Wildlifer
JF-Expert Member
- May 12, 2021
- 1,883
- 5,270
Niko sehemu, napata chai ya Tangawizi.
Wamekuja watu wawili, wakakaa meza ya Jirani yangu [kwa muonekano ni wapenzi], kiumri ni 20s. Sababu walikuwa mbele yangu, nilikuwa nikitazama yanayojiri. Jambo moja nililojifunza, watu wapo pamoja kimwili lakini kifikra hawapo pamoja. Kila mmoja yuko eneo lake. Wanakua pamoja kwa dakika 2, dakika 2 zingine wanahama. Wamekaa kama Nusu saa kisha wakaondoka.
Imenifikirisha na kuona jinsi gani ukaribu wa mapenzi kwa sasa unakabiliwa na tatizo kubwa sana. Smartphone! Hili dude linawaondolea watu kitu muhimu sana. Attention! Kabla hili dubuwasha halijaja, ukikaa na mwanamke, kwa muda wa nusu saa, unakuwa umejua mambo yote yanayomsibu, unajua kwenye shingo amechubuka, unajua kwenye mkono ameungua, unajua kiuno kimeongezeka, unajua hata kipele kwenye ulimi. Kwa sasa si ajabu, vijana kukaa na mwanamke na kuondoka bila hata kujua harufu ya perfume yake ikoje.
Ukiwa na mtoko na mtoto mzuri, basi jitahidi smartphone uiache nyumbani [so distractive], uwe na kitochi. Itakuongezea ukaribu sana na mtoto mzuri. Attention kwa mtoto mzuri ni jambo la muhimu sana. Inasikitisha zaidi unapoona mwanaume, ndio yuko busy na simu.
View attachment 2030688