Tuongee Leo Asubuhi Star Tv ni aibu

Tuongee Leo Asubuhi Star Tv ni aibu

Pascal Mayala kachambua mada vizuri sana, tuache siasa. Brother Mayala usikatishwe tamaa na hao, ukialikwa na Star tv kwenye hicho kipindi nenda kifua mbele usaidie kutuelimisha watanzania, uko vizuri aisee maana kutoa ufafanuzi in public tena live kwenye Tv au Radio sio mchezo ni wachache wanaweza. Hata huyo anayekukandya akiitwa kutoa ufafanuzi pale atachemsha ile mbaya.
 
Wakuu kauli ya mwisho maana yake nini? Haipingwi au....? Au ni lazima itekelezwe ikishatolewa? Na kama haipingwi haipingwi na nani? Waliochini yake kiserekali au wananchi wote? Tusije tukawa tuna ongelea vitu tofauti. Tukumbuke kuna mahakama na bunge hata kama mkulu amesema yeye ndiye mtafutaji na mgawa mafungu.
Mkuu Masiya, kwa kawaida nchi zote duniani zinatawaliwa na mihimili mitatu ya
1.Serikali, (The Executive), kazi yake ni kutawala nchi, kutekeleza maamuzi ya Bunge na Mahakama.
2.Bunge (The Legislature),Kazi yake ni kutunga sheria zitakazotafsiriwa na Mahakama na kutekelezwa na Serikali. Bunge pia linaisimamia Serikali.
3.Mahakama(The Judiciary),kazi yake ni kutafsiri sheria zilizotungwa na Bunge na kutekelezwa na Serikali.

Kinadharia, mihimili hii mitatu inatakiwa kufanya kazi kwa uhuru bila kuingiliwa (Independence) na wakati huo huo kila mhimili ni mwangalizi wa mhimili mwingine usivuke mipaka ya mamlaka yake (checks &balance). Hii inaitwa "The Principles of Separation of Powers, Checks and Balance".

Wakuu wa mihimili hii, Rais, Spika na Jaji Mkuu, wanatakiwa kuwa huru na kutokuingiliwa. Na hata ikitokea rais wa nchi hayupo tena kwa sababu yoyote ile(Kifo, Kujiuzulu, Kufukuzwa, Ugonjwa, Incapacitation, insane, etc), yoyote kati ya wawili hao atashika urais hadi uchaguzi mwingine.

Lakini rais wa Tanzania ni Executive President, ambaye huteua Mkuu wa Mhimili wa Mahakama, ambaye ni Jaji Mkuu. Rais wa Tanzania ni sehemu ya Bunge, huteua mtendaji Mkuu wa Bunge ambaye ni Katibu wa Bunge, huliunda Bunge, hulivunja Bunge na huweza kulivunja Bunge wakati wowote akiamua.

Rais wa Tanzania ni sehemu ya Bunge kwa sheria zinazotungwa na Bunge, haziwi sheria mpaka rais atakapo ridhia (acent).

Rais wa Tanzania ni sehemu ya Mahakama, sio tuu kwa kuteua watendaji wakuu wa mahakama, majaji, bali rais kupitia mamlaka ya DPP, anaweza kuingilia kesi yoyote, ikiwa katika hatua yoyote na kuamua kuifuta (Nolle Proseque), hukumu ya kifo haitekelezwi bila rais kuridhia na ana mamlaka ya kusemehe wafungwa waliohumiwa vifungo.

Hivyo rais wa Tanzania ndio kila kitu, anatunga sheria, anatafsiri sheria na kutekeleza sheria hivyo kauli ya rais ni sheria. Ila sio kila anachosema rais ni sheria, bali kile rais anachosema na kisha kikaandikwa rasmi kuwa ni sheria na kutangazwa kwa waraka wa kiserekali, GN na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali.

Rais akitangaza jambo fulani, kusipotolewa taarifa rasmi ya jambo hilo kupitia decree, jambo hilo linakuwa sio sheria.

Katazo la rais kuzitaka taasisi za umma kuweka fedha za makusanyo BOT, sio sheria na fedha zinazohifadhiwa BOT ni fedha za mapato tuu. Fedha za matumizi bado zinawekwa kwenye mabenki binafsi.

Paskali.
 
Pascal Mayala kachambua mada vizuri sana, tuache siasa. Brother Mayala usikatishwe tamaa na hao, ukialikwa na Star tv kwenye hicho kipindi nenda kifua mbele usaidie kutuelimisha watanzania, uko vizuri aisee maana kutoa ufafanuzi in public tena live kwenye Tv au Radio sio mchezo ni wachache wanaweza. Hata huyo anayekukandya akiitwa kutoa ufafanuzi pale atachemsha ile mbaya.
Mkuu Namujele Mukama, Asante.

Paskali.
 
Alijisemea Nyerere kuwa kwa Katiba yetu hii akitokea Nanihii...... Na sasa nadhani ametokea kweli.
 
Mkuu Masiya, kwa kawaida nchi zote duniani zinatawaliwa na mihimili mitatu ya
1.Serikali, (The Executive), kazi yake ni kutawala nchi, kutekeleza maamuzi ya Bunge na Mahakama.
2.Bunge (The Legislature),Kazi yake ni kutunga sheria zitakazotafsiriwa na Mahakama na kutekelezwa na Serikali. Bunge pia linaisimamia Serikali.
3.Mahakama(The Judiciary),kazi yake ni kutafsiri sheria zilizotungwa na Bunge na kutekelezwa na Serikali.

Kinadharia, mihimili hii mitatu inatakiwa kufanya kazi kwa uhuru bila kuingiliwa (Independence) na wakati huo huo kila mhimili ni mwangalizi wa mhimili mwingine usivuke mipaka ya mamlaka yake (checks &balance). Hii inaitwa "The Principles of Separation of Powers, Checks and Balance".

Wakuu wa mihimili hii, Rais, Spika na Jaji Mkuu, wanatakiwa kuwa huru na kutokuingiliwa. Na hata ikitokea rais wa nchi hayupo tena kwa sababu yoyote ile(Kifo, Kujiuzulu, Kufukuzwa, Ugonjwa, Incapacitation, insane, etc), yoyote kati ya wawili hao atashika urais hadi uchaguzi mwingine.

Lakini rais wa Tanzania ni Executive President, ambaye huteua Mkuu wa Mhimili wa Mahakama, ambaye ni Jaji Mkuu. Rais wa Tanzania ni sehemu ya Bunge, huteua mtendaji Mkuu wa Bunge ambaye ni Katibu wa Bunge, huliunda Bunge, hulivunja Bunge na huweza kulivunja Bunge wakati wowote akiamua.

Rais wa Tanzania ni sehemu ya Bunge kwa sheria zinazotungwa na Bunge, haziwi sheria mpaka rais atakapo ridhia (acent).

Rais wa Tanzania ni sehemu ya Mahakama, sio tuu kwa kuteua watendaji wakuu wa mahakama, majaji, bali rais kupitia mamlaka ya DPP, anaweza kuingilia kesi yoyote, ikiwa katika hatua yoyote na kuamua kuifuta (Nolle Proseque), hukumu ya kifo haitekelezwi bila rais kuridhia na ana mamlaka ya kusemehe wafungwa waliohumiwa vifungo.

Hivyo rais wa Tanzania ndio kila kitu, anatunga sheria, anatafsiri sheria na kutekeleza sheria hivyo kauli ya rais ni sheria. Ila sio kila anachosema rais ni sheria, bali kile rais anachosema na kisha kikaandikwa rasmi kuwa ni sheria na kutangazwa kwa waraka wa kiserekali, GN na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali.

Rais akitangaza jambo fulani, kusipotolewa taarifa rasmi ya jambo hilo kupitia decree, jambo hilo linakuwa sio sheria.

Katazo la rais kuzitaka taasisi za umma kuweka fedha za makusanyo BOT, sio sheria na fedha zinazohifadhiwa BOT ni fedha za mapato tuu. Fedha za matumizi bado zinawekwa kwenye mabenki binafsi.

Paskali.
Shukrani Mkuu, inaelekea tuna katiba/sheria mbovu kwenye separation of powers niaminivyo ni kuwa walitakiwa wakisha chaguliwa wawe na security of tenure na wasiingiliwe kabisa na raisi. Waweze kutoa maamuzi ambayo yanaweza kuiwajibisha serikali. Raisi akitoa tamko au uamuzi ukienda kinyume na sheria/katiba mihimili hii miwili iweze kuchukua hatua kurekebisha-andiko lako linaonyesha vinginevyo ndio maana umeandika raisi ni kila kitu. Kwa sasa naona usemavyo ni kweli lakini basi katiba yetu haikidhi the fundamental principle ya separation of powers.
Kumpa uwezo raisi kuingilia kesi yeyote (kama ni kweli)-hili ni janga la taifa na demokrasia. Au ndiyo haya tunayo ona Arusha na kwingineko. Labda ndio maana nchi nyingine wana independent prosecutors wanaochaguliwa na kuvalia njuga maswala nyeti na kuyaweka mbali na serikali (ingawapo gharama ni za serikal).
Ningependa neno la mwisho liwe lile linaloelekezwa na sheria-yaani matamko au maamuzi ya RAISI kama hayakidhi vigezo vya sheria yaweze kumulikwa mahakamani/bungeni na hata taasisi zisizo za kiserekali. Ndani ya serikali kunatakiwa kuwe na option ya voice na ile ya exit kama mtu hakubaliani na tamko au uamuzi wa mkulu.
Lingine ni kuwa maadili na weledi wa wale ndugu zetu wa NGOME kimsingi na kimantiki yanatakiwa yawe tofauti na sisi tuliopo nje ya NGOME. Nnje ya NGOME kuhoji au kukosoa ni kitu muhimu na hakuna anaetakiwa kuwa juu ya sheria.
 
Ndugu wana JF kama mtafuatilia yanayoongelewa leo kwenye STV tuongee Asubuhi ni haibu hasa pale muandishi anaposisitiza kwamba kauli ya rais ndio ya mwisho hata kama haina ukweli,hivyo kusitokee na mtu yeyote kuhoji.

kwa maana hiyo tuamini pamoja na yote aliyosema rais tukubali kuzaa sana,tukubali fedha zimefichwa kwenye magodoro n.k hii ni haibu kubwa kwa wana habari
Atakua ni mmoja wa waandishi wanaotakiwa kupunguzwa kazini ndio maana anamalizia machungu yake hapo
 
Back
Top Bottom