Tuongee Kiume: Mahari ni mabaki ya utumwa yaliyopewa jina zuri

Miiko ya ndoa mnaijua nyie vijana wa hiki kizazi?
Inajulikana, kwenye kuifuata hapo ndio swali ambalo ukiniuliza nitakuambia wengi wetu 'hapana'
Na ili mjuane, si lazima wote mkubali kuivunja?
Sasa vip Mwanamke/Msichana akiamua kuifuata na serious ukawa unauhitaji na ndoa nae?
 
Moja ya vitu vinavyonikwaza linapokuja suala la ndoa ni mahari. Ni kama nywele za kichwa, zipo hapo siku zote lakini zipo kwa ajili ya kazi gani hujui.

Mahari ipo miaka nenda rudi kama mila au desturi, huku idadi kubwa ya watu wanaoitekeleza wakiitafsiri kama pesa au kitu ambacho hutolewa na mwanaume kama malipo kwa familia ya mwanamke pindi anapotaka kumuoa.

Lakini kimantiki, vitu pekee vinavyolipiwa chini ya jua ni bidhaa na huduma. Tunalipia sabuni ya kuogea na dawa za meno dukani, tunalipia mafuta ya kupikia na sukari kwa mangi hizo ni bidhaa.

Wakati tukienda hospitali tunalipia matibabu, kwenye basi tunalipia nauli, huku Tanzania na Algeria zikicheza kwenye Afcon tunalipia ili kuingia uwanjani kutazama mechi, hizo ni huduma.

Sasa tukirudi kwenye mahari, kwa nini tunailipa familia ya mwanamke ili kumuoa binti yao? Je, ni kwa sababu mwanamke ni bidhaa au ni huduma? Kama sio ni kwa nini tunalipa ili kuoa?

Kuna baadhi ya watu wanajenga hoja kwa kusema kuwa unalipa kama zawadi kwa familia ya mwanamke kwa kumtunza binti kipindi chote hicho sawa ni kitu kizuri, lakini kwa upande wa pili, hata mwanaume ana wazazi, alitunzwa kipindi chote na familia yake, itakuwaje kama familia ya mwanamke nayo ikitoa zawadi ya pesa nyingi au ng’ombe kwa familia ya mume, haitapendeza?

Lengo hapa si kwamba na wanaume pia wawe wanatolewa mahari, lengo ni kujaribu kuona mahari ipo hapo siku zote kwa ajili gani?

Kama ipo kwa sababu zisizokuwa na msingi, kwa nini iendelee kuwepo? Yaani kwa nini tusiitoe kama ina sababu zisizoeleweka. Au kama tunaipenda sana, basi familia ya mwanaume itoe kwa mwanamke na familia ya mwanamke ifanye kinyume chake, itoe kwa mwanaume pia.

Kuna watu watabeza tunachokizungumza hapa, kwamba wanaume siku hizi wamekuaje? Wanadai kulipiwa mahari pia.

Lakini kama watatokea watakaobeza hivyo, wajiulize kwa nini wanabeza mwanaume kulipiwa mahari, watagundua kuwa kumbe hii kitu mahari ina kawaida ya kumshusha mtu anayelipiwa, anaonekana mdogo, anaonekana hana nguvu, anaonekana hajiwezi, anaonekana ni bidhaa, anaonekana ni mtoa huduma tu jambo ambalo kiukweli halistahili kuwemo ndani ya ndoa.

Kwa mtazamo wangu, mahari kwenye ndoa ni kama kipande cha utumwa kilichobaki, na kikapewa jina lingine zuri zuri ili kuufanya utumwa kuwa halali.

Natamani siku moja nione wanaharakati wanaotetea haki za wanawake, waamke na hii ya kupinga mahari kwa mwanamke pindi anapoolewa kwa sababu inamshusha thamani mwanamke.
Wapendao vya bure ni wengi sana hasa vijana.
 
Inajulikana, kwenye kuifuata hapo ndio swali ambalo ukiniuliza nitakuambia wengi wetu 'hapana'
Na ili mjuane, si lazima wote mkubali kuivunja?
Sasa vip Mwanamke/Msichana akiamua kuifuata na serious ukawa unauhitaji na ndoa nae?
Mwanamke mwenye misimamo hiyo huwezi kukuta mileage zinasoma nyingi kiasi hicho, labda tu awe ameumbwa namna hiyo
 
Wahenga walikaa na kulijadili hili jambo kwa undani sana hadi kufikia uamuzi kuwa; Mwanamume atoe "Mahari" ambayo mimi naiita "Fidia" kwa ajili ya mwanamke unayetaka kumuoa kwa sababu kadhaa ila kuu ni:

Malipo kwa kumfidia pale kwao anapotoka. Unampewa moja kwa moja, unaenda naye kusikojulikana kabisa na yeye anakufuata kwako. Kule kwako kuna wazazi wawili kama wale aliowaacha kwao na sasa ameamua kuja ongezewa kwenu. Familia moja inapoteza mtu au inapungukiwa mtu na familia nyingine inaongezewa mtu. Hapo huoni faida ya kulipa mahari?? Sema usemavyo ila inaitwa; Kulipa mahari. Unapotumia neno "Lipa" maanake; Umenunua kitu, sasa lipa uchukue.

Kwa kuwa ni, "Mtu" tunaogopa kusema; "Nimenunua". Kutokusema hivyo hakumaanishi kuwa hujanunua. Usingelisema; Nilimlipia mahari. Kama ulilipa mahari, ulimnunua. Lakini, sitaki kumwambia mke wangu maneno hayo ila kiukweli nilimnunua kutoka kwao kwa bei ya maridhiano mazuri tu.

Wanawake msinichukie ila ndo hivyo. Kule kwetu Tarime; Huruhusiwi kusema kuwa; Nitareta shilingi 4 milioni na ng'ombe 100 kama mahari yangu kwa binti yenu. Wale wamura walioko hapo watakuua ufe fwiii. Kwetu ni matusi kutanguliza pesa mbere harafu ng'ombe nyuma.

Tupo tiyari kusikia; Nitatoa ng'ombe 2 na shs 4milion. Tutakusikilisa na tutaanza kusumacha. Si vinginevyo.
Hayo yote ni yale yale. Tunamnunua mke.
Umedadavua vizuri sana muhenga
 
Mwanamke mwenye misimamo hiyo huwezi kukuta mileage zinasoma nyingi kiasi hicho, labda tu awe ameumbwa namna hiyo
Hapo ndio, endapo kweli ni msimamo wa kweli...
Vip kama ni kuficha kujulikana ya kua katembea Km nying katika kivuli cha Maadili?
 
iliwekwa ili kumfurahisha mwanamke nae ajisikie kwani hapo kabla walikuwa wakibebwa so walijisikia vibaya
 
Wahenga walikaa na kulijadili hili jambo kwa undani sana hadi kufikia uamuzi kuwa; Mwanamume atoe "Mahari" ambayo mimi naiita "Fidia" kwa ajili ya mwanamke unayetaka kumuoa kwa sababu kadhaa ila kuu ni:

Malipo kwa kumfidia pale kwao anapotoka. Unampewa moja kwa moja, unaenda naye kusikojulikana kabisa na yeye anakufuata kwako. Kule kwako kuna wazazi wawili kama wale aliowaacha kwao na sasa ameamua kuja ongezewa kwenu. Familia moja inapoteza mtu au inapungukiwa mtu na familia nyingine inaongezewa mtu. Hapo huoni faida ya kulipa mahari?? Sema usemavyo ila inaitwa; Kulipa mahari. Unapotumia neno "Lipa" maanake; Umenunua kitu, sasa lipa uchukue.

Kwa kuwa ni, "Mtu" tunaogopa kusema; "Nimenunua". Kutokusema hivyo hakumaanishi kuwa hujanunua. Usingelisema; Nilimlipia mahari. Kama ulilipa mahari, ulimnunua. Lakini, sitaki kumwambia mke wangu maneno hayo ila kiukweli nilimnunua kutoka kwao kwa bei ya maridhiano mazuri tu.

Wanawake msinichukie ila ndo hivyo. Kule kwetu Tarime; Huruhusiwi kusema kuwa; Nitareta shilingi 4 milioni na ng'ombe 100 kama mahari yangu kwa binti yenu. Wale wamura walioko hapo watakuua ufe fwiii. Kwetu ni matusi kutanguliza pesa mbere harafu ng'ombe nyuma.

Tupo tiyari kusikia; Nitatoa ng'ombe 2 na shs 4milion. Tutakusikilisa na tutaanza kusumacha. Si vinginevyo.
Hayo yote ni yale yale. Tunamnunua mke.
Kwa wale wenyw imani katika biblia nadhani kuna sehemu wameambiwa kijana atatoka kwao na binti atatoka kwao na wawili hawa wataungana na kuwa mwili mmoja. Sasa huyo mtu kaomgezwaje kwenye familia hapo au ni tamaduni zetu tunajiongezea mtu wenyewe
 
India wanaume ndiyo wanaotolewa mahari, sijui hilo nalo utalizungumzia aje...

Mengine yaache kama yalivyo, wewe nenda katoe hiyo mahari...

Cc: mahondaw
 
We ni me au ni ke?? Tuanze na hilo kwanza. Pili, uliona wapi me akiachana na wazazi wake akaondoka na huyo mkewe wakaenda kukaa mbali na kwao wakaanza maisha huko bila hata kufika kwao??
Unatakiwa uuelewe huo mstari na maana yake ili uweze kuuweka kwenye utendaji. Hakujawahi tokea me akaondoka kwao akaenda kusikojulikana. Ila kila mara ni ke huondoka kwao akaambatana na me wakaenda kukaa kwa me. Ke hubadili hata jina lake na kuitwa //asha /abdala japo babake na vyeti vyake vimeandikwa Asha Selemani. Upo hapo??
 
Tatizo siyto utamaduni wa mahari kuwa mbaya bali tatizo ni matumizi mabaya ya mahari na tafsiri mbivu ya mahari iloingia katika kizazi cha sasa cha wazazi wenye tamaa za fisi kupindukia.
Mahari ni zawadi anayopewa binti na mwanaumne na zawadi hii inakuja ni makubaliano katika ya binti na muoaji,kwa hiyo ukiona baba mzazi au mama mzazi anakomalia kuweka idadi ya mahari kwa binti yao,muulize WE MZEE UNATAKA KUFANYWA NINI ?
 
India wanaume ndiyo wanaotolewa mahari, sijui hilo nalo utalizungumzia aje...

Mengine yaache kama yalivyo, wewe nenda katoe hiyo mahari...

Cc: mahondaw
Hahah jha aha aha ndio maana huwa wanatyonea wivu sana wanaume wa bongo sababu sisi tunaoa na wao wanalipiwa mahari,sijui huwa wanajisikiaje
 
Moja ya vitu vinavyonikwaza linapokuja suala la ndoa ni mahari. Ni kama nywele za kichwa, zipo hapo siku zote lakini zipo kwa ajili ya kazi gani hujui.

Mahari ipo miaka nenda rudi kama mila au desturi, huku idadi kubwa ya watu wanaoitekeleza wakiitafsiri kama pesa au kitu ambacho hutolewa na mwanaume kama malipo kwa familia ya mwanamke pindi anapotaka kumuoa.

Lakini kimantiki, vitu pekee vinavyolipiwa chini ya jua ni bidhaa na huduma. Tunalipia sabuni ya kuogea na dawa za meno dukani, tunalipia mafuta ya kupikia na sukari kwa mangi hizo ni bidhaa.

Wakati tukienda hospitali tunalipia matibabu, kwenye basi tunalipia nauli, huku Tanzania na Algeria zikicheza kwenye Afcon tunalipia ili kuingia uwanjani kutazama mechi, hizo ni huduma.

Sasa tukirudi kwenye mahari, kwa nini tunailipa familia ya mwanamke ili kumuoa binti yao? Je, ni kwa sababu mwanamke ni bidhaa au ni huduma? Kama sio ni kwa nini tunalipa ili kuoa?

Kuna baadhi ya watu wanajenga hoja kwa kusema kuwa unalipa kama zawadi kwa familia ya mwanamke kwa kumtunza binti kipindi chote hicho sawa ni kitu kizuri, lakini kwa upande wa pili, hata mwanaume ana wazazi, alitunzwa kipindi chote na familia yake, itakuwaje kama familia ya mwanamke nayo ikitoa zawadi ya pesa nyingi au ng’ombe kwa familia ya mume, haitapendeza?

Lengo hapa si kwamba na wanaume pia wawe wanatolewa mahari, lengo ni kujaribu kuona mahari ipo hapo siku zote kwa ajili gani?

Kama ipo kwa sababu zisizokuwa na msingi, kwa nini iendelee kuwepo? Yaani kwa nini tusiitoe kama ina sababu zisizoeleweka. Au kama tunaipenda sana, basi familia ya mwanaume itoe kwa mwanamke na familia ya mwanamke ifanye kinyume chake, itoe kwa mwanaume pia.

Kuna watu watabeza tunachokizungumza hapa, kwamba wanaume siku hizi wamekuaje? Wanadai kulipiwa mahari pia.

Lakini kama watatokea watakaobeza hivyo, wajiulize kwa nini wanabeza mwanaume kulipiwa mahari, watagundua kuwa kumbe hii kitu mahari ina kawaida ya kumshusha mtu anayelipiwa, anaonekana mdogo, anaonekana hana nguvu, anaonekana hajiwezi, anaonekana ni bidhaa, anaonekana ni mtoa huduma tu jambo ambalo kiukweli halistahili kuwemo ndani ya ndoa.

Kwa mtazamo wangu, mahari kwenye ndoa ni kama kipande cha utumwa kilichobaki, na kikapewa jina lingine zuri zuri ili kuufanya utumwa kuwa halali.

Natamani siku moja nione wanaharakati wanaotetea haki za wanawake, waamke na hii ya kupinga mahari kwa mwanamke pindi anapoolewa kwa sababu inamshusha thamani mwanamke.
Nitarudi
 
Back
Top Bottom