Tuongee Kiume: Mahari ni mabaki ya utumwa yaliyopewa jina zuri

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
Moja ya vitu vinavyonikwaza linapokuja suala la ndoa ni mahari. Ni kama nywele za kichwa, zipo hapo siku zote lakini zipo kwa ajili ya kazi gani hujui.

Mahari ipo miaka nenda rudi kama mila au desturi, huku idadi kubwa ya watu wanaoitekeleza wakiitafsiri kama pesa au kitu ambacho hutolewa na mwanaume kama malipo kwa familia ya mwanamke pindi anapotaka kumuoa.

Lakini kimantiki, vitu pekee vinavyolipiwa chini ya jua ni bidhaa na huduma. Tunalipia sabuni ya kuogea na dawa za meno dukani, tunalipia mafuta ya kupikia na sukari kwa mangi hizo ni bidhaa.

Wakati tukienda hospitali tunalipia matibabu, kwenye basi tunalipia nauli, huku Tanzania na Algeria zikicheza kwenye Afcon tunalipia ili kuingia uwanjani kutazama mechi, hizo ni huduma.

Sasa tukirudi kwenye mahari, kwa nini tunailipa familia ya mwanamke ili kumuoa binti yao? Je, ni kwa sababu mwanamke ni bidhaa au ni huduma? Kama sio ni kwa nini tunalipa ili kuoa?

Kuna baadhi ya watu wanajenga hoja kwa kusema kuwa unalipa kama zawadi kwa familia ya mwanamke kwa kumtunza binti kipindi chote hicho sawa ni kitu kizuri, lakini kwa upande wa pili, hata mwanaume ana wazazi, alitunzwa kipindi chote na familia yake, itakuwaje kama familia ya mwanamke nayo ikitoa zawadi ya pesa nyingi au ng’ombe kwa familia ya mume, haitapendeza?

Lengo hapa si kwamba na wanaume pia wawe wanatolewa mahari, lengo ni kujaribu kuona mahari ipo hapo siku zote kwa ajili gani?

Kama ipo kwa sababu zisizokuwa na msingi, kwa nini iendelee kuwepo? Yaani kwa nini tusiitoe kama ina sababu zisizoeleweka. Au kama tunaipenda sana, basi familia ya mwanaume itoe kwa mwanamke na familia ya mwanamke ifanye kinyume chake, itoe kwa mwanaume pia.

Kuna watu watabeza tunachokizungumza hapa, kwamba wanaume siku hizi wamekuaje? Wanadai kulipiwa mahari pia.

Lakini kama watatokea watakaobeza hivyo, wajiulize kwa nini wanabeza mwanaume kulipiwa mahari, watagundua kuwa kumbe hii kitu mahari ina kawaida ya kumshusha mtu anayelipiwa, anaonekana mdogo, anaonekana hana nguvu, anaonekana hajiwezi, anaonekana ni bidhaa, anaonekana ni mtoa huduma tu jambo ambalo kiukweli halistahili kuwemo ndani ya ndoa.

Kwa mtazamo wangu, mahari kwenye ndoa ni kama kipande cha utumwa kilichobaki, na kikapewa jina lingine zuri zuri ili kuufanya utumwa kuwa halali.

Natamani siku moja nione wanaharakati wanaotetea haki za wanawake, waamke na hii ya kupinga mahari kwa mwanamke pindi anapoolewa kwa sababu inamshusha thamani mwanamke.
 
Kwani unapolipa mahari unakuwa hujajua bado?
km umekiuka mashart halisi ya ndoa yenye vigezo vyote au ile misingi ya kimaadili then yes, utakua umejua kwaio umekubaliana na hali....
Lkn kama ndio ile usiguse mpk umiliki utakutana na suprise attack
 
Wewe zaa nae pita hivi....
Sio lazima ulipe mahari
tapatalk_1552155620493.gif
 
Kuna binti mmoja amenishauri kama nina 300,000/= nifanye mpango wa kumchukua mazima.
 
Kuna baadhi ya watu wanajenga hoja kwa kusema kuwa unalipa kama zawadi kwa familia ya mwanamke kwa kumtunza binti kipindi chote hicho sawa ni kitu kizuri, lakini kwa upande wa pili, hata mwanaume ana wazazi, alitunzwa kipindi chote na familia yake, itakuwaje kama familia ya mwanamke nayo ikitoa zawadi ya pesa nyingi au ng’ombe kwa familia ya mume, haitapendeza?
Wahenga walikaa na kulijadili hili jambo kwa undani sana hadi kufikia uamuzi kuwa; Mwanamume atoe "Mahari" ambayo mimi naiita "Fidia" kwa ajili ya mwanamke unayetaka kumuoa kwa sababu kadhaa ila kuu ni:

Malipo kwa kumfidia pale kwao anapotoka. Unampewa moja kwa moja, unaenda naye kusikojulikana kabisa na yeye anakufuata kwako. Kule kwako kuna wazazi wawili kama wale aliowaacha kwao na sasa ameamua kuja ongezewa kwenu. Familia moja inapoteza mtu au inapungukiwa mtu na familia nyingine inaongezewa mtu. Hapo huoni faida ya kulipa mahari?? Sema usemavyo ila inaitwa; Kulipa mahari. Unapotumia neno "Lipa" maanake; Umenunua kitu, sasa lipa uchukue.

Kwa kuwa ni, "Mtu" tunaogopa kusema; "Nimenunua". Kutokusema hivyo hakumaanishi kuwa hujanunua. Usingelisema; Nilimlipia mahari. Kama ulilipa mahari, ulimnunua. Lakini, sitaki kumwambia mke wangu maneno hayo ila kiukweli nilimnunua kutoka kwao kwa bei ya maridhiano mazuri tu.

Wanawake msinichukie ila ndo hivyo. Kule kwetu Tarime; Huruhusiwi kusema kuwa; Nitareta shilingi 4 milioni na ng'ombe 100 kama mahari yangu kwa binti yenu. Wale wamura walioko hapo watakuua ufe fwiii. Kwetu ni matusi kutanguliza pesa mbere harafu ng'ombe nyuma.

Tupo tiyari kusikia; Nitatoa ng'ombe 2 na shs 4milion. Tutakusikilisa na tutaanza kusumacha. Si vinginevyo.
Hayo yote ni yale yale. Tunamnunua mke.
 
km umekiuka mashart halisi ya ndoa yenye vigezo vyote au ile misingi ya kimaadili then yes, utakua umejua kwaio umekubaliana na hali....
Lkn kama ndio ile usiguse mpk umiliki utakutana na suprise attack
Miiko ya ndoa mnaijua nyie vijana wa hiki kizazi?
 
Back
Top Bottom