TUONGEE ASUBUHI ON STAR TV Sunday 27th FEB 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TUONGEE ASUBUHI ON STAR TV Sunday 27th FEB 2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yahya Mohamed, Feb 26, 2011.

 1. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #1
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mfumko wa bei za bidhaa-Hatari!!!
  Habari wanajamii
  Nimeona nishee dukuduku langu pamoja nanyi wanajamii, ingawa ninafahamu kuwa si wote wanaoathirika na hali hii kutokana na utofauti wa vipato vyetu. ila ninaamini kwamba kuna baadhi yetu tunaumia na hili.
  Hivi huu mfumko wa bei za bidhaa serikali inatufikiria nini wananchi??? kumekuwa na kupanda kwa gharama za bidhaa kila kukicha, kila mtu ana aamua apandishe kulingana na maamuzi yake, hivi serikali haitufikirii sisi tunaopokea mishahara ya TGs D???
  Mafuta taa/kupikia/gari bei juu, hapa kwetu dizel mpaka 2200, sukari sasa ni 2000 @kg, mchele 1200, harage bei juu,bia juu daladala wamepandisha nauli.. Jamani hawa EWURA na wengineo wapo wapi? kwanini bei zanapanda tu watu wakiamka asubuhi? ..

  Hali hii bunge halijajadili budget na makodi yake, je budget ikishapitishwa sisi wa vipato vya chini tutaweza kuishi kweli?... wabunge baada ya kujadili hali ya uchumi na mfumuko wa bei kazi kubishania ubora wa vyama....
  Natamani kuukana utanzania mie!!!!
  POSTED BY BY SENIOR MEMBER JF

  LIFTED BY TUONGEE ASUBUHI
  Maoni yanakaribishwa katika mada hii itakayojadiliwa kesho asubuhi kuanzia saa 1 na dk 30 asubuhi kupitia Star TV
  Naomba kuwasilisha

  Yahya M
   
 2. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba Mtuletee wachambuzi bora sio watu hovyo hovyo, maana mada hunoga kwa kuwa na watu makini. Nani atakuwepo, ni kweli mfumko sasa ni balaa sana na maisha si maisha tena
   
 3. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Afadhali umerejea ili uchukue maoni yetu hapa jamvini, stay tuned tunakuja na vina vya mada hiyo ili kesho ufanye pure presentation hapo star tv...
   
 4. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #4
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ni muda mrefu hakika, Nami nategemea michango yenu kafanikisha zoezi hili hapo kesho. Tukirejea kwa nguvu upya
   
 5. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  Tatizo la Tanzania kuna utofauti mkubwa sana wa viwango vya mishahara tofuati na wenzetu mfano huku ughaibuni mhudumu wa ofisi anapokea kiwangokikubwa na hakitofautiani sana na wengineo ili aweze kujimudu malazi,makazi,chakula na matumizi mengineyo,lakini kwa bongo ukiangalia viwango wanavyolipwa EWURA, tume mbali mbali, TRA,majaji,wakurugenzi nk ni kikubwa sana kuliko hata kazi wanazofanya. Kwao hawamjui mwenye njaa.

  Inabidi serikali ifanye juhudi ya kuboresha uchumi, maliasili yetu tuimiliki wenyewe manake tumeshabinafsisha,madini yetu tumebaki na mashimo tukiwaacha wazungu watuibie bila hata kulipia kodi viongozi wapo tu wamelala usingizi tena hata mkwere aliulizwa akajibu hajui kwa nn Tanzania ni maskini inauma sana,ma********* wanatuuzia mafuta kwa bei juu wanayotaka wao na ushahidi upo kwa EWURA kila wanapopitisha bei ya mafuta wanalipwa % FULANI. nchi imeoza wajamini we have to wake up kama tunataka maisha mazuri.

  Aghhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh bora
   
 6. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #6
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Watakuwepo wachambuzi mahiri wenye hoja na si majina mkuu, weka mchango wako pia kama nyongeza
   
 7. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mh mie naona kama siku hizi haka Ka-TV kanafulia vile maana vichwa vyenye akili ya kuchambua mambo na kuhoji mambo vilivyokuwepo zamani sivioni tena siku hizi.

  Mnao CHADEMA kikosi kizima kanda ya ziwa, mmeshindwa kuwaita hiyo kesho mkae nao hapo watoe hoja za maandamano yao ya kanda ya ziwa, mkakati wao? Mlingano wao na yanayotokea Libya na yaliyotokea Misri na Tunisia na hofu ya watanzania katika hilo? Udhaifu wa upinzani kwa ujumla na umuhimu wa upinzani kuwa kambi moja ingawa sio kulazimishwa bali kwa makubaliano na kuondoa tofauti? Matumaini ya watanzania katika upinzani wa leo? Siku 100 za serikali mpya zilizomalizika na mwelekeo wa siasa za tanzania? Na mambo mengine mengi ambayo wenzenu kama Fox News, CNN, Al-Jazeera, Sky, NBC, VOA na wengine wengi makini wangeweza kuyafanyia kazi kwa kutumia mwanya wa uwepo wa vigogo hao wa CHADEMA kanda ya ziwa.

  Huwa hamuoni Ahmadneejad, Hugo chavez, Gadafi nk wakienda nje ya nchi zao vyombo vya habari huko vinavyo-take advantage ya kuwanasa na kuwa na mahojiano maalum ili kukata kiu ya watazamaji wao? Kumbuka Journalist unatakiwa kuwa Devil's advocate. Jaribuni kubadilika nyie watu wa Star TV jamani ama tafuteni watu wanaojua kuchanganua mambo sio mnachagua vihoja dhaifu kujadili na wageni dhaifu na mbaya zaidi hosts dhaifu zaidi.

  Ni ushauri tu lakini jamani

  :spider::spider::spider::spider::spider::spider:
   
 8. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #8
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mawazo yako yanaheshimikia
  Yahya M
   
 9. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hali ya maisha kwetu wananchi wa Tanzania ni mbaya na inazidi kuwa mbaya zaidi, hali hii ni sawa na BOMU ambalo lasubiri tu cheche lipate kulipuka. Inastaajabisha na kusikitisha kuona taasisi nyeti za serikali kutokemea hali hii tete kwa sisi raia kuangamia na mifumuko hovyo ya bei zenye kutuathiri, nasema tena inauma, inahuzunisha na inasikitisha sana.

  Imenisikitisha kupindukia kuona wateule wa wananchi WABUNGE kuendekeza vijembe, kejeli na majivuno wawapo kwenye chombo muhimu cha kutetea wananchi ambacho ni BUNGE. Si wabunge wa upinzani wala wa chama tawala...WOTE WAMEJISAHAU WAJIBU WAO KWETU SISI TULIOWATUMA. Wameingia bungeni tena ni muda mfupi sana wamesahau kutetea hali mbaya ya maisha, hali mbaya ya vipato, mifumuko hovyo ya bei za bidhaa, kodi kubwa kwa wafanyakazi etc.

  Leo hii mafuta yanapanda bei hovyo hovyo tu, nauli zapanda bei kila siku, bidhaa adhimu zapanda bei na wananchi kiujumla hatujui mustakabali wa hatma ya maisha yetu.

  Nikionacho...si muda mrefu hali ya ndani ya nchi itachafuka, minong'ono juu ya hali hii mbaya ya maisha imeshamiri na inatia khofu kwa kutokujua JE KWELI TUNAYO SERIKALI YENYE KUKEMEA UOVU HUU?

  Enyi wafanya biashara na watawala...na mtuhurumie sisi viumbe, tuhurumieni kwani safari yetu sote ni moja hapa duniani.
   
