Tunduma: Vurugu zaibuka mpakani mwa Tanzania na Zambia , Mabomu ya machozi yapigwa

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
24,192
2,000
Jana kulitokea sitofahamu baada ya Askari wa Tanzania kuwakamata vijana raia wa Zambia ambao huwa wanafanya kazi ya kubebea kwa wateja upande wa Tanzania.

Hao vijana maarufu kama Wamagasi ama madalali, walianza kuzuiwa baada ya wateja ambao ni wazambia wenzao wanaotokea mbali kulalamika kuwa wamekuwa wakiwaibia bidhaa na mali zao...

Sasa jana baada ya wenzao kukamatwa na Polisi wa Tanzania, leo asubuhi nao wameanzisha vurugu kwa kuwazuia Watanzania wanaovusha mizigo, machinga hata magari makubwa yanayoenda Zambia, Congo kuingia kwao.

Wakishinikiza wenzao waachiwe la sivyo hakuna Mtanzania kuvuka upande wao wa Zambia...baadae wakaanza kuchoma matairi na kuzusha mtafaruku.

Polisi wa pande zote mbili wameingilia kati kwa kupiga mabomu ya machozi na kutawanya raia, hivyo maduka yote pande zote mbili yamefungwa yaani Zambia na Tanzania, na mpaka umefungwa kwa muda.

Nakonde (Zambia) and (Tunduma) Tanzania boader post temporarily closed due to protesting youths. Risasi zinafyatuliwa kama Syria vile.

Wazambia wanailalamika Tanzania. Wanasema Tunduma hadi hapo ilivyo ni sababu ya wafanyabiashara wa Zambia

"Tanzanians must learn to co-exist at the Tunduma Nakonde boarder. One thing they don't realise is that, the confusion they have caused has affected their businesses a great deal. They forget that Tunduma is what it is today because of the Zambians and the trade they have with Zambians". Kalalamika Mzambia mmoja.

Shughuli zote mpakani zimesimama.
View attachment 1052880

=====

Geti kuu la forodha ya Tunduma na Nakonde limefungwa kwa muda baada ya raia wa Zambia kuzua vurugu mpakani wakishinikiza kuachiliwa huru kwa raia wenzao wa Zambia wanaoshikiliwa na polisi upande wa Tanzania waliokamatwa kwa tuhuma za uhalifu wa mpakani kufuatia operesheni ya Usalama inayoendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app

Picha
20190324_112020.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app

Hali ilivyokuwa kabla!
IMG_20190324_101600.jpeg
IMG_20190324_102414.jpeg
IMG_20190324_102206.jpeg
IMG_20190324_101604.jpeg
IMG_20190324_102419.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,400
2,000
Nakonde (Zambia) and (Tunduma) Tanzania boader post temporarily closed due to protesting youths. Risasi zinafyatuliwa kama Syria vile.

Wazambia wanailalamika Tanzania. Wanasema Tunduma hadi hapo ilivyo ni sababu ya wafanyabiashara wa Zambia

"Tanzanians must learn to co-exist at the Tunduma Nakonde boarder. One thing they don't realise is that, the confusion they have caused has affected their businesses a great deal. They forget that Tunduma is what it is today because of the Zambians and the trade they have with Zambians". Kalalamika Mzambia mmoja.

Shughuli zote mpakani zimesimama.
IMG_20190324_122935.jpg

=====

Geti kuu la forodha ya Tunduma na Nakonde limefungwa kwa muda baada ya raia wa Zambia kuzua vurugu mpakani wakishinikiza kuachiliwa huru kwa raia wenzao wa Zambia wanaoshikiliwa na polisi upande wa Tanzania waliokamatwa kwa tuhuma za uhalifu wa mpakani kufuatia operesheni ya Usalama inayoendelea.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom