Tuondoe term limit (mihula) kwenye uongozi, haina umuhimu wowote ule

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,028
12,349
Nilikuwa napendekeza.

Tuweze kufikia uamuzi wa pamoja kama nchi kuondoa kipengele cha ukomo wa mihula katika katiba.

Hiki kipengele binafsi naona hakina maana wala faida yoyote ile kinapaswa kuondoshwa.

Uongozi unapaswa kupewa uhuru wa kuongezewa muda wa kuongoza pale utakapo onesha matokeo chanya kwa watu wake.

Tuache kasumba ya kuwa uongozi ni kutawala miaka 10 mitano kwa mitano.
 
Tatizo tutatengeneza royal families maana nachoona hata katika hiyo miaka 10 bafo watu wanataka kuweka koo zao ziwe ndiyo rulers milele itakuaje ikiwa ni hakuna himula?
Sasa hapo ndipo suala la kuimarisha mifumo na taasisi nyengine unapo hitajika.
 
Kitendo cha kuondoa mihula katika bara letu hili ni uwazi kwamba tutakuwa tumewapa watawala nafasi za uongozi mpaka kifo.
Hata mifumo ya sasa bado sio kizuizi kwa watawala wengine kuamua kung'ang'ania madaraka Afrika.

Ni vyema tukaamua kujitofautisha na wengine japo ni ngumu.

Tuondoe term limit tuweke mifumo imara
 
Hata mifumo ya sasa bado sio kizuizi kwa watawala wengine kuamua kung'ang'ania madaraka Afrika.

Ni vyema tukaamua kujitofautisha na wengine japo ni ngumu.

Tuondoe term limit tuweke mifumo imara
Mifumo imara,inawekwa na nani,term limit hata marekani ipo kwenye mifumo imara kabisa.
 
Bibi tozo alishasema Katiba ni Kijitabu tu.

Kwahiyo kisikutishe, anaweza kuamua kuwa Rais wa maisha na hakuna kitu mtafanya
 
Kwa nchi kama ya kwetu ambapo sheria na katiba havifuatwi katika uendeshaji wa shughuli za kiutawala, uchaguzi hauheshimiwi, Tume za uchaguzi hazipo huru, Mahakama na Bunge vimefanywa kuwa idara za Serikali, na Rais amefanywa kuwa mfalme, ni muhimu sana kuwa na ukomo wa uongozi. Tena ni vema, uchaguzi ungekuwa unafanyika kila baada ya miaka 4, na ukomo wa lazima kipindi cha uongozi wa Rais mmpja iwe miaka 8. Miaka 10, ikitokea mmepata Rais wa hovyo, anakuwa ameharibu kila kitu.

Kama tungekuwa na katiba nzuri mpya, kama ile katiba pendekezwa ya Warioba, kukawa na Bunge huru, na tukawa na mahakama huru, kusingekuwa na haja ya kipindi cha ukomo wa Rais. Kwa sababu ikitokea Rais ni mbaya, ataondolewa kupitia uchaguzi. Akiwa hovyo sana anaweza kuondolewa hata kabla ya kipindi cha uchaguzi kupitia Bunge au mahakama.

Kwa sasa, kwa katiba yetu hii ya hovyo, na aina ya watawala tulio nao, na kwa chama hiki CCM kilichojaa mafisadi na watu wanafiki, NI MUHIMU SANA KUWA NA UKOMO WA LAZIMA KWA RAIS, TENA IKIWEZEKANA, UNGEPUNGUZWA NA KUWA MIAKA 8 BADALA YA 10.
 
Back
Top Bottom