Tuongee kifamilia/kitamaduni:-Kwa mwanamke je ni sahihi kufua nguo za baba mkwe wake?

Tuongee kifamilia/kitamaduni:-Kwa mwanamke je ni sahihi kufua nguo za baba mkwe wake?

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
11,250
Reaction score
24,084
Kulingana na mila na desturi zetu zinatofautiana kabila hadi kabila na jamii nyingine kwenda jamii nyingine.

Ni kawaida kukuta jamii au tamaduni ya watu hawa haziingiliani na tamaduni za jamii/kabila fln.

Mfano kuna baadhi ya makabila huoa binamu zao wengine huzaa na dada zao nk.

Kule uchagani kama sikudanganywa mwanamke kukupigia goti kama huku usukumani huhesabiwa kama tusi lakini usukumani ni heshima na ni lazima! Huo ndo utofauti kwa kifupi wa jamii na tamaduni zake.

Leo ningependa tujadiri kifamilia zaidi bila kuangalia kwanza tamaduni na desturi zetu kama ni sahihi kufua nguo za baba mkwe kwa wanawake.

Ikumbukwe kwa desturi za kisukuma ni marufuku na haitakiwi kabisa kufua nguo za baba mkwe wake.

Wasukuma walienda mbali zaidi hata bafu walikuwa hawachangii na wakwe zao japo kwa sasa hali ni tofauti(wanachangia)

Tukija kwa ujumla wake ni sahihi au sio sahihi kufua nguo za baba mkwe wako? Iwe kwa sababu yoyote Ile?

Kama sio sahihi ni kwanini?
Manyanza

Karibuni
 
Mkuu hii hoja yako kidogo ni ngumu na ina ukakasi sana kutokana na jinsi mabadiliko yanavyoletwa na usasa 😃
Lakini tukumbuke Kila jamii ina mizizi yake ya heshima. Tukiikanyaga kwa visingizio vya kisasa, tunapoteza utambulisho wetu. Ila tusisahau ubinadamu haupaswi kusahaulika pale ambapo hakuna mwingine wa kusaidia. Hekima ndiyo msingi.
 
Kama mkwe Hana mke ? au ni wazee ?.

Unafua baadae mawifi na mashemeji wanakuja kusema umeua baba yao,,

NAWATAFUTA MAWIFI KWA MARA NYINGN,,
 
Iwe kwa sababu yoyote ile si sahihi mwanamke kufua nguo za baba mkwe, wanaoweza kufua nguo hizo iwapo mhusika hajiwezi ni watoto wa mwanamke (wajukuu jinsia zote), watoto wake wa kiume, kaka zake na wadogo zake na hapo iwapo mke wa mhusika hayupo kabisa.
 
Huyo anayeopereiti hiyo mashine haitakiwi awe mkwe.Tatizo siyo nguo kufuliwa,je anayefua ninani?
Kama baba mkwe au simply baba huwezi ku operate washing machine kisa ubaba wako basi kuna tatizo big sana sehemu
 
Kama baba mkwe au simply baba huwezi ku operate washing machine kisa ubaba wako basi kuna tatizo big sana sehemu
Yawezekana baba mkwe ni mgonjwa,ndomaana lakini hiyo haihalalishi MKWE kuopareiti washing machine,afue boksa na nguo nyingine za babamkwe wake,ni utovu wa nidhamu.
 
Yawezekana baba mkwe ni mgonjwa,ndomaana lakini hiyo haihalalishi MKWE kuopareiti washing machine,afue boksa na nguo nyingine za babamkwe wake,ni utovu wa nidhamu.
Binadamu yoyote mwenye changamoto ya afyq anahitaji msaada wa kibinadamu, haijalishi ni mkwe au baba mkwe.

Unataka kuniambia wewe kama Baba mkwe upo nyumbani, wengine wote hawapo na njaa inakuuma, chakula kipo jikoni, utasubiri hadi mabinti au mkeo arudi aje kukuwekea chakula ?
 
Back
Top Bottom