TUONGEE ASUBUHI ON STAR TV Sunday 27th FEB 2011

Shukrani kwa michango yote iliyotufikia mpaka muda huu. Michango hiyo ndo itapata nafasi ya kusikika hewani. Itakayofuata zaidi ya muda huu itakuwa kwa matumizi ya Forum tu. Ila kama ujumbe utakuwa mfupi unaweza kushiri LIVE katika simu yangu ya kiganjani 0717 000013 (TEXT FUPI INAYOELEKEA KATIKA HOJA MOJA KWA MOJA) pia itasomwa Live
Shukrani kwa wanaJF wote walioshiriki, shukrani pia kwa wadau mlioona umuhimu wa suala hili (Mwanakijiji, Nyuyu and Speaker)

Yahya M
 
Tatizo ninaloliona mimi ni kuingiza siasa kwenye uchumi na sema hivyo kwasababu baada ya JK kuapishwa tu tulianza kushuhudia vionja vya kupata kwa vitu hovyo
pili wanao simamia kutokuweka masilahi ya taifa mbele yaani leo unaweza kwenda kununuua mafuta ya kupikia leo, kesho ukienda unakuta yamepanda zaidi ya 2000 ni vitu vya kushangaza sana sijui kama nilishashudia kupanda kwa vitu hovyo hovyo hivi.....
 
Tatizo ni uhaba wa uongozi wa juu Tanzania. Wachumi hawatumiki ,tunatumia wabunge wa darasa la saba na fomu4 kujadili bajeti,unategemea nini hapo?
 
Nawashukuru wachangiaji wanachambua vyema maana halisi ya mfumuko wa bei kwa watanzania.
 
swala si uzalishaji. ni udhibiti na matumizi ya mapato unafanyikaje? a way forward kwa sisi kuendelea ni kiongozi mkuu kuchukia rushwa toka rohoni mwake. atafanikiwa kwa haraka kuleta maendeleo. mfano ni rwanda.
 
Wanajitahidi ila si wachambuzi kwa kina kulingana na wimbi lilivyo
 
Tatizo ni uhaba wa uongozi wa juu Tanzania. Wachumi hawatumiki ,tunatumia wabunge wa darasa la saba na fomu4 kujadili bajeti,unategemea nini hapo?
Kwani enzi za Mkapa bajeti ilikuwa inajadiliwa na watu wenye elimu gani?
 
Tatizo tuna viongozi dhaifu, hawana uwezo wa ku-act the soonest, yani uwezo wao kiakili ni mdogo...watu kama hawa mbinu yao kubwa katika uongozi ni kukaa kimya....kwa sababu hawana jipya kutokana na uwezo wao kuwa finyu, wewe katika hali kama hii umemsikia kiongozi yeyote akitoa tamko lenye maslahi kwa taifa??? mara nyingi huwa ni vijembe tu, na sura zao huwa hazina u-serious zaidi ya mzaha, we need a president who can stand on his own feet during hard situations, sio mtu ambae mpaka ashauriane na japo la watu ndipo aje na jibu, na mara nyingi majibu yake huwa ya kisiasa zaidi ya kitaalam.

hatuna nishati madhubuti, hatuna mtu anaesimamia bei(hawa ewura,sumatra wapo tu wanalea vitambi vyao na kula kiyoyozi hovyo hovyo), serikali ipunguze matumizi yasio ya lazima(kama safari za raisi na timu anayoendaga nayo,magari,na ofa nyingi wanazopeana), serikali ianze kuipenda nchi yake(sio kama sasa ambapo wanajijali wenyewe), serikali iwe na meno ambayo yatamg`ata yeyote yule atae taka kuiharibu nchi yetu(mwangalie kagame anavyoipeleka serikali yake).

haya mambo yanayoendelea si yakuyachukulia poa, hiki ni kizazi kingine jamani, tunafikiria fasta na tunaheshimu tunachofikiria, hatuna woga tukiamua tumeamua, so serikali iendelee kutuchukulia poa one day watatambua kwamba wananchi ndio tuliwaweka madarakani.
 
Hivi hakuna mfumo mwingine mbadala wa kuongoza nchi hii tofauti na siasa?
Inasikitisha kwa nchi kama Tanzania ambayo watu wake asilimia 80 ni maskini, na asilimia 60 ni fukara kabisa bidhaa kupanda bei kila kukicha. Eti kisa kulipa gharama za uchaguzi kwenye mgongo wa economic shake up kwenye soko la dunia. huu ni wizi mtupu! Iko siku watanzania tutaamua, na hapatakalika.
 
dah hii hali sio hali hasa sisi walimu mshahara mdogo makato ya kutosha kodi asilimia 14, CWT asilimia 2, bima ya afya, ingawa hadi leo hatujapewa kadi, NSSF zote kama aslimia7 huku bado hatujapewa nyumba so kodi zitokane na huo huo mshahara bado usafiri kufika kazini tunajitegemea, hakuna vitendea kazi kalamu, vitabu, teaching aids tunatafta kwa hela yetu unafkiri kwa kipato hiki ntatafta hvo vitu ndo maana matokeo ni poor huwez amin hta scheme of work na lesson plan hatuandai coz eti tununue karatasi za kuandikia kwa pesa ipi? Huku wakuu wa shule wananeemeka kwa marupurupu wakishirikiana na maafsa elimu hawanunui vifaa. afu ukicompare na wenzetu hali yetu ni mbaya, kama juzi nliwaza na nkajuta why nimekuwa teacher coz nilikutana na watu tuliograduate nao chuo mmoja alisoma BBA na mwingine Law yani wako safi wana usafiri hadi kimavazi hatulingani huwezi amini ni miaka michache tu nyuma tulikuwa sawa wote tukihemea boom la bodi hebu watuangalie kwa jicho la tatu coz sisi tunadeal na kitu sensitive sisi ndo tunamould na kushape taifa la leo na kesho

Enyi walimu, nyie ndo mnaochangia kwa kiasi kikubwa nchi hii kuwa na utawala mbovu, kwanza nyie ndo mlio sambaa nchi nzima, mnatumika kuirudisha CCM madarakani mnaposimamia uchaguzi. Ninyi mkiamua kuiondoa CCM inayosababisha manyanyaso haya madarakani, hata kesho itaondoka. TUMIENI STYLE YA KARUME KENGE ALIYE KATAA KWENDA SHULE mtaona matokeo kama Misri na Tunisia.

Kwa vile mko kila kona ya nchi, wahamasisheni wananchi kwa njia mbali mbali ili wajue haki na wajibu wao katika kuipigania nchi yao iliyobinafsishwa kwa muiran RA. Mkisimama kwa pamoja mkaweka msimamo kupitia chama chenu cha CWT, mnaweza kuishinikiza Serikali ifanye mnavyotaka ili msiendelee kulalamika.

Walimu mnapo simamia uchaguzi, hakikisheni hakuna uchakachuaji wa kuipendelea CCM kwenye vituo visivyo na mawakala wa vyama vingine.

Walimu mna nguvu kubwa ya kuleta mabadiliko ya kiutawala ila hamjui kama mna nguvu hiyo. Kulalamika tu haisaidii!
 
Kwani enzi za Mkapa bajeti ilikuwa inajadiliwa na watu wenye elimu gani?

Mkwere ana kwambia uwaziri hausomewi, hivyo kwenye baraza wamo wachumba, washikaji, mafisadi nk, Mfano; Mmalawi Mkuro mwenye shahada ya mtaani atadhibitije mfumuko wa bei? Utaona muziki kwenye Bunge la Budget, lazima watajichanganya tu na wapinzani watawakaba koo, kama aliwapelekea wafadhili budget feki wakamstukia unategemea nini!
 
Huyo Musa Mziya kwa konklusheni yake naye nimemwona ndalo na lofa tangu leo.
 
Kwani enzi za Mkapa bajeti ilikuwa inajadiliwa na watu wenye elimu gani?

unataka kusema wakati wa mkapa kulikuwa hakuna mfumuko wa bei au?naweza nkawa sijaelewa swali lako mkuu. Ila maana yangu kubwa ni kuwa hatuwatumii wachumi na wataalamu wetu. Ni ajabu wataalam wanatengeneza bajenti(preliminary budgeting) lakini ikipelekwa bungeni wanasimama waliokimbia umande na kukata fungu la wizara moja kwenda nyingine,na kuvurugua professional economic planning. Mfano,wabunge wanakata bajeti ya wizara ya elimu rejea mwaka 2006/7 na pengine wanaongezea kwenye administration cost,mwaka wa bajeti unaisha ela za administration zinarudi hazina na uko kunafojiwa voucher za ajabu,chukulia wilaya ya kinondoni,kila mwaka ela ilikuwa inarudi hazina kila mwaka wakati mkulima wa mhugo,mahindi na mtama rungwe anakosa mbolea. Tufike wakati tuwaache professionals wafanye kazi yao kuliko kufanya kila kitu ni siasa! Politics is one aspect,we have economic,social,cultural aspects contributing to national develop,but leaving one aspect to override others,we limit development. Sisi tumezoom political aspect ndo imeze zilizobaki, tunapotea! Huwa najiuliza profession ya sheria ni nini kama tunawaruhusu akina Prof.maji marefu,vick kamata ndo wakatunge sheria,wakati wanasheria wanakimbilia kuwa advocates tu! Tusimtafute mchawi,tunao live, wasiokuwa na professional approach ndo wamepewa madaraka ya uhamuzi wakati wataalamu wanawekwa pembeni,jamani ehe,tumieni wataalam!mfumuko wa bei ni kitu kipana sana kiuchumi na kina vyanzo vingi,tusikae kusikiliza siasa tu tutapotea. Mkuu kama una ufahamu wa "inflation" jaribu kupitia tena makabrasha yako,ndo uone si siku cha kutaja taja kirahisi,it needs professional approach. Sijui kama tuko wote mkuu! Gudtym.
 
Tatizo la Tanzania kuna utofauti mkubwa sana wa viwango vya mishahara


Mkuu Lokissa nadhani hapo kwenye Gape la mishahara ni ukweli usiopingika, wengi wenye access ya kuongea kwenye vyombo vya habari na wenye kupata information ni wale wenye uwezo wa kununua sukari kwa hiyo pesa 2000, huo mjadala ungekuwa mzuri kama wangeingia mtaani (USWAZI), na kuona watu wanavyoishi kwa shida, unaweza usiamini, Mtaani maisha ni magumu mno, mtu anafanya kazi kwa muhindi kwa mshahara wa 80000/= kwa mwezi, nauli ni 500 kwenda na kurudi kwa siyeunganisha safari (magomeni to kariakoo)
, chumba cha kawaida kabisa ni 25000 mpaka 30000, bila gharama ya umeme wala maji, hapo ukiweka gharama za kusomesha, matibabu, chakula, nguo, na mengineyo, ni kweli kuwa hayo maisha ni mamgumu mno
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom