idawa
JF-Expert Member
- Jan 20, 2012
- 25,284
- 38,312
- Thread starter
- #21
Wapi hujaelewa mkuu?Bado hiyo habari haieleweki! Kumetokea nini mpaka kusababisha hali hiyo?
Sent using Jamii Forums mobile app
Kifupi Vurugu zimenzishwa na raia wa Zambia ambao ni madalali au wabebeaji, baada ya wenzao kukamatwa jana upande wa Tanzania...
Hao madalali hiyo ni shughuli yao ya kawaida kwa miaka mingi, yaani wazambia wanaotoka maeneo ya mbali mfano Lusaka, Kitwe ama Ndola wakati mwingine Malawi hata Zimbabwe kuja kununua bidhaa Tunduma mara nyingi wakifika huwa wanahitaji wasaidizi ambao ndio hao wabebeaji wakati ununuaji.
Sasa imefika wakati wale wasaidizi wakati mwingine huwaibia hao wageni ama kuwauzi bei kubwa tofauti na hali halisi.
Sasa wafanyabishara wa Upande wa Tunduma wakalalamika polisi kwamba hao watu wanachangia kuharibu biashara hivyo wazuiwe.
Jana ndio ikafanyika operation maalumu kuwakamata hao wabebeaji, baada ya kuona wenzao wamekamatwa walioko nje leo wameanzisha vurugu kwa kuwazuia Watanzania wote kuingia upande wao wa Zambia hata magari yanayovuka mpaka.... Wakishinikiza wenzao waachiwe na serikali ya Tanzania.
Kilichofuata ni mabomu kuwatawanya hao raia, Mpaka wa Zambia na Tanzania imeingiliana sana hivyo kukitokea vurugu upande mmoja wote mnaathirika bila kujali zipo Zambia ama Tanzania.
Sent using Jamii Forums mobile app