 10. Yahya Mohamed

  Yahya Mohamed Verified User

  #10
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mchango wako Umefika Mpevu

  Yahya M
   
 11. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Dah hii hali sio hali hasa sisi walimu mshahara mdogo makato ya kutosha kodi asilimia 14, CWT asilimia 2, bima ya afya, ingawa hadi leo hatujapewa kadi, NSSF zote kama aslimia 7 huku bado hatujapewa nyumba so kodi zitokane na huo huo mshahara bado usafiri kufika kazini tunajitegemea, hakuna vitendea kazi kalamu, vitabu, teaching aids tunatafta kwa hela yetu unafkiri kwa kipato hiki ntatafta hvo vitu ndo maana matokeo ni poor huwez amin hta scheme of work na lesson plan hatuandai coz eti tununue karatasi za kuandikia kwa pesa ipi? Huku wakuu wa shule wananeemeka kwa marupurupu wakishirikiana na maafsa elimu hawanunui vifaa.

  Halafu uki-compare na wenzetu hali yetu ni mbaya, kama juzi nliwaza na nkajuta why nimekuwa teacher coz nilikutana na watu tulio-graduate nao chuo mmoja alisoma BBA na mwingine Law yani wako safi wana usafiri hadi kimavazi hatulingani huwezi amini ni miaka michache tu nyuma tulikuwa sawa wote tukihemea boom la bodi hebu watuangalie kwa jicho la tatu coz sisi tuna-deal na kitu sensitive sisi ndo tunamould na kushape taifa la leo na kesho
   
 12. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mkuu,

  Kwa neno zima hapo unamaanisha kuwepo na hali mbaya sana kwa WALIMU ama sivyo?

  Kiujumla poleni wenye fani hizo, ila msisikitike jichangeni nanyi muanzishe vijishule vitawatoeni ipo siku. Usijilaumu kwa proffession yako, u r still marketable on the other way.
   
 13. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mada inakuwa ya maana kulingana na wazungumzaji wakuu. Ukiwaleta watu mbumbumbu kama tambwe hiza itakuwa ni bure tu.
   
 14. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Tunashukuru kwa taarifa Yahya nitapiga simu kesho na kuchangia, kwani hali inatisha sana na hakuna kiögozi yoyete anayelizumguzia mala kuchukuwa hatua wabunge juzi wanafikiria jinsi ya kuboresha maslahi yao bila kufiliria kwanza maslahi ya waliowachagu kwenza.
   
 15. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  hali ni mbaya ambayo inahitaji matendo zaidi ya hizi debate ambazo zinainamia kwenye vyama badala ya hali halisi!
   
 16. F

  Froida JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ahsante Yahaya.

  Kwa kweli Ni vizuri Star TV mumeliona hilo,Kunatatizo kubwa sana katika mfumo wa ulinzi na haki za mlaji(Consumer rights) ndio maana unakuta mfanya biashara na haki nyingi zinazomlinda kwa sababu sheria na mifumo ya ulinzi kwa mlaji haijawekwa wazi na iliyopo michache ni kandamizi kwa mwananchi.

  Ndio maana unaona hata bidhaa zisizofaa kwa uhai wa binadamu zinawekwa sokoni ikiwemo vyakula,nguo,vifaa mbalimbali vya ndani,vya ujenzi, vya kilimo nakadhalika.Hakuna mlinzi ,kutokana na uvunjifu wa haki za msingi za mlaji ,leo mfanyabiashara ana uhuru wa kuamua kuuza nini,kwa wakati wowote na kwa bei yeyote na mahali popote. Hakuna mahali popote duniani haya mambo yanafanyika ambapo serikali haisimamii ulinzi wa mlaji katika nchi kasoro hapa Tanzania.

  Kutokana na udhaifi huu ni rahisi sana kwa mfano wananchi kuharibika kisaikolojia kwa sababu hawana uwezo wa kupanga maisha ,unakuta wananchi wana hasira sana,wanajiingiza kwenye matendo ya kukosa imani na serikali na pia na wananchi wenzao ikiwemo wengi kujinyonga,kutaka kuwauuwa wenzao kwa visingizio vya wachawi na vibaka,wengine kukimbia na kutelekeza familia na kuzalisha watoto wengi wa mitaani,na mimba za utotoni kwa kweli upandaji holela wa bidhaa ni chukizo kubwa sana lkwa sisi wananchi kwa sababu wengi wetu vipato vyetu halali havitutoshi hata kwa siku tatu usishangae wafanyakazi tukijiingiza kwenye biashara ya kutunza vitoto vijiti vilivyokufa ili tukavizike kwenye mashimo ya taka kwa ujira wa elfu tano.

  Serikali ya awamu ya nne isiporekebisha hali hii itambue kwamba wananchi tutawawajibisha siku moja.
   
 17. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #17
  Feb 26, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Nashukuru umesa mkuu. Hii tabia ya star huwa naiona kama uhujumu. Wanatumia muda mwingi na wenye thamani kujadili vimambo dhaifu na visivyo na mvuto wala suport yetu watazamaji. Badilikeni tuwe tunashiriki katika mijadala yenye tija. Hiyo mijadala mingine muwe mnaitafutia muda tofauti na tuongee asubuhi. Ntachangia kesho.
   
 18. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #18
  Feb 26, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Taabu siyo mishahara midogo. Ni mfumuko wa bei. Tofauti ya vipato pia kwa watumishi ni kubwa sana. mwinine apate m4 hadi zaidi ya 20 na mwinine laki unuru. unadhanh wenye kipato cha juu wataona kama kuna shida? Wakipandisha kima cha chini ndo hali itakuwa balaa kwa kuwa lo wages huwa na watu wengi hasa viwandani. wapunguze mishahara yao na watakuwa wanajalg watu wa chini.
   
 19. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #19
  Feb 26, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Yahaya, Bunge letu halikujadili matatizo ya kila siku ya matanzania kama vile inflation, Umeme na huduma muhimu badala yake walijikita kwenye mijembe zaidi ya kuibeba serikali kwa kila hali.
  Tatizo la kununua vitu kwa kutumia USD hapa Tanzania badala ya TSh. linaongeza ukali wa maisha! kwa mfano huwezi kufanya malipo ya usafiri wa Anga kwa TSh.
   
 20. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #20
  Feb 26, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Asante sana Yahya, Hali ya hapa Tanzania ya kuwepo kwa tofauti kubwa ya kipato kati ya mtumishi wa kima cha chini na yule wa juu ndiyo inayo leta matatizo makubwa unapotokea Mfumuko wa Bei, mfano mtu analipwa 135,000 na mwingine 12,000,000* (*Sina uhakika) karibu mara 100 zaidi. Hali inayotokea Libya na iliyotokea Misri na Tunisia chanzo chake ni hali ngumu ya maisha watu hawaoni afadhali ndio wanapoamua kuchukua sheria mkonono viongozi wetu wanaweza kufikiri wako salama lakini wewe ni shahidi kwa maandamano ya Mwanza ya kumtaka JK ajiuzulu. Idadi hiyo inaweza kuingia mtaani kila mkoa na kufanya maandamano. Kwani hali sasa ni ngumu mno tofauti na ahadi za MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA kinachotokea sasa ni MAISHA HOVYO ZAIDI KWA KILA MTANZANIA. Uchapishaji wa pesa mpya bila kuondoa za zamani maana yake ni kuongeza pesa kwenye mzunguko (money supply) haya ndio matokeo yake, pesa nyingi uwezo mdogo wakununua. Serikali inaendeshwa kama hakuna wachumi. JK na timu yake wajipange haiwezekani kupunguza mfumuko wa bei wakati hakuna jitihada za DHATI kuondoa tatizo la umeme. Hadi hapo umeme utakapo stabilise ndiyo tutaweza kuzungumza habari ya kuinua thamani ya pesa na kuipa nguvu ya kununua. Asante sana Star TV kwa vipindi vyenu vyenye mada motomoto. Tunaomba wachambuzi Studio wawe wenye ufahamu wa yanayozungumzwa, siyo akina Tambwe Hiza
   
Loading...