Tunduma ni moja kati ya maeneo muhimu sana kuishi na kufanya biashara ya mazao

amate

Senior Member
Feb 23, 2017
157
377
Moja kati ya maeneo muhimu sana kuishi na kufanya biashara ya mazao (Mahindi, Ulezi, Maharagwe,.....) hapa Tanzania ni Tunduma border. Kwa siku kadhaa nilizoishi hapa Tunduma nmegundua vitu vifuatavyo na kuhisi kama ni eneo mhimu sana kweny biashara.

1. WATU WENGI
Tunduma ina watu wengi sana. Population ilioko Tunduma sehem zote (Tunduma TZ na Nakonde Zambia) zinaweza kubalibiana na jiji la mwanza kwa ukubwa na Population ya watu pamoja na magari.

2. BIASHARA
Mji wa Tunduma una kila aina ya biashara (Mazao, machinga, viwanda vidogo vidogo, maduka, nk). Kwakweli huwezi kuishi Tunduma ukakosa kazi.

3. UTULIVU
Tunduma na Nakonde kwa pamoja pametulia. Hakuna vurugu kati ya wazambia na watz kimasilahi.

4. KILIMO
Wilaya ya Tunduma mpaka sumbawanga hiyo lain inalima mahindi kwa wingi sana. Kwahiyo ukiishi tunduma mjin unaweza kuwa na access ya kulima mahindi pia.

5. TUNDUMA NI NZURI SANA........
 
Tunduma ni boda kubwa tanzania na kila biashara utauza hata iwe madawa ya kulevya yanauzika tu, tunduma kuna wamalawi, wazambia, wabotswana, wazimbabwe, wasouth africa, wanamibia, walesotho, hao wote wanapitia tunduma na kufanyia biashara zake pale note! Ukishangaa unaibiwa kirahisi yaani kariakoo ni salama kwa utapeli kuliko tunduma,
 
Mtoa mada unaijua Tunduma vizuri kweli?
Mahindi ya Tunduma hayatoki Sumbawanga.
Mahindi ya Tunduma yanatoka Halmashauri ya Wilaya ya Momba@zile kata zilizo njia ya kwendea Sumbawanga.

Mahindi ya kutoka Sumbawanga yakifika Tunduma huwa yanapita njia tuuu.

#YNWA
Hujaelewa wew, kasome post vizuri....
 
Back
Top Bottom