na mwanamke huyo wa Kichaga ambaye nilimwona anayajua mapenzi kumbe mnafiki na alikuwa amenishika haswa. Ilipofika mienzi mitano baadae, ikiwa ni Julai 2002, mke wangu alirudi nyumbani, siku aliyorudi hakunikuta kwani nilikuwa nimekwenda kazini na alimkuta mwanamke huyo wa Kichaga ambaye alikuwa akiishi hapo nyumbani kama kwake. Mwanamke huyo alimpokea mke wangu kwa matusi na kejeli na kumtaka aondoke. Lakini mke wangu alimjibu kuwa angenisubiri nirudi ili ajue ukweli wote. Mke wangu alikaa nje akiwa na mtoto wetu mchanga hadi niliporudi usiku sana.

  Nilimkuta nje, lakini sikushtuka kwa kweli, na wala sikutaka kujali kumwona mtoto wetu mchanga. Badala yake, bila huruma nilimfukuza na watoto wetu wawili. Mke wangu hakuamini hata kidogo. Alikuwa hajawahi kuniita kwa jina langu zaidi ya honey, dear au baba fulani, lakini siku hiyo aliniita kwa jina na kuniuliza, "Hasani, kweli unanifukuza kama mbwa?"

  Nilimjibu kwa kumwambia, "nikukumbuke wewe ni nani hasa, Mungu wangu au mzazi wangu……!"
  Siyo siri, maneno yale aliyoyatamka marehemu mke wangu yananijia mara kwa mara kichwani na kunifanya niangushe chozi hadi leo hii………

  Mke wangu hakulala pale, aliondoka na watoto wake na kuomba hifadhi kwa majirani kwani tayari ilikuwa ni usiku sana, asingeweza kutoka tabata Kisukulu hadi kwa mjomba wake Kijitonyama usiku ule akiwa na watoto na mizigo. Asubuhi aliondoka na kurudi kwao Turiani. Alipofika huko kwao wazazi wake walimwambia akae atulize akili huku wao wakitafakari nini wafanye ili kutatua tatizo hilo, lakini marehemu mke wangu hakuwa na moyo wa subira kwani aliwaaga wazazi wake anaenda kupumzika chumbani. Badala ya kujipumzisha, aliamua kujiuwa na kuacha ujumbe uliosema. "Nimeamua kujiuwa ili kuikimbia aibu iliyonikuta, sikutegemea kama ningefanyiwa unyama huu na mume wangu, kwani tumetoka mbali sana."

  Nilipopata taarifa za msiba sikushtuka wala kujali. Nilijua ameamua mwenyewe basi na iwe hivyo, lakini baadhi ya marafiki zangu walinishauri niende kwenye msiba kwani haitakuwa vyema kutokwenda kwa sababu nilikuwa sijampa talaka, alikuwa bado ni mke wangu. Wakati tunajadili hilo mara simu ikapigwa. Alikuwa ni shemeji yangu akinitaka kuwahi nilikuwa nasubiriwa mimi ili wajue watazika wapi.

  Niliamua kwenda Turiani na nilipofika kwenye msiba, nilikuwa kama mgeni japokuwa wakwe zangu na shemeji zangu walinipa heshima kama mume wa marehemu. Unajua kuna wakati hiki kitu tunachoita mapenzi kinatufanya tunakuwa kama vichaa. Yaani mtu kajiuwa kwa sababu yangu, halafu naenda macho makavuuu….! Nikikumbuka jambo lile, naona aibu sana.

  Tulimaliza msiba na kujadili kuhusu watoto ambapo tulikubaliana wakae kwa bibi yao kwanza na mimi nitakapooa mke mwingine nitawachukuwa na kuwalea. Wakwe zangu walinisisitizia nisijali, kwani kifo cha mke wangu ilikuwa ni ahadi ya Mungu. Niliumia sana waliposema hivyo.

  Nilirudi Dar na mambo yangu yaliendelea kuwa mazuri. Nilifanikiwa kumfungulia hawara yangu huyo wa Kichaga maduka mawili ili ayaendeshe, moja la vyakula na jingine la vipodozi.

  Hata hivyo mambo yalibadilika, kwani baada ya miezi saba tangu kufa kwa mke wangu mpenzi, yule hawara yangu alianza kuniletea wanaume zake ndani ya nyumba yangu wakati ninapokuwa safarini kikazi. Majirani waliponieleza niliwadharau na kuwaona ni wagombanishi. Ilifikia kipindi nikawa sipati safari mara kwa mara, hivyo kila akiwaleta wanaume zake nyumbani ananidanganya kuwa ni ndugu zake na walikuwa wanalala pale pale kwangu.

  Kumbe alichokuwa anafanya, usiku anavizia nimelala, halafu ananitoroka na kwenda chumba cha wageni alipolala huyo mwanaume wake ambaye siku hiyo yumo ndani. Nasema hivyo kwa sababu walishakuja kama watano hivi na sijui kwa nini nilikuwa sishtuki kwamba, kwao ana ndugu wa kiume tu…..!

  Wahenga walisema za mwizi ni arobaini. Siku hiyo kama kawaida yake aliniacha nimelala na kutoka huku nyuma nilishtuka nikajikuta niko peke yangu. Nilidhani amekwenda chooni lakini nikaona saa zinakatika. Nilitoka hadi chooni sikukuta mtu, nikaenda sebuleni, napo sikumkuta. Nilianza kuwaza, nikijiuliza wapi amekwenda usiku kama ule, tena bila kuaga.

  Niliamua kwenda kwenye chumba cha mgeni ili nimwamshe tusaidiane kumtafuta dada yake. Lakini kabla sijagonga mlango, niliamua kuchungulia kupitia tundu la funguo kwa kuwa nilisikia miguno isiyo ya kawaida kama watu wanaofanjya mapenzi. Kwa kuwa taa ya chumba hicho ilikuwa inawaka, hivyo niliweza kuona kila kitu. Niliwaona wakiwa katikati ya mapenzi. Sikuamini macho yangu na nilihisi kama ninayeota tu.
  Niliamua kushika kitasa na mlango ulifunguka, nikaingia na kuwagutusha. Hawara yangu alianza kulia na kuniomba msamaha. Nilimsameha na kumfukuza yule kijana. Sijui nililogwa au vipi…….!

  Baada ya miezi miwili ya fumanizi kupita, nilisafiri kikazi kwenda nchini Malawi. Hapo ndipo nilipompa nafasi, mwanamke huyokufanya umaaluni wake, kwani niliporudi nilikuta nyumba imefungwa na funguo kaweka kwa jirani. Nilipoulizia niliambiwa kuwa aliondoka siku tano tu baada ya mimi kusafiri. Na aliaga kwamba nilimtumia ujumbe nikimtaka anifuate. Nilishangaa sana, lakini niliondoka kwa jirani yule aliyenipa taarifa nikijua nitakuta ujumbe ndani kama kuna tatizo.

  Niliingia ndani na kuangaza huku na kule bila kuona ujumbe wowote. Nilianza kukagua vitu vya ndani nikakuta kachukua vitu vyangu vingi vya thamani na pesa zote kachukua. Redio kubwa ya cd tatu pia kachukua pamoja na vito vya dhahabu ambavyo vilikuwa ni vya marehemu mke wangu. Nilibaini pia kwamba alikuwa kafilisi maduka yangu yote mawili. Nina uhakika kama angeiona hati ya nyumba, angaiuza pia.

  Toka siku hiyo huwa maneno ya marehemu mke wangu yananijia kichwani. Ni yale maneno aliyoyasema siku ile usiku wakati namfukuza kama mbwa. Mpaka leo najutia kitendo changu hicho na ninahisi mimi ndiye niliyemuua mke wangu. Nilimuua bila kukusudia…………………….
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Kweli, ukamuua?
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Hapa hastahili hata huruma kabisa
  Kwani hakuwa na macho kuona kuwa anaibiwa
  We unaletewa wageni wanaume mpaka kwako hujashtuka tuu
   
 4. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #4
  Jul 24, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Majuto ni mjukuu!
   
 5. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wanaume wote mliokwisha kuoa mtubu dhambi zetu za kutoka nje ya ndoa kama ulitoka salama na ukarudi kwa mkeo inakupasa umshukuru mungu..kama bado haujarudi rudi leo

  Wanawake wengine ni kama mashetani..unapoteza memory yote.
   
 6. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  oooh inatia simanzi sana
   
 7. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  good plot.... but ni vizuri kuweka angalizo tangu mwanzo kama ni kisa cha kweli au ni tamthiliya
   
 8. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wewe mbona matatizo ujapat ngoja uone njinsi gania atakavyokutokea kama jini kabuka ndio utajua kama marage mboga au futali babu jinga wewe
   
 9. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,984
  Likes Received: 1,900
  Trophy Points: 280
  na hyo ndo faida ya kutoka nje ya ndoa. wala sikuonei huruma hata kidogo. kwanza lait wanaume mngejua hzo nyumba ndogo zinavyowaloga yaani mngeziepuka. nilikuwa naskiliza ushuhuda hapa ATN mtu anaambiwa afiche nyama kwenye utupu wake kisha baada ya siku 7 za wk ndipo aipike kwenye mboga halafu mume ale hiyo mboga lol!.

  huyu alikuwa anamfanyia buzi ambalo alikuwa anatembea nalo na alifanikiwa kumteka huyu baba kisha baba akasahu familia kabisa kiasi kwamba mkewe na mtoto wake wa mwisho walikufa pasi hata baba kujua wamekufa kwasababu gani. na yeye baba alaikwenda kuchukliwa nyumbani kwa huyu kahaba kuja kutoa idhini mkewe azikwe fikiria kweli hii ni akili?

  namshukuru sana Mungu kamtokea huyu dada na kaenda kanisani kutubu lakini wababa kweli mnaboa sana.
   
 10. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #10
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,931
  Likes Received: 955
  Trophy Points: 280
  Sad story
   
 11. f

  fidelis zul zorander JF-Expert Member

  #11
  Jul 24, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 679
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  story ndefu sana hiyo...ifanye iwe fupi nitaisoma..
   
 12. Signora

  Signora Member

  #12
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 20, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Can't believe this!!!!
   
 13. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #13
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  So sad! Imeniuma sana ngoja nilale maumivu yapungue
   
 14. L

  Loloo JF-Expert Member

  #14
  Jul 24, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Aisee nenda kwnye kaburi lake uombe radhi roho huwa zinawasiliana.watunze watoto wape mapenzi yote kama vile mama yao angewapa
   
 15. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #15
  Jul 24, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  malipo hapa hapa duniani...inaweza kuchukua hata miaka, lakini malipo yapo kabisa!!

  khaah, alivyomjibu mkewe ''nikukumbuke wewe ni nani hasa, Mungu wangu au mzazi wangu''
   
 16. r

  roy allan Member

  #16
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole baba kutereza c kuhanguka jipange upya mzee utatoka tu.
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Jul 24, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  cartura ni kisa cha kweli wala sio tamthiliya........... Mimi huw anaandika visa vya kweli daima.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #18
  Jul 24, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hawa watu wakukutana nao ukubwani waacheni tu jamani wengine hujaribu kufuta matongotongo kama vile hakuoni we unafukuzwa, nakwambia Mtambuzi kiuna dada mja ni kichaa hapo keri ukipata story yake chozi lakutoka weye hawa mahawara ningeomba mwenye naye aachane naye nduguzangu,nilishuudia mtu ameuwa mke na watoto wawili ili aanze afresh na hawara du
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. j

  jeneneke JF-Expert Member

  #19
  Jul 24, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 760
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Da so sad yaani God forbid.na ugender wangu wote namlaumu mwanamke wa kichaga.na watu wa humu "Asiye na dhambi awe basi wa kwanza kumpiga mawe"?hivi ingekuwa kunawekwa kipimo cha dhambi ikifikia level fulani mtu kapitiliza inaonyweshwa live kwenye pojector katika nchi yako nyie mliomsakama hapo juu mngebaki?kusengenya tu ni dhambi kama kuua vile,halafu mwenzenu mnakamia haya!
   
 20. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #20
  Jul 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  akome...........
   
Loading...