Tuongelee Saving yenye mafanikio

kitu bora hapa hata kama majukumu yamezidi, huwa nasema hata kama unapata lets say 700,000 per month, ishi kama mtu anaepata laki 4, matumizi yaendane na lak 4, ona kama laki 4 ndo unayopata, panga bajeti zako zote kulingana na laki4, laki 3 fanya saving. inawezekana. Huwa nasema kama kuna watu wanapata laki2 au 3 wanaish why usifanye kama unapata lak 4 na ukaish nayo na 3 ukafanya saving?
nataka niijaribu hii kuanzia july
 
Uko vizuri mkuu...me be4 sina family nilikuwa nasave 90%...ila baada ya kuwa na family now 70%.
Nikiwa namalizia miezi ya mwisho mwisho kuwa hapa JF tuongelee Saving.

Binafsi nina performance atleast kwenye Saving tangu pale nilopoweza kufanya-saving ya 800,000 Tzs kutoka katika 1M ambayo ni pesa ya ma-Boom mawili ya chuo ya miezi minne, kwahiyo kila mwezi nilitumia 50,000 Tzs only.

Falsafa yangu kwenye Saving 1)Haijarishi kipato changu napata kihasi gani ila hicho kipato nikiwa napata katika mfumo wowote wa kuingiza kipato Continuous kwamaana ya (kila siku/week/mwezi nk) nk lazima nifanye Saving, hata nikiwa napata 100,000 kwa mwezi nita-save.

2) Nikiwa nafanya Saving kitu pekee kinachokuwa cha lazima kutoa pesa ni chakula tu then ndio naangalia mengine je hiki na hiki muhimu wa kutoa pesa.

Saving kufanikiwa kwa kwa 90% kwanza kuwe na kitu kinacho ku-motivate kufanya Saving i.e kupata Mtaji, Pesa ya ujenzi nk...bila ya kuwa na target Saving inakuwa ngumu sana.

Kwa kijana kuna vitu vinavyoweza kukwamisha Savingi yake kuyumba/kutokuwa na mafanikio makubwa ukitoa sababu zingine ndogondogo, sababu moja wapo majukumu ya lazima, majukumu yamejigawanya katika maeneo mawili

1) Ya kuzaliwa nayo; haya ni kutegemewa na wazazi kila mtu akizaliwa yanamuhusu, haya hayaepukiki ila unaweza kuji-balance kidogo kuwawezesha wazazi kutegemeana na nature ya hao wazazi maana kuna wazazi chokambaya kabisa kuna wenye unafuu, sio unatoa tu maana pesa haimtoshi mtu.

2) Majukumu ya kujitakia; haya ni pale unapoamua kuoa, kuzaa au vyote kwa pamoja, kuoa hali ya kua uja-stable kiuchumi hata kwa 10% ni moja ya Bad Plan au kosa kubwa la kiuchumi unaloweza kufanya maishani, stablelize japo 5% maisha yako fanya Saving wekeza then ndio oa pale unapokuwa na source hata 2 za kipato kwamaana sehemu moja ya kuhudumia familia yengine yakufanya Saving ila ukianza kujipa majukumu hata iyo Saving ndogo itakuwa shida na ukiiweza hata 50% jua ungekuwa Single ungeiweza kwa 100%.

There is no Business you can start in this world without funding and Saving is best way of fundraising for your Business.

My Take:
Inaweza kuwa vizuri mtu mmoja akaanzisha Group la Saving yenye malengo maana Saving imekuwa changamoto kwa watu wengi.
 
Nakupa njia mbili za saving...hizo ukizishindwa wallah umaskini unaupenda


1: Vodacom mpawa Akiba:hii unaweka hela huku unaji funga kua ile hela utatoa baada ya either miezi 3,6 au mwaka...na si kabla ya hapo .hii ni Kama fixed account pia. Na utapewa gawio kidogo kutokana na ulivoweka Akiba yako.
2:Ukatili style: hii niliichukua kwa watani zangu wachaga...unachomelea boksi la chuma na unaeka lock za mageti ..na kitundu kidogo Cha kuwekea hela....halafu tuseme labda we unakaa dodoma..funguo unampa ndugu yako wa Kilimanjaro uko au dar ...kwahyo we unakua unaeka hela uku Cha kufungulia huna. Baada ya mwaka mkikutana ndo anakupa funguo...unatoa mzigo....hii staili ni ya kibabe
Heheee..ukatiri style.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom