Tunduma: Vurugu za kidini zaibuka upya

Tunduma: Vurugu za kidini zaibuka upya

Status
Not open for further replies.

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
25,298
Reaction score
38,440
Maduka yote yamefungwa matairi yanachomwa barabarani, magari ya polisi yanamwagwa mitaani. Chanzo cha vurugu ni mkuu wa wilaya kuzuia wakristu kuchinja na kwamba wanaoruhusiwa ni waislam tu.!!

Apdate:
Diwani anajaribu kuongoea na polisi kama kuna uwezekano wa kusitisha mabomu ili aitishe mkutano wa hadhara..hali bado ni mbaya sana mabom yanapigwa mfululizo.!!

Apdate: saa nane mchana
Polisi wameingia mitaani kulazimisha watu kujifungua ndani, polisi ni kama wamezidiwa wakitawanya upande huu raia wanahamia upande mwingine. Matairi yanachomwa kama kawaida na mabom yanapigwa mfululizo.... Hakujasikika kifo chochote.!

Taarifa kutoka Tunduma mkoani Mbeya zinadai kuwa hali si shwari katika eneo hilo kutokana na kuzuka kwa vurugu kubwa zinazodaiwa kusababishwa na masuala ya kiimani ya nani achinje kati ya mkristo na Muislam .

Mwandishi wetu kutoka Tunduma mkoani Mbeya anaripoti kuwa vurugu hizo zimeanza majira ya saa nne asubuhi kwa makundi ya vijana kuandamana mitaani na kuvutana kuhusu uamuzi wa viongozi wa dini ya kikristo Tunduma kuandika barua kwa mkuu wa wilaya kutaka kuruhusiwa kuchinja wakati wa pasaka.

Ripota wetu anaripoti kuwa kabla ya ijumaa kuu viongozi hao wa dini ya Kikristo walikutana na mkuu wa wilaya ya Momba Abuud Saibea ambae aliwataka kuwasilisha barua rasmi ya kutaka kibali cha kuchinja .

Hata hivyo inaelezwa kuwa vurugu hizo za leo zina mikanganyiko mingi kwani wanaoshiriki katika vurugu hizo ni vijana wapiga debe .....

Vurugu za uchinjaji zilifanyika siku ya Pasaka na hazikuwa na mvutano kwa sababu wakristo walichinja katika bucha zao na waislamu nao walichinja katika mabucha yao ....

Cha kushangaza leo ni baada ya kuibuka kundi la vijana wanaofanya kazi katika stendi na vijiwe mbali mbali ambao ndio walioanzisha vurugu kiasi cha polisi kuingilia kati kwa kutumia mabomu ya machozi na kuwatawanya wananchi waliokuwa wamekusanyika maeneo mbali mbali .

Kutokana na vurugu hizo mpaka wa Tunduma ambao unaingia nchi za kusini mwa Tanzania ulifungwa pamoja na magari yaliyokuwa yakitoka Sumbawanga pia yalizuiwa kuendelea na safari hadi hali hiyo ilipotulia mida ya saa 8 mchana baada ya kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athuman kufika eneo hilo.

Source: Mpekuzi

HII NDO HALI HALISI


TUNDUMA.jpg


408045_320549398071314_843401007_n.jpg



DSC00354.JPG





DSC00440.JPG

Wanafunzi wakisindikizwa na jeshi la polisi kurudi majumbani mwao
 
Na lile agizo la juzi kuwa wakristo wachinje limetoka wapi? Hata hivyo wakristo wote wakae wakijua hawajafunja sheria yoyote katika taifa hili, Kwa kuchinja kwani hakuna kifungu chochote cha katiba kinachoeleza na kufafanua kwa kina kuhusu uchinjaji,
 
Maduka yote yamefungwa matairi yanachomwa barabarani, magari ya polisi yanamwagwa mitaani.Chanzo cha vurugu ni mkuu wa wilaya kuzuia wakristu kuchinja na kwamba wanaoruhusiwa ni waislam tu.!!

ni lazima tutetee imani yetu ila kwa kufunga na kusali zaidi na si vurugu.
 
Wakamatwe mara moja. Jela mwaka with no option for fine!
 
Mhhhhhhh huyu naye,anawakataza kwanini mshenzi tuu,sasa nchi hii haina dini ni bora kila mtu achinje anavyojisikia kuepusha hizi vurugu.:yo:
 
Eleza vizuri mkuuu!
Hili ni jambo zito kama ni la kweli!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom